Aminah Al-Said .. mhariri mkuu  mwanamke wa kwanza katika vyombo vya habari vya Misri

Aminah Al-Said .. mhariri mkuu  mwanamke wa kwanza katika vyombo vya habari vya Misri

Aminah Al-Said .. mhariri mkuu  mwanamke wa kwanza katika vyombo vya habari vya Misri. Aminah Ahmed Al-Said alizaliwa tarehe ya ishirini, mwezi wa Mei, mwaka wa 1914, huko Kairo. Baba yake, Dk. Ahmed Said, alikuwa daktari maarufu aliamini kwa umuhimu wa elimu ya wasichana hadi kufikia kiwango cha elimu cha juu. Amina alisoma katika Shule ya Shubra, na akiwa na umri wa miaka kumi na tano, alikutana na Huda Shaarawy, aliyemchukua katika shule ya sekondari. Katika mwaka wa 1931, Amina alijiunga na darasa la kwanza la kike katika Kitivo cha Sanaa, na mkuu wa kitivo hicho wakati huo alikuwa Dkt. Taha Hussein.
 
Aminah alifanya kazi ya uandishi wa habari katika jarida la Al-Amal, Kawkab Al-Sharq, Akher Sa'a, na Al-Musawwar mnamo wa masomo yake ya chuo kikuu, na kuwa msichana wa kwanza kufanya kazi ya uandishi wa habari. Miongoni mwa wenzake katika chuo kikuu walikuwa Louis Awad, Rashad Rushdi, Muhammad Fathi na Mustafa Amin aliyemtambulisha kwa Muhammad Al-Tabe'i, hivyo akamkabidhi baadhi ya hadithi za kijamii alizozichapisha katika jarida la "Akher Sa’a" kama lilivyowasilishwa na Muhammad Fathi kwenye redio ili kufanya kazi kwa kipande, hivyo alitafsiri baadhi ya hadithi za Kiingereza na kuzikariri kwa sauti yake kwenye maikrofoni, na kuigiza katika tamthilia ya chuo kikuu ya "Mwanamke wa chuma" ya Tawfiq Al-Hakim. Amina alihitimu mwaka wa 1935.

Baada ya kuhitimu kwake, alifanya kazi katika gazeti la Dar Al-Hilal, kisha akafanya kazi kwenye redio, akarudi tena Dar Al-Hilal mwaka wa 1945 na akabaki huko hadi kifo chake. Aminah alipendezwa na shughuli za wanawake, na Huda Shaarawy alimsaidia kufanya safari mbalimbali nje ya nchi, muhimu zaidi yake ikiwa ni safari yake ya India, iliyotoa kitabu chake "Mitazamo yangu nchini India". 

Mnamo wa kazi yake na Al-Musawwar, alianza na sehemu ya “Niulizeni”, ambayo alijulikana kwayo, na alikuwa akijibu maswali ya wasomaji, na idadi ya barua iliongezeka maradufu katika kipindi alichochukua sehemu hiyo, ambapo jukumu lake lilikuwa mfululizo miongoni mwa waandishi, na aliwataka wasomaji kuwasilisha matatizo yao kwake. Katika mwaka wa 1954, enzi ya hayati Rais Gamal Abdel Nasser ilishuhudia kuibuka kwa nyota ya mwanamke wa kwanza wa Kimisri kuchukua nafasi ya mhariri mkuu. Ndivyo alivyokuwa mwandishi wa habari Aminah Al-Said , ambapo Amin Zaidan alitoa gazeti la "Hawaa" na kulikabidhi kwa mhariri mkuu. Kisha akachukua uhariri wa jarida la Al Musawwar, na katika mwaka wa 1976, Amina alichukua uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Dar Al Hilal.

Alikuwa mwandishi wa habari wa kwanza alizuru Marekani na Umoja wa Kisovieti, mwanamke wa kwanza wa Misri alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Kikundi cha Waandishi wa Habari, na mwanamke wa kwanza alishika cheo cha Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Waandishi wa Habari mwaka wa 1959. Alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Wanahabari, na baada ya kustaafu, akawa mshauri wa Dar Al-Hilal, mjumbe wa mabaraza maalum ya kitaifa, katibu mkuu wa Umoja wa Wanawake, na mjumbe wa Baraza la Shura kwa mihula miwili.

Aminah amechapisha vitabu kadhaa, vilivyo muhimu zaidi ni "Nyuso Katika Giza, Kutoka kwa Msukumo wa Upweke, Lengo Kuu, Mwisho wa Njia" na vingine. Alitafsiri vitabu vingi vya kimataifa, vikiwemo: "Wanawake Wadogo", "Miradi ya Mustakabali", na " Maisha ya Mshairi Mwingereza Lord Byron". Na alidai kufutwa kwa mahakama za Sharia na kurekebisha Sheria ya Hali ya Kibinafsi.

Na alipokea medali kadhaa kwa heshima ya juhudi zake, ambapo Rais Gamal Abdel Nasser akamtunuku nishani ya sifa ya daraja la kwanza mnamo wa mwaka wa 1963, na akamtuma kwa misheni na Dkt. Abdel Qader Hatem kwenda Marekani ili kuelezea msimamo wa Misri katika misimamo kadhaa ya kisiasa, na mnamo wa mwaka wa 1970, Rais Sadat alimtunuku Nishani ya Jamhuri, na katika mwaka wa 1979, alishinda Tuzo ya Kimataifa ya Sayari ya Dhahabu, na mnamo wa mwaka wa 1992, Rais Hosni Mubarak alimtunuku Nishani ya Utamaduni na Fasihi.

Aminah Al-Said alifariki tarehe ya kumi na tatu, mwezi wa Agosti, mwaka wa 1995.