Fouad Haddad Mwenye Kuleta Matumaini na Mshairi wa Lugha ya Mtaani ya Kimisri

Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
“ Kila Sehemu katika nchi yangu ni Sehemu ya ini yangu na pia ni Sehemu katika wimbo “ , Fouad Haddad ni mshairi wa lugha ya mtaani ya kimisri aliyepata lakabu ya "Mshairi wa Raia" ambapo yeye ni mwanzilishi wa kwanza wa ushairi wa lugha ya mtaani huko nchini Misri na ulimwengu wa kiarabu, na mojawapo wa watetezi wakuu wa suala la Palastina katikati ya karne ya 20.
Fouad Salim Amin Haddad aliyepata lakabu ya mshairi wa lugha ya mtaani ya kimisri, amezaliwa mnamo Oktoba 30 ,1927, katika kitongoji cha Daher, kairo, mama yake alitoka Syria lakini amezaliwa kairo, na baba yake aliyetoka Lebanon halafu alihamia Misri ili kufanya kazi kama Mhadhiri Mwandamizi wa Hisabati za kifedha, kwenye Kitivo cha Biashara chuo kikuu cha Fouad Alawal , na hadi sasa vitabu vyake vinafundishwa , mshairi huyo wa lugha ya mtaani amesoma katika shule mbili za kifaransa Al-Farrer na Lycee Francias na alifahamu vizuri urithi wa ushairi kwenye maktaba ya baba yake, halafu akajua fasihi ya kifaransa kutokana na usomaji wake wa lugha ya kifaransa jambo ambalo lilimwezesha kujua baadhi ya kazi zilizofasiriwa kuelekea kifaransa , ambapo ushairi wake wa kwanza ilikuwa na kichwa cha " Wahutu nyuma ya reli " , na baada ya ushairi huu amekuwa mmoja wa mashairi.
Na miongoni mwa kazi zake za kipekee programu maarufu zaidi ya runinga (kutoka kwa ubunifu na matendo ya vizazi), ambapo aliitangaza programu hiyo kupitia vipindi 30 mwaka 1969 kwa sauti ya mtungaji wa muziki Sayed Mekawy , aliyeimba wimbo wake maarufu (ardhi inaongea kiarabu), na pia aliandika "Elmesaharati" kwa Sayed Mekawy mwaka 1964, pamoja na shairi nyingi za utendi , kama ushairi muhimu zaidi wa Adham Elsharkawy " kifo cha Gamal Abd Elnasser" mwaka 1982 , na pia (Elshater Hasaan ), na ushairi wake wa mwisho alioandika ulikuwa (kondoo wa Palastina) , alichapisha mwaka 1985, na baada ya hapo alifariki novemba mnamo mwaka huo huo, kwa umri wa miaka 58 , akiacha safari ndefu nyuma , safari ambayo itakuwa kama ushahidi mkubwa wa ufadhili wake wa kuwahamasisha washairi watakaojitokeza, wa lugha sanifu au ya kimtaani, ambapo lugha ya mtaani ya kimisri ndani ya shairi zake haijawa kinyume cha kiarabu sanifu, bali zinafanana huwezi kuzifananisha.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy