Tuzo ya Dola za Marekani elfu tano kwa Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kuhusu Uadilifu na Kupambana na Rushwa
Imetafsiriwa na: Esmaa Hagag
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Chama cha Jumuiya ya Chad nchini Marekani kimemheshimu mwanaharakati wa Chad Ahmed Haroun Lari, katika Kituo cha Utamaduni cha Al-Mina, kwa "Hali ya Uhuru", yenye thamani ya dola elfu tano za Marekani, tuzo ya uadilifu na mapambano dhidi ya rushwa nchini Chad, tuzo ambayo inawasilishwa kwa mara ya kwanza kwa mwanaharakati wa ndani nchini Chad
Larry, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo la pili, wakati ambapo alijifunza juu ya uzoefu wa Misri katika kujenga, maendeleo, kuimarisha taasisi za kitaifa, na jukumu la vijana katika kupambana na rushwa, pia ni mmoja wa Chad watano waliochaguliwa kwa mafunzo ya kupambana na rushwa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti (UNITAR), iliyofadhiliwa na serikali ya Kijapani.
Kwa upande wake, "Larry" wakati wa hotuba yake, alielezea furaha yake na shukrani kwa tuzo hiyo, akimshukuru mfadhili, akibainisha kuwa anajitolea kwa wanaharakati wote wa asasi za kiraia (wasio wa kisiasa) kama alivyoweka, na kwa kumalizia aliwashukuru kila mtu kwa ujasiri huo, akiwaahidi watazamaji juhudi zaidi, akiwataka kufanya kazi pamoja kwa ajili ya kuinua nchi.