Ensaiklopedia ya Fiqhi ya Kiislamu ya Gamal Abdel Nasser ....ya Kwanza ya Aina yake katika Kiwango cha Wazo la Mkusanyiko wa Vitabu

Ensaiklopedia ya Fiqhi ya Kiislamu ya Gamal Abdel Nasser  ....ya Kwanza ya Aina yake katika Kiwango cha Wazo la Mkusanyiko wa Vitabu

Imefasiriwa na / Zeinab Mekky

Baraza kuu la Masuala ya Kiislamu lilitoa zawadi kubwa kwa tasisi na nchi mbalimbali na hivyo mnamo Ramadhani 9, mwaka wa 1388 Hijria, iliyokuwa sawa Novemba 29, 1968.

 Zawadi hiyo ilikuwa inajumulisha nakala 100 za Quran Tukufu, na nakala 100 za Ensaiklopedia ya Fiqhi ya Kiislamu ya Rais Gamal Abdel Nasser , Silinda 7000 za  kufundisha mila za kiislmau na jinsi ya kuzitekeleza, zilizotafsiriwa na lugha na lahaja zinazoenea katika Ulaya, Afrika, na Mashariki ya Mbali.

Zawadi hiyo ilipewa kwa Chuo kikuu cha Vienna,  Baghdad na Makumbusho ya Uingereza huko London, na Maktaba ya Congress huko Amerika, pia  Quran na Vitabu 30,000 Vilipewa kwa 
Pakistan, Yemen Kusini na Kaskazini, Ufalme wa Hashemite wa Jordan, Sierra Leone, Malaysia, Ufilipino, Somalia, Sudan na Uganda.

Baraza la Masuala ya Kiislamu lilitimiza hamu ya watu wa Sudan, likasajili Quran ya mwalimu kwa kusoma Al-Douri kutoka kwa Abi Amr, ikaitikia matakwa ya watu wa Libya, hivyo Quran ya Kaloni ilianza kusajiliwa, na Quran ya  Mwalimu ikisajiliwa kwa  kusoma Warsha na kusoma Hafs kwa watu wa Kiislamu, ili kuchangia kufundisha Quran kupitia nakala hizo.

Edwerd Lambert Mwanasheria Mfaransa alikuwa mmoja wa watu wa kwanza waliotamani kua uwepo wa Ensaiklopedia ya Fiqhi ya kiislamu wakati The Hague ilipokutana kwa ajili ya sheria linganishi mnamo mwaka 1932, ndoto hiyo hiyo ilirudiwa katika mapendekezo ya chama cha Wanasheria wa Kimataifa huko Tha Hague mwaka 1948, mwaliko ulirudiwa upya mara tena mnamo mwaka 1951, katika mkutano wa Fiqhi wa Mashariki uliofanyika Kitivoni mwa Sheria huko Paris, ambapo mapendekezo yake yalidai kuzindua kazi  ya ensaiklopedia iliyopangwa kwa  sheria kama ensaiklopedia ya Fiqhi, baadhi ya wenye Fiqhi wa Syria walikuwa wameshuhudia mkutano huo na walishiriki katika kazi zake, huku wakarejea nyumani yao, wakihakikisha kwamba ulimwengu wa kiislamu, kutokana na turathi zake za Fiqhi ni lazima kutekelezwa, na kuanzisha kamusi hiyo ambayo mkutano uliitaka ni jambo ambalo watalaamu wa kiarabu wanapaswa kulikuza , na wakaeneza wazo hili na kuliita mpaka wakakishawishi Kitivo cha Sharia katika Chuo Kikuu cha Damascus, hicho kinakubali mtazamo huo vizuri na inaona ni ya kupongezwa sana, mpaka ikaweza kukishawishi chuo kikuu na kushawishi serikali ya Syria kabla ya muungano. na Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na kutoa amri ya Jamhuri ya kuanzisha kamusi hii kwa mfumo maalum Asili yake inatokana na amri hii.

Kamati ya watu wa Fiqhi ilianzishwa katika kitivo cha sheria ili kuweka kamusi hiyo, kamati hiyo haikuharakisha katika kazi yake lakini iliitayarisha kwa utaratibu na sahihi kwa manufaa zaidi  kusaidia kufikia lengo.
Hatua zikienda polepole kisha kasi ya kazi iliongezeka ndani ya mwaka wa Umoja wa Kiarabu kati ya Syri na Misri, wakati uamuzi wa Wizara wa namba 24 wa mwaka 1961, uliotolewa mnamo Januari 18, mwaka wa 1961, ili kuunda kamati ya kufanya kazi ya ensaiklopedia ambayo inajumuisha kundi la wafiqhi  wanayopobea wa Syria na Misri kama Dkt. Marouf Al-Dawalibi na Dkt. Mustafa Al-Sibai Na Dkt. Ahmed Al-Samman, Prof. Mustafa Al-Zarqa, Dkt. Youssef Al-Ash, na Dkt. Zaki Abdel-Bar, mwaka huo huo uamuzi wa nambari 33 ulitolewa ili kuiita jina la Ensaiklopedia ya Fiqhi ya Kiislamu ya Gamali Abdel Nasser.

Ensaiklopedia inazingatiwa mradi mkubwa sana, unaojumuisha maamuzi ya Fiqhi na tafsiri na herufi za alfabeti katik shule nne maarufu za Fiqhi:- Hanafi, Shafi’is, Malikis, Hanbalis, na wengine kama vile Dhahiris, Zaidis, na Shia.... kamati ilikuwa na nia kwamba Ensaiklopedia iwe kamili ya aina za Fiqhi ya kiislamu kwa mujibu wa madhehebu tofauti za Waislamu ndani yake, ili watafiti wanaweza kupata katika kamusi hiyo baada ya kukamilika kwake marejeo ya kina kwa kila kitu kinachoweza kukusanywa kutoka kwa maoni, ya watu wa Fiqhi wa Kiislamu katika hukumu, bila kujali tofauti ya rai hizi na aina zake  .... nia ya kamati si kuonesha sheria katika Ensaiklopedia hiyo kama ilikuwa inaoneshwa katika vitabu vya kale, yenye utata, ambayo wamekuza sayansi za dini tu wanaoweza kuifahamu, bali imewasilishwa kwa ibara iliyo wazi inayoeleweka na wanachuoni wa kidini, mafaqihi wa sheria, na kila mwanaelimu anayetaka kujua moja ya rangi za utafiti wa Fiqhi wa Kiislamu.

Wakati awamu ya Hayati Rais Gamal Abdel Nasser mnamo miaka sitini ya karne iliyopita hadi leo, zaidi ya juzuu arobaini zimechapishwa pamoja na uangalifu wa Wizara ya Wakfu na kamati ya Fiqhi ya kiislamu kwenye Baraza Kuu la masuala ya kiislamu ya kimisri kwa uiongozi wa mjumbe wa Mamlaka ya Wanazuoni Waandamizi wa Al-Azhar Al-Shareif, marehemu Bwana Ahmed Ali Taha Rayan.

Mwishoni mwa miaka sitini ya karne iliyopita, Misri ilizoea kuitoa Ensaiklopedia ya Gamal Abdel Nasser kwa nchi za ulimwengu katika Fiqhi ya kiislamu katika sherehe maarufu ya kidini kama kuzaliwa kwa Mtume mtukuy na mwezi wa Ramadhani, na Ensaiklopedia hiyo ilikuwa ya kwanza ya aina yake , katika kiwangu cha wazo la vitabu vikuu maarufu.

Vyanzo

Kitabu cha maneno ya Dkt. Taha Hussein.

Tovuti ya Al- Mizan.