Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta

Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta
Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta
Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta
Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta
Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta
Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta
Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta
Kampuni ya Kitani na Mafuta ya Tanta

Kampuni ya Tanta ya Kitani na Mafuta E.S.C ilianzishwa kwa mujibu wa idhini iliyotolewa tarehe 4, mwezi wa Novemba mnamo 1954, pia ilichapishwa katika toleo Na. 92 la Gazeti la Misri la Al-Waqaea, yenye bajeti ya paundi elfu 85. 

Kampuni hiyo ilianzishwa baada ya kuunganishwa kwa viwanda vitatu vya Kitani, ambavyo ni: 

Kiwanda cha Kitani cha Farkouh (F.F.F) inayomilikiwa na mmiliki wake Emile Farkouh kwa  utengenezaji wa nyuzi za kitani na mazao yake katika kijiji cha Mit Hobeish Al Bahariya katika Mkoa wa Gharbia, kwa umbali wa kilomita 93 takribani kaskazini mwa Kairo, na kiwanda cha kutengeneza kamba za Kitani (Al-Gamalin) kinachomilikiwa na Edward Nasser na  washiriki wake, na kilikuwa karibu na barabara ya kilimo ya Kairo-Alexandria, na kiwanda cha Robert Khoury na washiriki wake kwa uzalishaji wa kitani na mazao yake, na mafuta ya kitani yaliyochemshwa kwa (Abu Al-Rish). Na kilichukua eneo la ekari 35 kwenye mahali pa sasa pa kampuni huko Mit Hobeish Marine.

Kampuni hiyo ilifanya kazi katika kulima, kutengeneza na kuagiza Kitani na mazao yake, hadi ilipotaifishwa baada ya Mapinduzi ya Julai, mwaka wa 1952, na ikawa kumilikiwa kabisa na serikali, na rasiliamali yake iliongezeka hadi paundi  elfu 400 mnamo 1960.

Na mnamo 1962, kiwanda cha mbao wa chembe kilifunguliwa, na kilikuwa cha kwanza cha aina yake nchini Misri na Mashariki ya Kati, chenye uwezo wa kuzalisha tani 30 kwa siku kutoka bodi za mbao wa chembe. Pia, kiwanda kilifunguliwa kwa ajili ya kutengeneza mbao wa chembe uliobandikwa kwa melamine mnamo 1981, na mwanzoni mwa miaka ya tisini, viwanda vilifunguliwa kwa ajili ya utengenezaji wa mbao laini wa chembe, resini (gundi) na countertops, baada ya upanuzi huu, kampuni ilichukua eneo la ekari 73 takribani.

 Idara za kampuni:

 Kiwanda cha Kitani.

 Kiwanda cha Kamba 

 Kiwanda cha Mafuta.

 Viwanda vya Mbao wa Chembe.

 Kiwanda cha Mazao ya Mbao.

 Kiwanda cha Resini- Gundi.

 Kiwanda cha Countertops.

 Kiwanda cha Mbao ya Foil.

Miongoni mwa mazao makuu ya kampuni ni:

Mbao wa Chembe uliobandikwa kwa Foil.

Mbao wa Countertops.

Samani.

Mafuta ya Kitani ya kuchemsha kwa rangi.

Kamba ya Kitani.