Ronald Edward.. Mshawishi Mkubwa aliyeokoa Uganda
Imefasiriwa na / Fatma Mahmoud
Ronald Edward ni nani?
Ronald Edward Frederick Kimera Mwenda Mutebi amezaliwa mnamo Aprili 14, mwaka 1955. Alisoma kwenye Shule ya Bodo Junior huko Sussex na Chuo cha Bradfield kisha akajiunga kwenye Kitivo cha Magdalene huko Cambridge. Pia ameshawahi kuwa Mhariri Mshiriki wa Jarida la Pan-African Concord na akawa mjumbe wa Kamati Tendaji katika kongamano la taifa la Afrika (ANC) huko London. Baadaye akawa chifu wa ukoo na kiongozi wa kiutamaduni kwa Waganda milioni 7.5 wakati wa kurejeshwa kwa falme za Uganda na baada ya hivyo akawa Mdhibiti wa Ufalme wa Buganda baada ya kifo cha babake mnamo Novemba 21, 1969.
familia yake
Amemwoa Bi. Silvia Nganda - ambaye mwana wa John Mulumba, mwanachama kwenye ukoo wa Omos - hayo mwakani 1999. pia Ana watoto watano (Safio Mwenda, Joan Nasulu, Victoria Nkenzi, Katrina Sarah na Richard Simakukrero).
mafanikio yake
Aliteuliwa kuwa mshauri wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Kifalme cha Mutesa mnamo Aprili 15, 2011. Chuo kikuu hicho kilianzishwa kwa kumbukumbu ya Mutesa wa kwanza wa Buganda, hivyo kwa mujibu wa juhudi zake katika kuendeleza elimu nchini Uganda na ujuzi wake wa kipekee wa kidiplomasia katika kuwasiliana na Waingereza, wahusika wa Wafaransa na Waarabu mwishoni mwa karne ya 19.
anazingatiwa pia ni balozi wa kutokomeza UKIMWI kati ya wanaume katika mashariki na kusini mwa Afrika akizingatia haswa Ufalme wa Buganda nchini Uganda. vilevile , alihimiza watu kupambana na UKIMWI hayo wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 68 kwenye kasri yake huko Mingo, hivyo chini ya kaulimbiu: "Jitihada za kutokomeza VVU/UKIMWI ifikapo mwaka 2030."
Buganda wakati wa utawala wake imepata nafuu kutoka misukosuko iliyokuwa imeikumba ufalme huo, pamoja na kutukia maendeleo mapya ambapo Kabaka Mutep ameanzisha taasisi ambayo ni, baraza inahusisha kwa Ardhi katika Buganda, ili kusimamia ardhi na mali zinazorejeshwa kulingana na Sheria ya Urejeshaji Mali na miliki mnamo mwaka 1993. Kwa kweli, taasisi hiyo imechangia kusitisha mizozo juu ya ardhi hizo, na kutoa hati za miliki za ardhi kwa wahodhi wengi wa zamani.
Kwa ufupi, Ronald Edward anazingatiwa ni mhusika wa kipekee nchini Uganda ambaye ana mchango mkubwa katika kuwaunganisha Waganda na kuendeleza nchi hiyo.