Mohamed Faik
Mohamed Faik ni mwananchi mmisri.
Amezaliwa tarehe 28, mwezi wa kumi na moja, mwaka 1929 mjini Mansoura(Mkoa wa El-Dakahlia). Alisomea kitivo cha Biashara, kisha alipata kozi kadhaa zinazohusisha ulinzi wa angani nchini Uingereza mwaka 1951.
Maisha yake ya kikazi :
■ Alipewa jukumu la katibu mkuu wa Shirika la Kiarabu linaloshughulika na kutetea haki za binadamu kuanzia mwaka 1986 hadi mwaka 2008, naye ni mmoja wa wanachama wa baraza la wadhamini wa shirika hilo kuanzia mwaka 2008 mpaka sasa.
■ Mkuu wa baraza la waaminifu wa gazeti la El-Arabi.
■ Alikuwa mkuu wa ofisi ya Rais wa zamani wa Misri Bw. Jamal Abdel Nasser inayoshughulikia mambo ya kiafrika kisha alipandishwa cheo, akawa mshauri wa Rais anayeshugulikia mambo ya Afrika na Asia.
■ Alikuwa waziri wa vyombo vya habari wa Misri kuanzia mwaka 1966 hadi mwaka 1970.
■ Aliteuliwa ili kushughulikia nafasi ya waziri wa mambo ya nje mwaka 1970.
■ Alikuwa makamu wa mwenyekiti wa kamati ya Misri ya mshikamano wa Afrika na wa Asia pia.
■ Ni mkuu na mmliki wa shirika la Uchapishaji la El-Arabi lililojengwa mnamo mwaka 1981.
■ Anaongoza baraza la kitaifa la haki za binadamu kuanzia tarehe 22, mwezi wa Agosti, mwaka 2013 hadi sasa.
Maelezo ya jumla kuhusu Mohamed Faik :
Mohamed Faik ni mwanasiasa maarfu wa kitaifa ambapo alipoteza umri wake akiutetea uhuru nchini Misri na nje ya Misri pia. Mwanasiasa huyo alikuwa na jukumu la kukuza harakati za ukombozi za kimataifa, pia alikuwa kama ishara ya harakati hizo barani Afrika ambapo alikuwa kama mkono wa Rais Jamal Abd El-Nasser barani humo. Aidha, alifanya kazi bega kwa bega na Rais wa zamani wa Misri Jamal Abd El-Nasser, pamoja na hayo alipewa majukumu kadhaa ya kisiasa na ya kiwizara kwenye kipindi cha utawala wa Rais Jamal Abd El-Nasser. Alikuwa mshauri wa mambo ya kiafrika na baadye alipandishwa cheo, akawa mshauri wa mambo ya kiafrika na kiasia. Alichangia kwa kiasi kikubwa katika mapambano ya ukombozi na alilaani vikali suala la ubaguzi wa rangi barani humo. Pia alifanya urafiki na viongozi wa harakati ya ukombozi wa kitaifa ulimwenguni na viongozi wa harakati ya kutoungana na pande zozote kama Nelson Mandela, Kwami Nkroma, Andira Ghndi, Pandaranika, Videl Kastro, Arnsto Guivara. Mara nyingi mahojiano yake yameathirika na wale viongozi kwa upande wa uundaji wa mtazamo wa kina kwa harakati ya ukombozi wa kitaifa ulimwenguni.
Aliendelea na majukumu yake kama waziri wa vyombo vya habari katika kipindi cha utawala wa Rais Anwar El-Sadat, lakini alijiuzulu mwaka 1971 baada ya kulalamika juu ya mielekeo ya kisiasa ya Rais Anwar El-Sadat inayohusiana na kufuta madhara ya uchokozi wa Israel mwaka 1971. Jambo ambalo lilimweka kifungoni na kumlazimisha apoteze muda wa miaka 10 ya umri wake kifungoni ambapo alituhumiwa na tuhuma za bandia tu kama {jaribio la kuipindua/kuiangusha serikali}.
Alipata umaarufu mkubwa kutokana na misimamo yake iliyodhihirisha ujasiri wake ambapo wakati wa uchokozi wa nchi tatu {Uingereza-Ufaransa-Uyahudi} dhidi ya Misri mnamo mwaka 1956, alivaa nguo za wavuvi na kujipenyeza mwenyewe kati ya upinzani wa kiraia dhidi ya majeshi ya Uingereza mjini Port-Said. Na mnamo mwaka 1976 alipinga uamuzi wa Rais Anwar El-Sadat unaompa Mohamed Faik uhuru wake kamili kwa sharti moja tu, sharti lililokuwa ni kumwomba Rais Anwar El-Sadat amsamehe kwa kosa lake hilo alilolitenda, lakini Mohamed Faik alikataa kufanya hivyo, kwa sababu yeye mwenyewe hakufanya kosa lolote ili kuomba msamaha, akaishi miaka mitano mingine kifungoni. Na baada ya miezi michache tu tangu kuachwa huru, alikamatwa tena akiwa pamoja zaidi ya viongozi wengine 1500, lakini mara hii viongozi hao wote pamoja na Mohamed Faik hawakuachwa huru ila baada ya Rais Anwar El-Sadat kuuwawa mwaka 1981 wakati wa maadhimisho ya ushindi wa majeshi ya Misri dhidi ya Israel kwenye vita ya Oktoba.
Umri wake haukupotezwa bure kifungoni ambapo aliandika kitabu cha Abd El-Nasser na mapinduzi ya kiafrika kwenye kipindi cha kifungo chake.
Mafanikio yake yaliyo muhimu zaidi
- Aliunda programu ya kimuziki kwenye redio.
- Aliunda programu za kielimu kwenye kituo cha televisheni pamoja na kituo cha uandishi wa habari.
- Mwenye wazo la kuunda cheo cha Mzungumzaji Rasmi kwa mara ya kwanza nchini Misri.
- Kazi zake zilikuwa nyingi sana, kwa mfano {utafiti kuhusu Afrika na haki za binadamu, tafiti kuhusu Rais Jamal Abdel Nasser na utafiti kuhusu mapinduzi ya kiafrika.