Maadhimisho ya Siku ya Uokoaji Tunisia

Maadhimisho ya Siku ya Uokoaji Tunisia

Imetafsiriwa na/ Habiba Mohammed 
Imeharirwa na/ Mervat Sakr 

Mnamo tarehe nane ya Februari 1958, vita vya Uokoaji vilianza nchini Tunisia baada ya uvamizi wa Ufaransa katika kijiji cha Sakia Sidi Youssef, ambacho kiko kwenye mpaka wa Tunisia na Algeria,  uliolenga taasisi kadhaa za mitaa na kusababisha vifo vya mashahidi kadhaa wa Algeria na Tunisia. Mnamo Julai 17 mwaka huo huo, serikali ya Tunisia iliamua kufanya kazi ya kuondoa mabaki ya majeshi ya Ufaransa kutoka kambi ya Bizerte kwa njia za kidiplomasia, lakini hali ilirudi kwenye mgogoro mnamo Julai 1961, na mnamo mwezi wa nne wa mwezi huo huo, ofisi ya kisiasa ya chama tawala cha Katiba Huru iliitisha vita vya Uokoaji, na siku mbili baadaye Rais Habib Bourguiba alituma mjumbe maalumu kutoka kwake kwa Rais wa Ufaransa Charles de Gaulle na Ujumbe wa kumkaribisha kwenye mazungumzo makubwa.

Mnamo Julai 23, 1961, usitishaji mapigano ulitangazwa kuacha fursa ya mazungumzo, yaliyomalizika na Ufaransa kutangaza kuondolewa kwa vikosi vyake kutoka mji wa Bizerte na kuhamishwa kwa kambi ya jeshi la majini kutoka kwake, na mnamo tarehe kumi na tano ya Oktoba 1963, Admiral wa Ufaransa Viviay Menad aliondoka mji huo akitangaza mwisho wa Ukoloni wa Ufaransa wa Tunisia, ulioanza tarehe kumi na mbili Mei 1881, ambapo ilidumu miaka 82.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy