Kampuni ya Maziwa ya Kimisri…. Kampuni Kubwa Zaidi ya Kipekee ya Utengenezaji wa Maziwa na Mazao yake Ndani ya Mashariki ya Kati na Afrika kwa Ujumla
Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled
Chini ya andiko la “ kikombe safi cha maziwa kwa watoto wote wa Misri” na kwa ajili ya kuiwezesha Misri iwe mdhibiti wa utengenezaji wa kiafrika na kiarabu, Rais mwendazake Gamal Abdel Nasser alianzisha kiwanda muhimu zaidi mojawapo ya viwanda vikuu alivyoanzisha ambapo ni “ Kampuni ya kimisri ya maziwa na vyakula” mwaka 1956 , kwa lengo la kutengeneza , kuchuja na kukusanya maziwa pamoja na kuyauza na kutengeneza bidhaa zake tofauti kama jibini kwa aina zake , mgando wa maziwa hata baralai .
mnamo mwaka 1973 , mtaji wa kampuni hiyo ulifikia pauni milioni 5 ya kimisri na ilipata matawi mengi ambapo ilikuwa na viwanda 9 ndani ya miji ifuatayo: kairo , Alexandria, Damietta، Mansoura, Tanta , Ismailia، kom Ombi na Sakha , pamoja na kituo cha taifa cha mafunzo huko Alexandria, ambapo ni kituo pekee katika mashariki ya kati kinachohusika kuendeleza tafiti husika za bidhaa za maziwa, na zaidi ya vituo 60 vya kuyakusanya maziwa kutoka maeneo yote ya kimisri wakiwemo wakazi wa nyanda za juu na watengenezaji wa maziwa ili kuyasafirisha kuelekea viwanda vya kampuni, kupitia mlolongo mrefu wa magari mahususi yaliyoagizwa kutoka nje , na baadhi yake yanafanya mambo ya kuchuja na kuyasafisha wakati wa usafirishaji, na viwanda vilisambazwa kwa mujibu wa maeneo na idadi za raia kama ifuatayo:

1/ kiwanda cha kairo: kinashughulikia nafasi ya kilomita laki nne na elfu mbili , kitongojini mwa Amreya ، na ndani yake kinajumuisha viwanda vitano vya kutengeneza vinaainishwa kama ifuatayo:
_ kiwanda cha jibini iliyopikwa
_ safu ya kuchuja na kuyajaza maziwa
_ kiwanda cha jibini nyeupe
_ kiwanda cha mgando wa maziwa
_ kiwanda cha kutengeneza samli
_ kiwanda cha baralai .
2/ kiwanda cha Alexandria (Seclam): na hicho ni kiwanda kikale zaidi miongoni mwa viwanda vya kimisri vya kutengeneza maziwa, na kinashughulikia nafasi ya laki 3 na elfu mbili kilomita, na kinajumuisha safu za kuchuja , kuyajaza maziwa na maji ya matunda na kutengeneza jibini na pia pale kuna mapumziko kale ya kifahari.

3/Kiwanda cha Damietta: kinachoshughulikia nafasi ya ekari 12 yaani kilomita elfu 50 kwenye mtaa wa Al Shuaraa ، na kinajumuisha safu za kutengeneza maziwa, jibini , mtindi, jibini na samli .
4/ kiwanda cha Mansoura: kinachoshughulikia nafasi ya kilomita elfu 35 na kina safu za kutengeneza jibini, maziwa na mtindi na hicho ni tofauti na safu pekee ya utengenezaji wa jibini ya Roquefort ambapo kilikuwa kiwanda cha pekee nchini Misri kinachotengeneza aina hiyo ya jibini na baada ya kufungika kwa kiwanda hicho hakuna mtu amewahi kutengeneza aina hiyo.
5/ kiwanda cha Tanta: na kina safu kamili za utengenezaji wa bidhaa za maziwa.

6/ Kiwanda cha Kafr El Sheikh: na kinashughulikia nafasi ya kilomita elfu 30 katika eneo la Shaba , na kina safu kamili zinazotengeneza bidhaa zote za maziwa.
7/ kiwanda cha kom Ombo kusini mwa Misri: ni mojawapo ya viwanda vikubwa zaidi kilichohisiwa na utengenezaji katika eneo la nyanda za juu na kilikuwa na mlolongo mrefu wa magari na kwa mujibu wa ripoti ya kamati rasmi kutoka wizara ya viwanda mnamo mwaka 1973 hisa zake zilihesabiwa kwa milioni 2 na laki 8 na elfu 40
8/ kiwanda cha Ismailia: kilikuwa kikubwa na kilitoa bidhaa za maziwa kwa eneo lote la kairo.

9/Kituo cha kitaifa cha Alexandria: kilianzishwa mwaka 1936 , kwa kushirikiana na shirika la vyakula na kilimo la Umoja wa mataifa (Alfao ) ambapo kililenga kuendeleza tafiti zinazohusiana na kutengeneza bidhaa za maziwa na kutoa aina tofauti mpya kwa viwanda vya kambuni, pamoja na uchangiaji wake katika utengenezaji na kuzisafirisha bidhaa zake zenye hali ya juu .
Mbali na viwanda hivyo vikubwa, mali ya Kampuni ya Maziwa ya Misri ilijumuisha kundi kubwa la magari na vituo vya maonesho na usambazaji katika maeneo mbalimbali ya miji, vituo na hata vijiji na , kulingana na makadirio ya kamati ya Wizara ya Viwanda mnamo 1973, iligharimu takriban pauni milioni moja na laki 6 na elfu hamsini za Misri wakati huo .
Matokeo ya majengo haya makubwa ya kitaifa yalikuwa uzalishaji wa kampuni ya maziwa maarufu ambao watu wote wa Misri walijua kutoka mwisho wa miaka ya sitini hadi mwisho wa miaka ya themanini, pamoja na bidhaa maarufu za jibini za kampuni, na kukidhi mahitaji yote ya Misri na taasisi zake za kijeshi, afya, na hata ya elimu kutoka maziwa na bidhaa zake, na iliweza kufungua njia ya kuuza nje kwa nchi za nje.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy