Wanaume Karibu ya Rais Abdel Nasser(5)... Rubani Abdul Latif Al-Baghdadi, Makamu wa Rais wa Jamhuri

Wanaume Karibu ya Rais Abdel Nasser(5)... Rubani Abdul Latif Al-Baghdadi, Makamu wa Rais wa Jamhuri

Imetafsiriwa na/ Abdelrahman Mohamed
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed 

Abdul Latif Al-Baghdadi amezaliwa tarehe Septemba 20, 1917, katika kijiji cha Shawa, kinachohusiana na kituo cha Mansoura, baba yake alikuwa meya wa kijiji, alikariri Qur'an na kujifunza kitabu cha kijiji, na alipata baccalaureate (sekondari) kutoka Shule ya Sekondari ya Mansoura mnamo mwaka 1937, kisha alijiunga na Chuo cha Kijeshi mnamo mwaka 1938, na akashika nafasi ya pili katika darasa lake, kisha akajiunga na Chuo cha Anga na kuhitimu mnamo mwaka 1939, na akaorodheshwa wa kwanza katika darasa lake. Alifanya kazi kama afisa wa majaribio katika Jeshi la Anga kwa ujumla, na aliendelea kutoka cheo cha rubani wa pili hadi cheo cha kamanda wa mrengo "Kanali".

Al-Baghdadi alishiriki katika vita vya Palestina mnamo mwaka 1948, na alikuwa afisa wa kwanza wa majaribio wa Misri kuangusha mabomu katika mji wa Tel Aviv, alipewa tuzo ya kijeshi mara mbili wakati wa vita vya Palestina, na mwaka huo huo aliteuliwa kuwa kamanda wa kituo cha anga magharibi mwa Kairo.

Mnamo mwaka 1950, al-Baghdadi alijiunga na Shirika la Maafisa Huru, na baada ya mapinduzi ya Julai 23, 1952, aliteuliwa kuwa mwangalizi mkuu wa bodi ya wahariri, na kisha waziri wa vita chini ya Rais Muhammad Najib.

Mnamo tarehe Septemba 16, 1953, aliteuliwa kuwa rais wa mahakama ya kwanza ya mapinduzi, na kesi ya mkuu wa Mahakama ya Kifalme, Ibrahim Abdul Hadi, ilizingatiwa.

Mnamo tarehe Aprili 17, 1954, aliteuliwa kuwa Waziri wa Manispaa na Masuala ya Vijijini na Mwenyekiti wa Baraza la Huduma za Umma katika Wizara ya Rais Gamal Abdel Nasser. Baada ya uchokozi wa pande tatu, alichukua jukumu la kujenga upya Port Said, na mnamo 23 Juni 1956, Al-Baghdadi alipewa Nishani ya Nile.

Abdul Latif al-Baghdadi alichaguliwa kuwa spika wa kwanza wa bunge baada ya mapinduzi, na baada ya kuungana na Syria, Bunge la Taifa lilivunjwa na al-Baghdadi aliteuliwa kuwa makamu wa rais kwa masuala ya uzalishaji mnamo tarehe Agosti 1958.

Mnamo tarehe Novemba 8, 1960, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri ya Masuala ya Uchumi Mkuu, na mnamo tarehe Oktoba 17, 1961, kisha akateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uzalishaji na Waziri wa Hazina na Mipango, na alipewa faili ya kurekebisha na kuandaa vifaa vya serikali na utawala wa serikali.

Mnamo tarehe Oktoba 24, 1962, aliteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Umoja wa Kisoshalisti na alibaki katika Baraza la Urais, lililoundwa mnamo tarehe Novemba 1963.

Alijiuzulu mwezi Machi 1964 na kustaafu kutoka katika maisha ya kisiasa.

Alifariki dunia mnamo tarehe Januari 15, 1999, na kutuacha kumbukumbu zake kama shahidi wa historia ndefu ya maisha ya kijeshi na kisiasa, na aliomboleza katika mazishi ya kijeshi yaliyowasilishwa na Rais Mohamed Hosni Mubarak, Rais wa Jamhuri.

Vyanzo

Tovuti ya Urais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri

Tovuti ya Magazeti ya Al-Ahram

Tovuti ya Mamlaka ya Kitaifa kwa Vyombo vya Habari


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy