Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani

Imeandikwa na / Ali Mahmoud
Mnamo kila mwaka, Kiswahili huadhimishwa tarehe Julai 7, na inazingatiwa miongoni mwa lugha zinazozungumzwa zaidi na watu wengi Barani Afrika baada ya lugha ya Kiarabu, ambapo idadi ya wazungumzaji wa Kiswahili ni zaidi ya watu milioni 200 na inawekwa kati ya lugha 10 maarufu zaidi Duniani.
Umoja wa Mataifa uliadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani kwa kauli mbiu ya Kiswahili kwa ajili ya Umoja, Amani na Kukuza Utofauti wa kiutamaduni,basi Kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazotumiwa zaidi Barani Afrika na inajikita zaidi katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika ya Kati, pia lugha hiyo ina lahaja kadhaa.
Kiswahili kinafundishwa katika Vyuo Vikuu vingi Duniani, kama vile Vyuo Vikuu vya Misri, Ulaya na Marekani, Kiswahili pia hutumika katika vituo vingi vya Redio Duniani, kama vile BBC, VOA, DW, China Radio, na matangazo yanayoelekezwa kwa nchi za Afrika mashariki “Mowagahat” kwenye Jengo la Radio na Televisheni (Maspero) huko Misri.
Kiswahili ni mojawapo ya lugha rasmi kwenye Umoja wa Afrika na pia kwenye Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nchi zake zikiongozwa na Kenya na Uganda.