Maadhimisho ya kuanzishwa kwa UNICEF
Imetafsiriwa na/ Meret Magdy
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Tangu kuanzishwa kwake, UNICEF imekuwa nguvu isiyoweza kuzuilika, na tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ikipigania mabadiliko katika maisha ya watoto duniani kote, bila kujali utambulisho wao, popote wanapoishi, wakati ambapo shirika hilo limekuwa mstari wa mbele wa migogoro ya kibinadamu, migogoro ya silaha na majanga ya asili, kukabiliana na mamilioni ya watoto na kutetea haki yao ya kuishi, na kujitolea kwake, washirika na utaalamu wa shamba kufikia zaidi ya nchi na maeneo ya 191.
Mnamo tarehe Septemba 11, 1946, UNICEF ilianzishwa kwa azimio la 57 (I) la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kutoa vifaa na msaada kwa watoto baada ya Vita vya Pili vya Dunia, na jina lake la awali lilikuwa Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa kwa Watoto, kama mfuko wa misaada ya muda wa Umoja wa Mataifa: Uhuru kwa wote, usawa kwa jamii zote.
Mnamo mwaka 1956, shirika hilo lilitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel.
Kamati ya tuzo hiyo ilitangaza kuwa shirika hilo lilitimiza masharti ya mapenzi ya Nobel na liliweza kukuza udugu miongoni mwa mataifa, na kuongeza kuwa UNICEF inatambua kuwa watoto ndio ufunguo wa mustakabali, na kuisifu kwa maandishi yanayosomeka: "Kuelewa lugha ya UNICEF ni jambo lisiloweza kuepukika, na hata watu wahafidhina zaidi wanaweza tu kukiri kwamba kazi ya UNICEF imeonyesha kuwa huruma haiwezi kufunga mipaka yoyote ya kitaifa."
Kauli mbiu ya kwanza ya UNICEF mnamo mwaka 1953 ilikuwa "Mtoto anayekunywa glasi ya maziwa", ikionesha shughuli kuu ya shirika hilo wakati huo: kutoa maziwa kwa watoto. Wakati wa kuhifadhi vipengele vya nembo ya Umoja wa Mataifa iliyokuwa msingi, kama vile tawi la mzeituni na sura ya ulimwengu kwa nyuma, na kisha nembo ilibadilika kuwa aina ya "mama aliyembeba mtoto wake" kama UNICEF ilipanua mtazamo wake ili kujumuisha mahitaji zaidi ya watoto, na hii pia ilihusishwa na kupitishwa kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto mnamo mwaka 1959, ulioelezea haki za mtoto kwa ulinzi, elimu, huduma za afya, malazi pamoja na lishe bora, na ishara ya ulimwengu inayowakilisha mama anayelea mtoto wake inaashiria matumaini, usalama na furaha. Hii ndio UNICEF inataka kuwapa wazazi na watoto wao, kuleta nguvu na shauku yao, kuonyesha matumaini ya UNICEF na matokeo inayotaka kufikia kwa kila mtoto.
Hivyo, lengo la UNICEF katika miaka iliyopita limekuwa kupeleka meza, iliyopambwa na vitu vyote vizuri ambavyo asili hutoa, kwa watoto wote wa ulimwengu, na kwa sababu hii shirika linachukuliwa kuwa sababu ya umuhimu mkubwa.
Mnamo mwaka 2016, Umoja wa Mataifa uliidhinisha maneno "kwa kila mtoto" kama ishara ya mkakati wa UNICEF, pamoja na jukumu la kimataifa la UNICEF la kulinda haki za watoto kila mahali, linalojumuisha dhamira ya shirika hilo kutoa umuhimu mkubwa kwa watoto walio katika mazingira magumu zaidi.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy