Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba

Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba
Udhamini wa Nasser watembelea makumbusho ya vikosi vya anga katika matukio ya siku saba

Jumatatu Asubuhi, wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walitembelea makumbusho ya vikosi vya anga, mwanzoni mwa matukio ya siku ya saba ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la pili ulioandaliwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na  Dkt. " Ashraf Sobhy" kwa kushirikiana na Chuo cha kitaifa cha mafunzo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na taasisi nyingi za kitaifa, ukiwa na Ufadhili wa Rais wa Jamhuri, na utaendelea hadi kati kati mwa Juni ijayo chini ya kauli mbiu " Ushirikiano wa Kusini_ Kusini" kwa ushiriki wa viongozi wengi wa vijana wa kipekee kutoka Bara la Asia, Afrika, na Amerika ya Kusini.

Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wakati wa ziara yao kwa makumbusho ya majeshi  ya kimataifa walijua maelezo ya vipengele vya makumbusho, na walifanya ziara ndani ya makumbusho na walijua historia ya kuibuka usafiri wa Anga Duniani iliyoanzishwa na wamisri wa kale, ambapo picha ambazo zinafanana ndege zilipatikana katika makaburi ya wamisri wa kale kisha jaribio la "Abbas Ibn Firnas" hadi kufikia umbo la sasa la usafiri wa Anga Duniani, na pia walijua asili na historia ya jeshi la vikosi vya Anga vya Misri na kuzungumzia vita ambavyo vikosi vya anga kuanzia vita vya 48 hadi Oktoba 1973 na mahanga ya vikosi vya anga tangu uanzilishi wake na jukumu na medali waliopokea, na picha adimu zinazoonesha ushiriki wa vikosi vya Anga katika vita mbalimbali.

Ziara ya washiriki wa Udhamini huo ilijumuisha pia kukagua chumba cha kufundisha ndege, kutazama mfano wa chumba cha operesheni za vita vya Oktoba, kuingia ukumbi wa mashahidi wa vikosi vya anga, karakana ya kiufundi na kuingia katika ukumbi wa Al_Majd, ambapo ni ukumbi mkuu katika makumbusho, ambapo maonesho ya filamu kwa anwani ya

 " Ngao na Upanga"kuhusu vita vitukufu vya Oktoba 73 na inasimulia historia ya vikosi vya anga, viongozi, ushindi na vita ambavyo vikosi vya anga vilipigana na jukumu la kikosi cha wanajeshi katika vita vya Oktoba pamoja na kutambulisha vita vya "Almansora Algawiya" ambapo ni vita vikubwa na virefu zaidi ya anga katika historia ya kisasa baada ya vita vya pili vya Dunia, ambavyo Oktoba 14 ikawa sikukuu ya kila mwaka ya vikosi vya Anga vya Misri. 

 Mkurugenzi wa makumbusho ya vikosi vya anga Meja Jenerali Mwanahewa

 " Magdi Dowidar" alikutana na washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kupitia ziara yao kwa makumbusho, ambapo aliwakaribisha washiriki wote wa raia mbalimbali, akielezea kwamba kile kilichoonyeshwa katika ukumbi " Al_ Majd" ni mfano mdogo tu uliofanywa na vikosi vya anga haswa au jeshi kwa jumla. 

Alisisitiza kuwa maendeleo ambayo wanajeshi wa Misri wanayoshuhudia hivi sasa ni maendeleo ambayo hayajawahi kutokea; kwani kipengele cha kibinadamu na ushirikiano wa pamoja uliunganisha juhudi na fahari,

na " Dowidar" alieleza kwamba Misri inachukua haki yake kwa nguvu mbili: nguvu ngumu na nguvu laini, Na nguvu ya majeshi ni njia ya kumzuia mchokozi au mbakaji, Na fahari hiyo ya ushindi wa Oktoba ni fahari kwa waarabu kwa jumla sio kwa wamisri tu, akisisitiza kuwa vikosi vya jeshi na wamisri wana imani kamili katika uongozi wa kisiasa, ambapo unaongoza nchi kwa maendeleo na ustawi na kila mtu yuko na moyo wa mtu mmoja na lengo ni ulinzi na maendeleo.

Matukio ya ziara ya washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa yalimaliza kwenye makumbusho ya vikosi vya anga kwa kukagua eneo la maonesho yanayofungua ambayo lina ndege halisi za kivita na mifano ya ndege za vikosi vya anga vya Misri, historia ya matumizi yake, nchi asili na kujua aina zote za ndege za kivita na vita walivyovishiriki na walifanya ziara pia ndani ya mfano wa ndege yenye skrini zinazoonyesha filamu ya anga kuhusu timu ya michezo ya anga ya Misri. 

Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walielezea fahari na furaha zao kuhusu walichokitazama katika makumbusho ya vikosi vya ndege, pia walichokisikia kuhusu maandalizi, na walichokijua kuhusu historia ya vikosi vya anga vya Misri vinavyotakiwa fahari na walioshiriki katika ushindi wa Oktoba na walirejesha heshima ya Mmisri na Mwarabu, wakisifu stadi na uhodari wa Askari Mmisri na wanajeshi wa Misri.

Na kwa upande wake, Mratibu mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

" Hassan Ghazaly alielezea kuwa ziara ya makumbusho ya vikosi vya anga vya Misri inakuja; kwa ajili ya kuwajulisha washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwa historia ya vikosi vya anga vya Misri na michuano waliyoipiganwa kwake, katika kila vita walivyoshiriki hata vita vya sasa dhidi ya ugaidi, akiashiria kuwa wanajeshi wa Misri ni chanzo cha fahari kwetu sote na ngao inayowalinda wamisri kutokana na njama zinazopangwa dhidi yao. 

Na " Ghazaly" aliongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unakuja kama njia moja ya kuhakikisha lengo la nane la Mtazamo wa Misri wa 2030, na ni kuhakikisha na kuimarisha cheo cha uongozi wa Misri, ambapo Ajenda ya kitaifa iliangalia kuunganisha malengo yake ya kimaendeleo kwa malengo ya Kimataifa kwa upande na kwa Ajenda ya kikanda, haswa Ajenda ya Afrika 2063 katika upande mwingine. Baada ya mafanikio ya Misri katika kurejesha utulivu wake na kuboresha mahusiano yake na miduara yake ya nje,  lengo la kuimarisha cheo cha Misri na uongozi wake wa kikanda na kimataifa ni dharura; ili kusonga mbele kwa maendeleo kwa jumla, jambo linalohakikishwa kwa njia mbalimbali ambapo umuhimu wake zaidi ni kuunga mkono kuimarisha Ushirikiano wa kikanda na kimataifa, kwa hivyo kauli mbiu ya " Ushirikiano wa Kusini_ Kusini" ya Udhamini ilikuja kama moja ya Njia hizo.