Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa wazindua Kikao cha Kwanza cha "Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa"

Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa wazindua Kikao cha Kwanza cha "Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa"

Imetafsiriwa na/ Mratibu wa Lugha ya Kiswahili "Mervat Sakr"

Jana jioni, Julai 8, 2024, Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa (Harakati ya Nasser kwa Vijana- Idara ya Lugha ya Kiswahili) uliandaa kikao cha kwanza cha "Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa" yenye kichwa cha habari "Harakati ya Ufasiri kwenye Ulimwengu wote wa lugha ya Kiswahili", ikiambatana na Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani, Harakati hiyo inayolenga kuangazia jukumu la Misri kwenye harakati za ufasiri barani Afrika. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Dkt. Alaa Salah Abdel Wahed, Mwalimu wa Fasihi ya Kiswahili kwenye Idara ya Lugha na Fasihi ya Kiafrika, Kitivo cha Lugha na Ufasiri, Chuo Kikuu cha Al-Azhar, na Mhadhiri wa Fasihi ya Kiswahili kwenye Idara ya Lugha za Kiafrika, Kitivo cha Al-Alsun, Chuo Kikuu cha Ain Shams.

Mpango huo ulifunguliwa na Mwanaanthropolojia na Mwanaharakati wa Kimataifa Hassan Ghazaly kwa kumkaribisha Dkt. Alaa Salah na waliohudhuria, akitangaza uzinduzi wa vikao vya kwanza vya Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa, na akaeleza kuwa kikao hiki kinakuja ndani ya vikao mbalimbali vinavyozungumza Kiswahili, vimevyopangwa kufanyika kila wiki mwezi Julai ili kusherehekea ulimwengu mzima wa lugha ya Kiswahili. Pia aliwaalika watazamaji kwenye kikao muhimu kitakachofanyika kesho, Alhamisi. Alitaja Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, uliozindua mpango huo kwa mara ya kwanza wakati wa janga la Korona (Covid-19), akisisitiza haja ya mshikamano wa kibinadamu.

Ghazaly alisema kuwa Mpango wa Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa unakuja kama msaada wa mpango wa "Vipindi vya Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa", uliozinduliwa na mtandao mnamo mwaka 2020 chini ya jina la "Global Citizen Talks", na mpango huo unalenga kukuza mazungumzo na uelewa kati ya vijana kutoka tamaduni tofauti na asili duniani kote, na kuunda jukwaa la wazi la majadiliano na kubadilishana kiakili kuhusu masuala ya mshikamano wa kimataifa, na pia inatoa fursa kwa vijana wa Misri na wanafunzi wanaojifunza lugha kufanya mazoezi ya lugha yao ya kujifunza na watu wa asili, iwe Asia, Ulaya, Afrika na Amerika ya Kusini, na mpango huo umepangwa kuandaa lugha zao za kujifunza na watu wa asili, iwe Asia, Ulaya, Afrika na Amerika ya Kusini, na mpango huo umepangwa kuandaa lugha yao ya kujifunza na watu wa asili, iwe Asia, Ulaya, Afrika na Amerika ya Kilatini, na Mpango huo umepangwa kuandaa majadiliano kadhaa ya jopo katika lugha tofauti.

Katika muktadha huu, kikao kilijumuisha mada kadhaa, hasa umuhimu wa kujifunza lugha na Ufasiri, kwani Ufasiri ni chombo muhimu kwa kubadilishana tamaduni na ustaarabu kati ya watu. Aidha Dkt. Alaa alisisitiza jukumu la fasihi ya Kiswahili katika kuelewa utamaduni wa watu wa eneo hilo, kwani fasihi ni kioo cha jamii na njia ya kuelewa saikolojia ya watu, akieleza kuwa Ufasiri wa kazi za fasihi uwe maandishi au simulizi, unachangia kuimarisha utambulisho wa kitamaduni, kitaifa na Kiafrika kwa wazungumzaji wa Kiswahili.

Katika muktadha unaohusiana, Dkt. Alaa alimshukuru Mwanaanthropolojia na Mwanaharakati wa kimataifa Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, kwa juhudi zake kubwa kuelekea bara la Afrika na nia yake ya kueneza lugha ya Kiswahili na kusherehekea Siku ya Kiswahili Duniani, akisifu juhudi za Harakati ya Nasser kwa Vijana kwenye kueneza na kupendezwa kwa lugha ya Kiswahili kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri wanaojifunza lugha hiyo kuhusu kutafsiri na kuandaa warsha, semina na matukio yanayochangia kukuza ujuzi na maarifa ya watafsiri, na alipongeza juhudi za lango la "Makala na Maoni", ambayo huwapa wanafunzi fursa ya kuandika makala kwa Kiswahili kunaongeza uwezo wao wa kuandika na michango ya kifikra, kuwapa uhuru wa kuwasilisha maoni na mawazo yao.

Dkt. Alaa alieleza kuwa harakati za ufasiri kati ya lugha za Kiarabu na Kiswahili ni tajiri sana, akieleza kuwa mwanzo wa tafsiri uliwakilishwa katika uzalishaji wa Kiislamu kutoka Kiarabu hadi Kiswahili, na ulianza kabla ya kipindi cha ukoloni. Aliasisitiza kuwa harakati za ufasiri kwa wakati huu zinastawi na zinahitajika katika nyanja zote, jambo linalochangiwa na uenezaji mpana wa lugha ya Kiswahili na shughuli za harakati za ufasiri.

Kikao hicho kilisimamiwa na Mtafiti na Mtafsiri Mervat Sakr, Mtafiti kwenye Shahada ya Uzamili kwenye lugha za Kiafrika, Idara ya Lugha ya Kiswahili, na Mratibu wa Lugha ya Kiswahili kwenye tovuti rasmi ya Harakati ya Nasser kwa Vijana, na Alipokea tuzo ya Kituo cha Kitaifa cha Ufasiri mnamo mwaka 2023.

Ni vyema kutajwa kuwa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa ni jukwaa linalojumuisha miradi, mipango na programu mbalimbali kwenye nyanja za vyombo vya habari, utamaduni, vijana, uongozi, na mahusiano ya kimataifa, na inalenga kuimarisha jukumu la Misri na dhana ya mshikamano kati ya watendaji wa kijamii na wanasiasa vijana katika ngazi ya kimataifa, hasa Ulimwenguni Kusini, na pia inalenga kufikia haki na demokrasia katika mahusiano ya kimataifa, miradi ya mtandao huo imefaidika hadi sasa zaidi ya vijana wa kiume na wa kike elfu 18 duniani kote, kwani inafanya kazi hasa kukuza maadili ya amani, mshikamano, na uelewa kati ya tamaduni tofauti.