Sherehe ya Wamisri kwa Eid Al-Fitri

Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud
wakati wa kuingia Uislamu nchini Misri mnamo karne ya saba AD, Eid Al-Fitri ikawa mojawapo ya Sikukuu muhimu zaidi za kidini zinazosherehekewa na Wamisri, ambayo shughuli zake kati yao zilitofautiana na ulimwengu wa Kiislamu kote , haswa katika enzi mbili za Fatimid na Mamluk.
Maandalizi ya Eid Al-Fitri yalianza mwishoni mwa mwezi wa Rajab, ambapo serikali iliainisha kiasi cha dinari 20,000 zinazopa "Dar Al-Fitri", iliyoundwa na Wafatimi kwa ajili ya kupika keki na peremende,ambapo wanapika keki zinazojazwa kwa karanga pamoja dinari za dhahabu , na dinari moja ilikuwa imetosha gharama za familia kwa miezi mitatu kwa uchache, vilevile Dar Al-Fitri ilikuwa ikisambaza keki na peremende kwa wakuu na umma kwa ujumla kabla ya Sikukuu, na baadhi ya vipande vilipelekwa nchi jirani pia. pamoja na hayo , kiasi kikubwa cha pesa kilikuwa kiimeainishwa ili kutengeneza " mapambo " nazo ni nguo za pamba na hariri zilizoshonwa kwa dhahabu na Fidha na hizo zilisambaza kwa watu kiasi kwamba wamisri waliita Eid Al-Fitri "sikukuu ya mapambo."
Mnamo wiki ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, misikiti hupambwa na kuwashwa kwa taa, na muadhini huimba kasida - kabla ya kila adhana - kasida za "Tawshih za Ramadhani" kwa kuaga mwezi mtukufu, wakisema:
“Mwenyezi Mungu hajaweka mwezi mtukufu hukumbukwa zaidi yako ewe Ramadhani .. hajaweka mwezi mtukufu hukumbukwa zaidi yako ewe mwezi wa Qur’an.”
Wakati jua linapozama mnamo usiku wa mwisho wa Ramadhani, msafara mkubwa unaoongozwa na hakimu mkuu na anasindikizwa na Mashekh na wakuu wa amri za Kisufi hupanda Mlima wa Mokattam ili kuangalia wa mwezi wa Shawwal, hadi ikiwa mwezi wa mpevu ikithibitishwa, misikiti inatangaza kuwa kesho ni siku ya kwanza ya Eid Al-Fitri.
Kuanzia Asubuhi ya Eid , umati mkubwa wa watu ukisubiri mbele ya kasri ya Khalifa kwa ajili ya msafara wake ili kwenda kuhudhuria swala ya Eid, ambapo msafara wa idadi mkubwa ya wana wa mfalme na askari huelekea uwanja wa swala ya Eid . ambayo kawaida hufanyika Bab Al-Nasr, pia ,msafara mwingine unatoka mbele ya nyumba ya imamu wa swala pamoja na masheik, wataalamu na umma kwa uwanja wa swala ya Eid , pindi swala imeisha , msafara wa khalifa unasonga pamoja na kundi la wapiganaji na wakuu, na vikundi vya Sufi, tembo na twiga pia hushiriki kwenye masindikizo haya, hadi uwanja wa sherehe kwa sikukuu ambapo " Sumat" inafanyika, ambayo ni Karama ya chakula kubwa inayoendelea kutoka asubuhi hadi sala ya adhuhuri na hudumu kwa muda wa siku tatu, na huandaliwa kwa Kiasi kikubwa cha chakula, kinywaji, keki na pipi, na wakuu na mafaqihi wanampongeza khalifa kabla ya kukaa mezani, na khalifa anawapa zawadi na dinari za dhahabu , pia hurusha dinari za dhahabu dirishani mwa jumba lake kama mkono wa eid kwa watu, ambayo ilijulikana kama "Jamaika" . vilevile , anaamrisha kutoa msamaha kwa wafungwa katika tukio hili la heshima, na Watu hutoka ili kusherehekea sikukuu kwenye bustani na matembezi kwenye ufuo wa Mto Nile, ambapo muziki, wanasarakasi, wacheza muziki, na vikao vya burudani vilieneza kufurahia Eid iliyobarikiwa.
Vyanzo
Tovuti ya Makumbusho ya Ustaarabu ya Misri.