Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu

Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu
Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu
Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu
Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu
Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu
Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu
Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu
Chuo cha Nasser cha kijeshi cha Juu

Tangu zamani, mtu wa Misri ni mali yake inayoendelea. Mwamko ni moja wapo wa ujuzi, na Mmisri aliishi katika matukio mengi, migogoro, na ustaarabu, tamaduni tofauti. Hayo yote yameumba hisia ya ajabu inayoitwa mwamko wa pamoja. Kuanzia hapa likaja wazo na umuhimu wa kuunda mwamko wa kitaifa; kwa sababu ardhi ambayo haina uwezo wa kuilinda inatamaniwa, na Ufahamu wa vitisho, changamoto na hatari zote ni nguvu, nguvu kubwa inayofanya kazi ya uwiano, na kuunganisha dhana; ili kukabiliana na hatari yoyote, na kwa kuwa kujenga mwamko ulikuwa lengo la makabiliano na uwiano wa kitaifa, amri ya utekelezaji namba 4/11/18 /1808 ilitolewa kwa tarehe 4/12/1964 kuhusu uanzishaji wa Chuo cha Nasser cha kijeshi cha juu, kinachohusika masomo ya juu.

Chuo cha  Nasser cha kijeshi cha juu kilifunguliwa mnamo Machi 6, 1965 kwa mahudhurio ya kiongozi hayati / Gamal Abd El Nasser, na kitivo cha wataalam wa Urusi kiliundwa kwa ajili yake, na utafiti huo ulikuwa wa Chuo cha Vita vya Juu. Na mwanzo wa kikao cha pili cha Chuo cha Vita vya Juu mnamo Septemba 1966, kikao cha kwanza kilifanyika katika Chuo cha Kitaifa cha Ulinzi.

Masomo yalisitisha katika Chuo hicho kuanzia Juni 1967 hadi Desemba 1973, na kozi zake za kimsingi ziliahirishwa; kwa sababu ya hali ya vita.Katika kipindi hiki, kozi fupi zilifanyika kwa maafisa wakuu wa jeshi. Baada ya ushindi wa Oktoba 1973, masomo yaliendelea katika Chuo, Marejeleo ya Urusi yalitafsiriwa kwa Kiarabu, na mitaala ilifundishwa na walimu wa Misri.

Mnamo 1975, ulikuwa mwanzo wa mapokezi ya  wanafunzi kutoka nchi ndugu za Kiarabu na nchi mbalimbali za kirafiki za ulimwengu.

Majukumu ya Chuo:

Kukarabatisha na kuendeleza uwezo na ujuzi wa maafisa wakuu wa vikosi vya kijeshi kushika nafasi za juu kwa kufanya kozi za mbinu za kimkakati katika Chuo cha Vita cha Juu.

Kukarabatisha na kuendeleza uwezo na ujuzi wa wale walioteuliwa na waajiri wao kutoka kwa wanajeshi na wafanyakazi wakuu wa serikali katika nchi kwa kufanya kozi za masomo katika Chuo cha Ulinzi cha taifa.

Kuchangia katika kila kitu kinachohusiana na masomo ya juu ya kijeshi na utafiti wa kisayansi katika uwanja wa kijeshi na nyanja nyingine zinazohusiana na kuhimiza upinzani wa kimkakati wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa kufanya na kuhudhuria semina za kisayansi za kijeshi za kimkakati za ndani na nje.

Kuimarisha viunganishi vya kiutamaduni na kisayansi kati ya Chuo na Vyuo vingine katika ngazi ya Kiarabu na kimataifa.

Vyuo Vikuu na Vituo vya Chuo cha Nasser  cha kijeshi cha juu:

Kitivo cha Vita cha Juu:

Baada ya kutoa azimio la Jamhuri kuhusu kuanzisha kwa Chuo cha Nasser cha juu cha kijeshi , kikao cha kwanza cha chuo hicho kilifanyika Machi 6, 1965. Chuo kilianza kupokea wanafunzi kutoka nchi ndugu na rafiki kuanzia kikao Namba (3) vita vya juu.

