Mhitimu wa Udhamini wa Nasser yuko kati ya vijana thelathini wanadiplomasia kwa kiwango cha bara la Afrika ili kupata Shahada ya Uzamili huko Roma

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser  yuko kati ya vijana thelathini wanadiplomasia kwa kiwango cha bara la Afrika ili kupata Shahada ya Uzamili huko Roma

Al-Zubair Al-Barkey, mhitimu wa toleo la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa alichaguliwa kama moja wa vijana thelathini wanadiplomasia kwa kiwango cha bara la Afrika ili kupata Shahada ya Uzamili katika uwanja wa Diplomasia ya umma ya kimataifa na uwanja wa maendeleo endelevu.

Kulingana na ombi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia, Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti (UNITAR) na Chuo Kikuu cha Luiss Guido Carli na Shule ya Luiss ya Utawala ya Italia, ziliingilia ushirikiano wa kuendeleza Uzamili wa kiutendaji wa Kipekee katika diplomasia ya umma ya kimataifa na uwanja wa maendeleo endelevu.

Na hili linazingatiwa kama maendeleo ya kukubali hadi 30 vijana viongozi wa Afrika wenye ujuzi wa hali ya juu ili kupata Shahada ya Uzamili kwa mwaka mmoja huko Roma, mji mkuu wa Italia.

Na Al-Zubair akifuatana na idadi ya watu vijana wanaoidhinishwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi yao au walioteuliwa katika Umoja wa Afrika, Taasisi ya Serikali ya Kimataifa ya Maendeleo (IGAD), Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).