Video| Muungano wa kitaifa wa Vijana wa Liberia wasifu Harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana
Katika eneo la ufalme wa Morocco, kandokando ya Kongamano la kwanza la ushauri la kila mwaka kwa Vijana waafrika, lililoandaliwa na Muungano wa Vijana wa Afrika, kwa kushirikiana na taasisi kadhaa za bara, ikiwa ni pamoja na APRM, na Shirika la Afrika la ushirikiano kwa ajili ya maendeleo, pamoja na Ufadhili wa Mfalme Mohammed wa sita, Mfalme wa Morocco, na sambamba na maadhimisho ya watu huru kwa kumbukumbu ya miaka sabini ya mapinduzi matukufu ya Julai. "Flomo Mau Maiwo” Naibu wa katibu mkuu wa Muungano wa kitaifa wa vijana wa Liberia, na mhitimu wa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa uongozi wa kimataifa, alitoa pongezi kwa harakati ya kimataifa ya Nasser kwa Vijana kwa kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake.

Katika muktadha unaohusiana, “Mau Maiwo”, mgombea wa karibu wa Urais wa Muungano wa kitaifa wa Liberia, alieleza kuwa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana ina jukumu muhimu katika kukuza ufahamu wa watu wa Afrika kuhusu masuala ya maendeleo na historia ya pamoja, tangu harakati za ukombozi wa kitaifa, akielezea kuwa harakati hiyo ilikuwa na ushawishi mkubwa katika safari yake ya kazi na ushawishi wake wa jamii, akisema kuwa imemfanya awe na nia ya kuwekeza katika nguvu na utashi wa vijana kuhakikisha kuwa mwamko wa Afrika, mikononi mwa vijana.
Aliongeza kuwa Afrika inastahili kutoa zaidi na zaidi ya muda na juhudi katika jaribio la kuhakikisha maendeleo na ustawi wake, na kuweka Amani ndani ya eneo lake, na aliendelea akipendekeza vijana wa bara la Afrika kuzunguka majukwaa ya vijana kama hayo yanayowawezesha kutoa maoni yao, mawazo na matarajio, na yaweza kuelewa vguvu zao na kuziwekeza kwa maslahi ya mustakabali yao, sawa na njia inayofuatwa na uongozi wa kisiasa wa Misri katika nyanja za uwezeshaji wa vijana.
Kwa upande wake, “Hassan Ghazaly”, Mwanzilishi na Mratibu mkuu wa harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana alisisitiza ubora wa mahusiano ya ushirikiano wa kiutamaduni na kisayansi kati ya nchi hizo mbili, ambayo maarufu zaidi ni utoaji wa Misri misaada 12 ya kimasomo kwa ajili ya utafiti wa chuo kikuu kwa Liberia mnamo Mwaka wa kitaaluma wa 2020-2021, pamoja na utoaji wa Al-Azhar Al-Sharif misaada 5 ya kimasomo kwa ajili ya utafiti wa chuo kikuu kwa Liberia, na ushiriki wa maimamu wa Liberia katika kozi za mafunzo kwa maimamu, zillnazofanyika na Chuo cha Al-Azhar Al-Sharif, akiashiria uangalifi wa Misri kujenga uwezo wa binadamu wa makada wa Liberia katika sekta mbalimbali za serikali kupitia mazoezi yaliyotolewa na shirika la Misri la ushirikiano kwa ajili ya maendeleo katika nyanja mbalimbali, akiashiria uangalifu wa Misri katika kusaidia viunganishi vya ushirikiano na Liberia na Kuendeleza mahusiano katika nyanja zote na kuendeleza kutoa Misri kwa aina zote za misaada na tegemezo kwa upande wa Liberia.