Saba-Saba.. Lugha yangu ni Kiswahili 

Saba-Saba.. Lugha yangu ni Kiswahili 

Imeandikwa na /  Nourhan Khaled Eid

Hatuwezi kugusia suala hilo kabla ya kutia mwangaza Kiswahili, na sababu ya kuiita kama hivyo, basi tunajua kuwa Kiswahili kinajulikana kwa jina hilo kwa mujibu wa kueneza kwake kwenye pwani za Afrika Mashariki, na vilevile ni lugha ya Kibantu.

Hapo awali, Kiswahili kilikuwa kinaandikwa kwa herufi za Kiarabu, hadi baada ya kupita zama kadhaa, na kwa kuangushwa nchi hizo katika njama za ukoloni, kilikuwa kimebadilika kutoka herufi ya Kiarabu hadi herufi ya Kilatini, na kuna maandishi kadhaa ya mashairi yaliyopo hadi leo yaliyoandikwa kwa herufi za Kiarabu, na bila shaka ili kuthibitisha kuwa Waarabu wa Oman waliikalia Tanzania, jambo linalothibitisha kuwa Waswahili wameathiriwa na utamaduni wa Waarabu, na Waswahili wenyewe wakaathiriwa na lugha ya Kiarabu, kulikuwa na misemo mingi kuhusu kiwango cha kuathiriwa  Kiswahili na Kiarabu, lakini bila shaka Kiarabu ndiyo lugha yenye athari mkubwa zaidi katika Kiswahili.

 Tarehe 7 Julai ni siku muhimu kwa Kiswahili na wazungumzaji wake, kwani siku hiyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliamua kutengea Julai 7 kila mwaka kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani, ili kuendeleza matumizi yake ya Umoja na Amani na kuimarisha mawasiliano kutokana na wingi wa wazungumzaji wake.

 Kiswahili ni lugha rasmi ya Umoja wa Afrika, na ndiyo lugha inayozungumzwa na watu wengi zaidi Barani Afrika.

Na vilevile Kiswahili inafundishwa katika Vyuo Vikuu kadhaa vya Misri, kwa mfano, Chuo Kikuu cha Kairo, Chuo Kikuu cha Ain Shams na Chuo Kikuu cha Al-Azhar, Kiswahili kinafundishwa katika Vyuo hivyo vya Misri kwa masomo yake ya fasihi na tafsiri, pia tamthilia nyingi zinazopatikana katika Vyuo Vikuu hivyo kama vile riwaya, tamthilia na hata hadithi fupi, na miongoni mwa waandishi mashuhuri wa Kiswahili ni James Mbotela aliyeandika "Uhuru wa Watumwa", Shaaban Robert na Dkt. Kyalo Wadi Wamitila, ambaye ni Dokta wa Fasihi ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kenya, Fasihi ya Kiswahili imejulikana kwa aina nyingi za riwaya, kwa mfano riwaya ya kisaikolojia, kijamii na kiupendo na nyinginezo zilizohusu riwaya ya Upelelezi katika Fasihi ya Kiswahili kulingana na athari yake kwa Ukoloni wa Ulaya, na miongoni mwa waandishi wake maarufu ni Said Ahmed Mohmed, aliyeandika Siri ya Sifuri, pamoja na Ben Rashid Mtobwa aliyeandika Maliaka wa Shetani na aliyechukua mhusika Joram kuwa msimulizi wake katika riwaya zake zote, tena Fasihi ya Kiswahili  iligusia masuala ya kihistoria katika tamthilia zake kama vile tamthilia ya "Kinjeketile" inayoandikwa na Ebrahim Hussien ambapo Kinjeketile alikuwa shujaa wa taifa katika vita vya Majimaji.