Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wako kwenye ziara ya Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji
Wajumbe Vijana walioshiriki katika Udhamini huo, walitembelea Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, walipokelewa na Dkt. Ragab Abdel Azim, naibu katibu wa Wizara msimamizi wa Ofisi ya Waziri, Dkt. Osama Al-Dhaher, Mwenyekiti wa idara kuu ya mambo ya Ofisi ya Waziri, Dkt. Iman Sayed Mwenyekiti wa sekta ya Mipango, na Dkt. Tahani Saleet Mwenyekiti wa Idara Kuu ya Ushirikiano wa Kimataifa katika sekta ya maji ya Nile, Dkt. Ayman Al-Sayed Mwenyekiti wa sekta ya Ufuatiliaji na taarifa, na mkutano uliongozwa na Profesa. Amira Sayed, mwanachama wa bunge la vijana la kimataifa la maji.
Kwa upande wao, wawakilishi wa Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji walikaribisha vijana wa Udhamini huo, wakiwatoa salamu za Dkt. Mohamed Abdel-Ati, Waziri wa Umwagiliaji na Rasilimali za Maji, na nia yake ya ziara hiyo inayoakisi haja ya kuimarisha ushirikiano wa mahusiano ya ukamilifu, ushirikiano wenye faida kwa jamii katika nyanja za umwagiliaji na maji, haswa vijana katika nchi mbalimbali Duniani.
Pia, Vijana wa Nasser walijua hali ya maji ya Misri, ukubwa wa changamoto zinazokabili sekta ya maji nchini Misri, haswa ongezeko la Idadi ya watu na mabadiliko ya tabianchi, uzoefu wa kitaifa wa Misri katika uwanja wa Umwagiliaji na Rasiliamali za maji, na jukumu la serikali ya Misri katika kuhakikisha mkakati wa kitaifa wa kurekebisha matumizi ya maji. Ziara hiyo ilihusisha kuonesha filamu ya kurekodi, inayoangazia umakini wa Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, katika awamu inayofuata, kukabiliana na changamoto za Usalama wa maji, na kuchangia katika kuhakikisha kiwango cha ubora katika mbinu za kusimamia rasilimali za maji kwa wingi na ubora, pamoja na kuendana na kasi ya maendeleo ya kiteknolojia na kuirekebisha ili kuhudumia kazi zote inazozifanya.
Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walipiga picha za ukumbusho mwishoni mwa ziara yao huko Wizara ya Umwagiliaji na Rasilimali za Maji, pamoja na mwingiliano, mapokezi makubwa na furaha ya wote kwa ziara hiyo.