Ushindi wa Kweli
Imeandikwa na: Shahd Ahmed
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili/ Mervat Sakr
Tarehe Julai 23 ni kumbukumbu ambayo bado inaishi katika akili zetu, ikiwakilisha ushindi wa kweli na kukomesha kutoroka na kusitasita. Tukio hili lilihusisha kukabiliana na utawala wa kifasidi na mtawala dhalimu aliyekuwa akijificha katika utawala wake bila kujali maslahi ya wananchi wake na kutekeleza mahitaji yao. Mfalme Farouk wa Kwanza alikuwa picha ya wazi ya utawala wa nchi, lakini wakati huo huo, ushawishi wa Uingereza uliongezeka katika masuala ya nchi, na mfalme alishindwa kukabiliana na uingiliaji wa kigeni, jambo lililoonesha hali mbaya ya kisiasa na kijamii nchini, na udhaifu wa utawala wa Mfalme Farouk na kushindwa kwake kukabiliana na ushawishi wa kigeni.
Mnamo mwaka 1949, kikundi cha maafisa vijana walianzisha Kikundi cha Maafisa Huru iliyoongozwa na Muhammad Naguib; kwa sababu ya hali mbaya ya kisiasa na kijamii nchini Misri kama vile ufasidi wa serikali ya Mfalme Farouk, na udhalimu wa kisiasa ambapo uchaguzi haukuwa huru, na kuingilia kwa kasri la kifalme katika maisha ya kisiasa, na ufasidi wa vyama vya kisiasa vilivyokuwa vikishindana juu ya utawala. Pia, miongoni mwa sababu za mapinduzi ni kuongezeka kwa ushawishi wa Uingereza nchini na kuingilia katika masuala ya utawala; jambo lililosababisha madhara mengi kwa jamii ya Misri kutokana na dhuluma na ukandamizaji wa ushawishi wa Uingereza kwa wananchi.
Pia, miongoni mwa sababu za kuzuka kwa mapinduzi ya Julai 23 ni hali mbaya za kiuchumi za wananchi wa Misri; ambapo umaskini na ukosefu wa ajira vilienea kati ya wananchi na kuongezeka kwa hali mbaya ya kijamii. Kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya matabaka ya jamii, jambo lililozidisha hasira ya wananchi na jeshi, na kupoteza haki za wafanyakazi kutokana na ukosefu wa sheria za kuwalinda dhidi ya udhalimu wa waajiri. Sababu kuu ya kuzuka kwa mapinduzi ilikuwa hasira ya maafisa wazalendo ambao walipotumwa na Mfalme Farouk katika vita vya Palestina mnamo mwaka 1948 bila maandalizi, silaha, risasi au vifaa vya kutosha; jambo lililosababisha kushindwa kwao. Hivyo, kundi la maafisa waliamua kuanzisha Kikundi cha Maafisa Huru mnamo mwaka 1948.
Malengo ya Maafisa Huru ni kutokomeza ukoloni na washirika wake, kuondoa unyonyaji na udhibiti wa mtaji katika utawala, kuondoa ukabaila unaoonea wakulima na kuwafanya wateseke kutokana na umaskini. Pia, Kikundi cha Maafisa Huru kililenga kuanzisha haki ya kijamii katika jamii ya Misri, na kuanzisha jeshi la kitaifa lenye nguvu kukabiliana na adui. Maafisa Huru walilenga pia kuondoa mfumo wa kifalme unaoongozwa na Mfalme Farouk na kuanzisha Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.
Mnamo tarehe Julai 23, 1952, Maafisa Huru waliongoza mapinduzi ya kijeshi chini ya uongozi wa Gamal Abdel Nasser na Mohamed Naguib. Mapinduzi haya yalisababisha kuondoka kwa Mfalme Farouk wa Kwanza na kuondolewa kwa utawala wa kifalme, na kutangaza jamhuri. Mohamed Naguib aliteuliwa kuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na kusaini mkataba wa kuondoka kwa vikosi vya Uingereza kutoka Misri ndani ya miezi ishirini... Vikosi hivyo viliondoka mnamo tarehe Julai 1956.
Rais Gamal Abdel Nasser alitangaza kutaifisha Kampuni ya Kimataifa ya Mfereji wa Suez na kuhamisha mali, haki, na majukumu yake yote kwa nchi. Pia alifanya mageuzi ya kijamii na kiuchumi kupitia utoaji wa sheria za mageuzi ya kilimo, kugawa ardhi kwa wakulima, na kurekebisha mfumo wa elimu. Alijali haki za wanawake na kuwapa haki ya kugombea katika uchaguzi.
Baada ya Mapinduzi ya Julai 23, 1952, Misri ilisaidia mataifa ya Kiarabu dhidi ya ukoloni, ikiwemo Sudan, nchi za Maghreb, Umoja wa Falme za Kiarabu, na Yemen Kusini kupata utulivu. Iliunga mkono mapinduzi ya Kiarabu kama vile Mapinduzi ya Iraq na Mapinduzi ya Yemen, na bado inaunga mkono haki za wananchi wa Palestina kurejesha haki zao na kuanzisha taifa lao.
Misri pia iliunga mkono mataifa ya Afrika katika harakati za kupata uhuru kutoka ukoloni na kusaidia katika ujenzi wa kiuchumi. Ilisaidia harakati za ukombozi katika nchi za Afrika Mashariki kama Somalia, Kenya, Uganda, na Tanzania, pamoja na nchi za Afrika Magharibi na Kusini kama Nigeria, Ghana, na Congo kwa kuzipa silaha na fedha, pamoja na msaada wa kisiasa na kidiplomasia; hali iliyosababisha nchi 17 za Kiafrika kupata uhuru mnamo mwaka 1960.