Kitivo cha Masomo ya Juu ya Kiafrika

Kitivo cha Masomo ya Juu ya Kiafrika
Kitivo cha Masomo ya Juu ya Kiafrika

Wengi hukielezea kama lango la Misri kuelekea Afrika, na Watafiti na wahusika wa uwanja wa kiafrika wanakielezea kama "Mwelekeo na Nyumba ya Waafrika wanaohangaika Elimu na Utamaduni kwa utaifa au hata itikadi zao", mwaka huu kinaingia mwaka wake wa mtano baada ya sabini, kilianzishwa  mnamo 1947 , kinatengwa na kitivo mama  kwa karibu miaka 39, wakati ambapo  Chuo Kikuu cha Kairo kilianzishwa mnamo 1908 . Kwa sasa ni Kitivo cha Mafunzo ya Kiafrika ya juu - zamani Chuo cha tafiti na Mafunzo ya kiafrika.

Asili ya Kitivo cha Masomo ya Juu ya Kiafrika ilianzia mwaka 1947 , ambapo kilianzishwa chini ya jina la Taasisi ya Mafunzo ya Sudan, ambayo wakati huo ilihusishwa na Kitivo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Kairo na kilijumuisha idara mbili tu: Historia na Jiografia. Mnamo 1954 jina la taasisi hiyo lilibadilika kuwa Taasisi ya tafiti za Kiafrika, basi jina hilo lilibadilika tena mnamo 1970 na kutolewa kwa Uamuzi wa Jamhuri kwa kuanzisha Taasisi ya tafiti na Mafunzo ya Afrika, ambapo idara nne mpya ziliongezwa nazo ni: Siasa, Uchumi, lugha za Kiafrika, Rasilimali asili na Elimu ya Binadamu.

 

Mnamo Desemba 3, 2018, Waziri Mkuu alitoa uamuzi wa kubadilisha Chuo cha tafiti na Mafunzo ya Kiafrika na kuwa Kitivo cha Masomo  ya Juu ya kiafrika, na hii ilikuwa sanjari na matayarisho ya Misri kuchukua Urais wa Umoja  wa Afrika na imani ya uongozi wa kisiasa uliowakilishwa na Rais  Mheshimiwa, Abd El-Fatah El-Sisi wa umuhimu wa jumba hili la zamani la Kiafrika katika kuboresha na kuimarisha mahusiano ya Misri na Afrika kupitia Elimu, sayansi na nguvu nyoro.

Kuna takwimu na dalili zinazothibitisha msimamo wa upainia kwa jumba la kipekee la Kiafrika.Tukumbuke kutoka kwake kwamba maelfu ya wanafunzi kutoka Misri na nchi mbali mbali za Kiafrika wamehitimu kutoka kwake, na miongoni mwao walioshikilia nafasi za juu za uongozi katika nchi zao baada ya kubeba bango la maarifa kutoka Misri. Kwa mfano, idadi ya wanafunzi waliojiunga na Kitivo mwaka huu ni takriban 617 tu katika mipango ya masomo (Diploma maalum - Uzamili - Uzamivu), kwa kuongeza wanafunzi 100 waliojiunga na diploma za kiufundi, na 593 wameshapata digrii za Uzamili na Uzamivu katika nyanja tofauti mnamo miaka mitatu iliyopita.

 

Kitivo hiki ni pamoja na maktaba kubwa ya kipekee iliyo maalum katika mambo yote ya Kiafrika ambayo ina maelfu ya marejeleo, vitabu, nakala na mamia ya Tafiti za Uzamili na Uzamivu , wakati ambapo maktaba hiyo inajumuisha nadharia 1267 za  Uzamili na nadharia 771 za Uzamivu, ikimaanisha kuwa ina nadharia za kisayansi 2038, pamoja na upitishaji wa nakala 134 za Kiarabu na nakala za kigeni za 117 , na vitabu na marejeleo takriban 20338 katika taaluma zote na nadharia na kutumika kwa sayansi ya masomo ya Kiafrika. Kitivo hiki pia kinajumuisha kikundi cha maprofesa wakubwa na wataalamu katika masuala anuwai ya Kiafrika, maprofesa hawa wanawasilisha masomo yao na utafiti wa kisayansi ili kuhudumia masuala ya Kiafrika na kutoa masuluhisho kwa shida zinazozikabili nchi na watu wa bara hilo. Ikiwa tutafuatilia uzalishaji wa kisayansi wa wanachuoni wa Kitivo wakati wa miaka mitano iliyopita tu 2015-2020, tutapata kuwa idadi ya utafiti iliyochapishwa kimataifa na ndani katika mambo anuwai ya Kiafrika yalifikia  tafiti 700 za kimataifa na ndani.

 

Kwa kuongezea, Kitivo hicho ni pamoja na mamia ya wanafunzi waafrika, sawa iwe wanasoma katika idara mbali mbali za Kitivo hicho katika Diploma,  Uzamili, na Uzamivu au wanafunzi waliosajiliwa na Ofisi ya Masuala ya Wanafunzi waafrika katika Chuo Kikuu cha Kairo na Chama cha Mawasiliano cha Wanafunzi wa Kiafrika  wanaoshiriki katika shughuli zote za Afrika na vikao vilivyoandaliwa na Kitivo hicho.

 

Kitivo cha Masomo  ya Kiafrika pia kina jukumu muhimu katika kuelimisha na kuhimiza jamii ya kienyeji na ya Kiafrika juu ya masuala  yote ya Kiafrika Katika suala hili, Kitivo kilipanga shughuli za bure za masomo na semina kama (Afrika ni Binadamu na Mahali 1) na (Afrika ni Binadamu , Mahali na Changamoto 2) na kozi zingine za mafunzo zilizopangwa na ofisi ya utunzaji wa masuala ya Wanafunzi waafrika, Chuo Kikuu cha Kairo, Kituo cha Habari na Mashauriano ya Afrika, au Programu ya Kuijenga uwezo na Mafunzo ya Afrika.

 

Kitivo hicho pia kilifanya shughuli nyingi za kimataifa na za mitaa, Mipango, mikutano na semina zilizolenga kutafakari shida na masuala ya  Kiafrika na kutoa maoni na masuluhisho kwao .. Kitivo hiki pia kilipanga mradi wa viongozi 1,000 wa Kiafrika, ambao uliwasilishwa kwa zaidi ya wanafunzi 5,000 kutoka nchi 35 za Kiafrika na walipata mafunzo kwa mwaka mzima na wataalam na maprofesa kutoka Kitivo katika taaluma zote. 

 

Kitivo cha Masomo ya Kiafrika  - hakika - ni  dirisha la Misri barani Afrika, lango lake kuu kwa bara lake la Afrika, na kiunga kinachounganisha Misri na ndugu zake wa kiafrika.