Chuo kinawawezesha maafisa wakuu kuchukua majukumu ya uongozi, wanajeshi, na kazi za kiuongozi katika jeshi ya barabara, maeneo ya kijeshi, na vifaa vya uongozi mkuu wa jeshi nchini Misri na nchi ndugu na rafiki. Na pia utafiti wa kisayansi katika uwanja wa kuhakikisha mkakati wa kijeshi.

Kozi zinazofanywa kutoka kwa Kitivo hicho:

kozi ya juu ya Vita.

Kozi ya juu kwa viongozi wakuu.

Kozi ya viongozi wa maandalizi.

kozi ya kimkakati ya Kiafrika.

Kozi ya maandalizi  mapema kwa viongozi.

Kozi ya Vikosi vya Kulinda Amani.

Kozi ya walimu wa historia ya kijeshi.

kozi ya Kusuluhisha migogoro na kulinda Amani.

Shahada ya Kitivo hicho .

Shahada ya Ushirika wa Kitivo cha juu cha Vita.

Kitivo cha Ulinzi wa Taifa :

Kitivo hicho  kinachukuliwa kuwa kituo cha juu zaidi cha kisayansi cha masomo na utafiti katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kuhusu maswala ya mkakati wa kitaifa na usalama wa kitaifa na pande zake za kisiasa, kiuchumi, kijeshi, kijamii na kinafsi.

Kitivo hicho kinakarabatisha na kuendeleza uwezo na ujuzi wa maafisa wakuu kushika nafasi za juu katika jeshi, kukarabatisha wafanyakazi wakuu wa serikali kushika nafasi za juu serikalini na kushiriki katika kuweka maoni ya mkakati kwa jumla na sera kuu za nchi. na kufahamu mambo yote yanayowaathiri, pamoja na kukarabatisha wahamiaji wanaokuja kutoka nchi ndugu na rafiki kushika kazi za uongozi za juu zaidi katika nchi zao. Kuhakikisha maelewano wa pamoja kati ya kikundi kilichochaguliwa cha wafanyikazi wakuu katika sekta tofauti za serikali (raia - wanajeshi) pamoja na wahamiaji ambao wanavumilia, kwa mujibu wa kazi zao za mustakabali  jukumu la kuunda uamuzi.

Kozi zinazofanywa kutoka kwa Kitivo hicho: 

Kozi ya Ulinzi wa Taifa.

Kozi ya Juu ya Usimamizi wa Mgogoro na mazungumzo

kozi ya kudhibiti Silaha.

Kozi ya wahariri wa vyombo vya habari wa kijeshi.

Kozi ya sheria za kimataifa na za kibinadamu kwa vikosi vya anga na bahari.

Kozi ya kuchangamsha kwa washikaji ulinzi na wake wao.

Kozi ya maandalizi mapema kwa kushirikiana na kitivo cha Vita vya Juu.

Shahada ya Kitivo hicho

Ushirika wa kitivo cha Ulinzi wa Taifa.

Uzamivu wa Falsafa katika Mkakati wa Kitaifa.

Kituo cha Masomo ya Kimkakati kwa Wanajeshi:

Kituo cha Masomo ya Kimkakati kwa Wanajeshi kilianzishwa kwa uamuzi wa Namba (321) ya mwaka wa 1994 uliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri. Kituo hiki kina uhusiano na Chuo cha Nasser cha kijeshi cha juu.

Majukumu ya kituo: 

Kuandaa masomo ya kina na za uchambuzi wa matatizo na mada zinazohusiana na usalama wa taifa wa Misri katika ngazi mbalimbali (kimataifa - kikanda - ndani ya nchi).

Kuendeleza na kukuza mawazo ya kimkakati kwa maafisa wa jeshi katika nyanja zote (kisiasa - kijeshi - kiuchumi - kijamii - kiutamaduni).

Kuendeleza mahusiano na vituo vya utafiti vingine (za ndani, kikanda na kimataifa).

Kuhudhuria semina na vikao vya majadiliano vinavyofanyika katika vituo vya masomo katika ngazi ya kienyeji na kikanda.

kuchangia katika kuweka maoni na mawazo ya kupanga mipango ya mbali na ya kimkakati ambayo majeshi hushiriki pamoja na mashirika mengine ya serikali.

