Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni Makamu wa mwenyekiti wa Umoja wa Kitaifa wa Vijana wa Jamhuri ya Sudan Kusini 2022

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni Makamu wa mwenyekiti wa Umoja wa Kitaifa wa Vijana wa Jamhuri ya Sudan Kusini 2022

Dkt. Benjamin Bang Bang, mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Katibu Mkuu wa zamani wa Vijana wa Taifa wa Sudan Kusini, aliteuliwa kuwa Makamu wa Mwenyekiti kwa amri ya Bw. «Gula Buyoy» Gola, mwenyekiti wa Umoja wa Kitaifa wa Vijana Sudan Kusini, na hiyo kwa mujibu wa ufanisi na juhudi za maendeleo, imani kubwa iliyofurahishwa na Mamlaka ya kiutendaji au Baraza la Umoja.

Katika muktadha huo, ustadi na athari za jamii za "Benjamin Bang Bang" katika jamii ya Sudan Kusini zilijitokeza kupitia uwezo wake wa hali ya juu wa kubuni na kufanya utafiti na masomo ya uchunguzi, kutathmini mahitaji, pamoja na kukusanya na kuchambua data kwa ufanisi na makini, licha ya uwezo wake wa kufanya mashirikiano na taasisi za kitaifa na kuzindua miradi na programu za maendeleo, hata katika maeneo yenye migogoro ambapo hali ngumu inayatawala, kwa imani yake kwamba hilo lingetuliza makali ya mgogoro huo na kuchangia katika kurejea Amani na Usalama hatua kwa hatua.

"Benjamin Bang Bang" alihitimu Shahada ya Kwanza ya Tiba ya Mifugo katika Chuo Kikuu cha Bahri, Khartoum, Sudan, na kupata Shahada ya Uzamili ya Sayansi ya Maliasili na Masomo ya Mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Juba, Sudan Kusini, kisha akasomea sheria katika Chuo Kikuu cha Juba, na kwa sasa anasomea shahada ya Uzamili katika Huduma ya umma, katika Kitivo cha Huduma ya Umma, Chuo Kikuu cha Juba, Sudan Kusini.

«Benjamin Bang Bang» alipata tuzo kemkem za kitaifa kwa kusifu juhudi zake, na pia alishiriki, kama mwakilishi wa Jamhuri ya Sudan Kusini, katika vikao kadhaa vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika ujumbe wa Sudan Kusini katika mkutano wa Kairo wa Kitaifa wa kwanza wa Vijana wa Sudan Kusini, mnamo  Aprili 2021 nchini Misri, ndani ya mradi wa Umoja wa Bonde la Nile - maoni ya Baadaye.

Kwa upande wake, Benjamin Bang Bang, mratibu wa Harakati ya Nasser kwa Vijana nchini Sudan Kusini, alieleza furaha yake kutokana na imani aliyo nayo miongoni mwa vijana wenzake na watoaji wa maamuzi, akisisitiza kuwa atafanya kila awezalo katika kazi kwa ajili ya maendeleo, ukarabati, urekebishaji, uwezeshaji wa vijana, kuhimiza ushiriki wao katika kazi za umma na kuandaa kada wenye uzalendo wanaochangia kuinua taifa, Jamhuri ya Sudan Kusini.

Dkt. Bang Bang, akisifu Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akisema: "Napenda kuwashukuru kwa kujitolea na kazi yenu ya juu chini mliyoonesha kupitia programu ya Udhamini, taasisi na uzoefu wa Misri ulioshiriki nasi, na pia napenda kuchukua fursa hii ili kukupa Shukrani zangu za dhati kwa usaidizi wenu unaoendelea hata baada ya kumalizika, na ninatazamia kwa hamu kupokea usaidizi huo huo tena katika uteuzi wangu mpya.”

Kwa upande wake, Hassan Ghazali Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser ya Kimataifa kwa Vijana alisifu nguvu ya Diplomasia ya Vijana wa Jamhuri ya Sudan Kusini, akisema: "Nilishuhudia kwa undani ufanisi wa vijana wa Jamhuri ya Sudan Kusini, utamaduni wao mkubwa na uwezo wao wa kujadili na kusimamia majadiliano katika programu kemkem za bara na za Kimataifa iliyozinduliwa."

Na akiongeza kuwa anaamini kabisa ya uwezo wa vijana hawa katika Jamhuri ya Sudan Kusini kwa kuongoza maendeleo ya nchi ndugu kwa mwamko na uelewa wa ukubwa na uwezo wa nchi, licha ya ufanisi wa ushawishi wao si tu katika mazingira yao na jamii, bali hata majukumu yao maarufu katika kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya Misri na Jamhuri ya Sudan Kusini, kwa njia yanayopandisha kiwango cha mahusiano ya pande mbili kati ya nchi hizo ndugu mbili.

Ghazali alihitimisha maneno yake kwa akisisitiza kuweka nafasi  kubwa zaidi kwa vijana wa Jamhuri ya Sudan Kusini katika programu nyingi ya mafunzo na ukarabati wa Bara anaozindua, au hata anasimamia utekelezaji wake, kwa kuimarisha ushiriki wao na kuwawezesha kukutana na watoaji wa maamuzi kwenye njia moja ya mazungumzo, akisheria kwamba hii ni sehemu ya maoni ya Nchi ya Misri na nia yake ya kuunga mkono wa mahusiano ya pande mbili na nchi za Bonde la Nile, haswa nchi za Tambarare ya Nile.