Siku ya Afya na Usalama wa Kazi Duniani

Siku ya Afya na Usalama wa Kazi Duniani

Tarehe ishrini na nane, Aprili kila mwaka, Dunia huadhimisha Siku ya Afya na Usalama wa kazi Duniani, ambayo ni kampeni ya kimataifa inayoanzishwa na Shirika la Kazi Duniani kila mwaka, na hiyo ili kuzuia ajali za kazini, likitegemea nguvu zake tatu: mashirika ya waajiri na mazungumzo ya kijamii, serikali, mashirika yanayowakilisha waajiriwa .

Shirika la Kazi Duniani liliadhimisha Siku ya Usalama na Afya ya Kazi kwa mara ya kwanza mnamo 2003, na tangu wakati huo linaendeleza shamrashamra za siku hii ili kuongeza utamaduni wa kimataifa kuhusu njia za kuzuia magonjwa na ajali mbalimbali ambazo wafanyakazi wanakabiliana nazo katika kazi zao za kawaida za kila siku. Pia, Shirika lilichagua siku hii kwa kumbukumbu ya waathirika wa ajali za kazini mnamo wa mwaka wa 1996.