Kutoa kituo cha maelezo na taarifa zinazochangia katika kufanikisha shughuli za kisayansi na kiutafiti za kituo hicho.

Maktaba ya Chuo:

Maktaba ya Chuo hicho ilianzishwa katika mwaka wa 1965, na katika1969 ilipewa jina la shahidi "Abdel Moneim Riyad", ambaye aliuawa mnamo Machi 9 mwaka huo huo. Inachukuliwa kuwa moja ya maktaba ya kisayansi maalum katika mkakati wa kitaifa na usalama wa kitaifa.

Maktaba hiyo ina vitabu elfu 55 vya marejeleo, majarida katika lugha za Kiarabu na za kigeni, utafiti za kijeshi wa Vita vya Juu na Vyuo vya Ulinzi vya Kitaifa, tafiti za Uzamivu, na vitabu vya kodi za kijeshi.

Sehemu za Maktaba: 

Sehemu ya Kwanza: Maonyesho ya Vitabu vya Kisasa

Ina vitabu vya hivi punde vilivyopokelewa na maktaba pamoja na kamusi, atlasi, Ensaiklopedia na vitabu vya mwaka.

Sehemu ya Pili: Ukumbi wa Chini

Ina ukumbi wa majarida na kongamano lenye majarida elfu tatu, na ukumbi ulioambatanishwa wa kuhifadhi tafiti zote zilizojadiliwa katika chuo hicho tangu kuanzishwa kwake.

Sehemu ya tatu: ya juu

Ina takriban vitabu elfu hamsini vya Kiarabu na kigeni katika sayansi zote za kijeshi, kimkakati na kiutamaduni.Maktaba hii imeainishwa kulingana na uainishaji wa  Dewie  Al_ Ashry wa dunia.Kuna kompyuta ambazo mfumo wa maktaba unatumika kurahisisha kukuta yaliyomo kwenye maktaba kupitia programu ya juu ya maktaba kwa njia nyingi, ikiwa ni pamoja na (jina la kitabu - maudhui wa kitabu - jina la mwandishi - Mchapishaji - Ainisho Na.)

Sehemu ya nne: ukumbi wa maktaba ya elektroniki

Ina kifaa cha mtandao cha kuwahudumia wanafunzi na watafiti katika kupata taarifa za hivi punde kwa muda mfupi zaidi. Pamoja na vifaa viwili ambavyo vina mfumo wa maktaba wa kukuta yaliyomo maktaba kutoka kwa vitabu, marejeleo na Tafiti.

Sehemu ya Tano: Maktaba ya Kodi

Ina vitabu vya kijeshi vilivyotolewa kwa  taasisi ya Utafiti wa Kijeshi, ambavyo vimeainishwa kuwa vya siri na haviruhusiwi kusambazwa na wanachama wasio wanajeshi wa Kikosi cha Wanajeshi wa Misri.

Chuo cha Nasser pia kinatoa kikundi  cha vyeti na kozi kwa raia, pamoja na:

 kozi ya Mafunzo ya Kimkakati na ya Usalama wa Kitaifa kinalenga kuongeza ufahamu wa dhana na vipande vya Usalama wa taifa.

Kozi ya Migogoro na Mazungumzo inalenga kuandaa msingi wa elimu katika uwanja wa kudhibiti migogoro ili waweze kushiriki vyema katika kudhibiti migogoro halisi katika siku zijazo.

Kozi ya wafanyi uamuzi inalenga kuandaa makada wa wafanyakazi katika sekta mbalimbali za nchi kufanya kazi katika kufanya maamuzi na kufanya maamuzi na kutambua njia mbadala sahihi zaidi za kuchukua maamuzi.

Kozi ya Urais wa Jamhuri; kuwawezesha vijana kuwa na sifa za uongozi.

Chuo cha Nasser cha kijeshi cha juu kinaendeleza utendaji wa kazi katika mchakato wa elimu; kulingana na fikra za hali ya juu katika sayansi mbalimbali, na sanaa vita na kiraia.