"Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" watembelea Chuo cha Polisi 

"Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" watembelea Chuo cha Polisi 
"Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" watembelea Chuo cha Polisi 
"Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" watembelea Chuo cha Polisi 
"Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" watembelea Chuo cha Polisi 

Shughuli za siku ya tano ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" katika toleo lake la pili, unaoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy, kwa kushirikiana na Chuo cha Kitaifa cha mafunzo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na Taasisi kadhaa za kitaifa, kwa Ufadhili wa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri, Rais Abd El Fatah El-Sisi, unaofanywa hadi katikati ya Juni ijayo, kwa kauli mbiu ya "Ushirikiano wa Kusini-Kusini", kwa ushiriki wa baadhi ya Viongozi mashuhuri wa Vijana kutoka mabara ya Asia, Afrika na Amerika Kusini.

Matukio ya siku ya tano ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" katika toleo lake la pili yamejumuisha kuandaa ziara ya washiriki wa Udhamini huo katika Chuo cha Polisi katika mji wa Al-Tagamoa Al-Khames, kwa ushiriki wa Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na kundi la Viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo, ambapo walipokelewa wakati wa kuwasili kwao na Meja Jenerali Dkt. Ahmed Ibrahim, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Chuo cha Polisi, aliyefuatana nao katika tembezi ndani ya Chuo kwa mfumo wa mkakati wa Wizara ya Mambo ya ndani unaolenga kuimarisha ushirikiano na kujenga madaraja ya mawasiliano pamoja na taasisi na vyombo vyote kutoka nchi mbalimbali za Dunia.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Chuo cha Polisi, Meja Jenerali Dkt. Ahmed Ibrahim aliwakaribisha wajumbe walioshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akitoa salamu za Meja Jenerali Mahmoud Tawfiq, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na kujali kwake kukubwa kwa ziara hiyo ambayo ni kielelezo cha ushirikiano uliopo kati ya Wizara mbili  za Mambo ya Ndani na Vijana na Michezo katika uwanja wa kutoa mafunzo kwa Vijana wa kada kutoka nchi mbalimbali Duniani, unaochangia pia katika kuimarisha mifumo ya ushirikiano kati ya Misri na nchi za mabara matatu zinazoshiriki katika matukio ya Udhamini huo.

Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, mnamo ziara yao ya Chuo cha Polisi, walikagua vifaa na taasisi za chuo hicho na uwezo unaozijivunia kuzifanya kuwa mwanzoni mwa orodha ya taasisi zinazohusika na mafunzo maalum ya Usalama katika ngazi ya kikanda na kimataifa ambapo washiriki wa Udhamini huo walijifunza  juhudi zilizofanyika katika kuandaa na kukarabati wanafunzi wa Chuo cha Polisi kwa njia ya kisasa na ya kimaendeleo, na walitembelea Utawala Mkuu wa Mafunzo ya Ulinzi na Mbwa wa Walinzi, Vikosi vya Wapanda Farasi wa Kitivo cha Polisi, pamoja na kutembelea Kitivo cha Mafunzo ya Juu, na Kituo cha Utafiti cha Polisi kinachojishughulisha na kutoa mafunzo kwa kada za ulinzi kutoka nchi rafiki za Afrika na nchi za nje.

Pia washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa mnamo wa ziara yao kwenye Chuo cha Polisi, walitembelea taasisi kadhaa za mafunzo na kielimu, kama uwanja wa mafunzo ya kujilinda, kijiji cha mbinu, na nyanja za mafunzo ya kiufundi ya Usalama kwa utaalamu wa kazi na mfumo wa Uigaji , pamoja na kutazama maonesho ya wanafunzi katika sanaa ya upigaji risasi na ustadi wa kubomoa na kukusanya silaha, na mapitio ya mbinu maarufu za mafunzo ya Usalama unaotegemea matumizi ya data kutoka kwa teknolojia za kisasa ili kukuza uwezo na ujuzi wa usalama wa wanafunzi katika Chuo cha Polisi.

Kwa upande wao washiriki wa " Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" wameelezea furaha yao kubwa kwa ziara hiyo na Shukrani zao  za dhati kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri na Chuo cha Polisi kwa ziara hiyo iliyowawezesha kujua jukumu la chuo hicho katika kuandaa na ukarabati wa watu wa Usalama na jukumu lake katika kutoa mafunzo kwa kada za Usalama.

Matukio ya siku ya tano ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" yalihitimishwa na  kutembelea kwa washiriki wa Udhamini huo Sinema ya "Zawia" huko Downtown;kutazama maonyesho ya filamu ya Misri "Ardhi" ya Mtoajii Mkuu Youssef Shahine, kwa kuhudhuria kwa Mtoaji Mkuu Yousry Nasrallah, Mtengezaji Gabi Khoury, na Mwandishi wa Skripti Sayed Fouad, Mkuu wa Tamasha la Filamu la Afrika.

Washiriki wa "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" walizungumzia na Mtoaji Mkuu Yousry Nasrallah baada ya kuonyesha filamu ya "Ardhi", na kulikuwa na mijadala mingi kuhusu filamu, hadithi yake, na madhumuni yake, kwa kuzingatia kumsifu Mtoaji Mkuu Youssef Shahine kutoka kila mtu, na mwishoni walichukua picha za ukumbusho pamoja naye, wakiwa na  furaha kubwa kutoka kwa kila mtu na heshima kwa filamu ya Kimisri, iliyopata pongezi na kuthaminiwa na kila mtu.

Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Hassan Ghazaly, aliashiria kuwa ziara ya washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika Chuo cha Polisi inakuja ndani ya mfumo wa jukumu muhimu la Wizara ya Vijana na Michezo ili kufahamiana vijana pamoja na juhudi zilizofanywa ndani ya chuo hicho katika kuandaa na kukarabati watu wa Usalama kupitia kufuata mifumo na mbinu za hivi karibuni za kimataifa pamoja na kuhamisha uzoefu wa Misri ya kale katika kuimarisha na kuunda taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha viongozi vijana wa mabadiliko wenye maono yanayofuata na maelekezo ya urais wa Misri katika nchi mbalimbali kupitia ushirikiano, pamoja na kuwaunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi Duniani kwa mafunzo na ujuzi muhimu na maoni ya kimkakati.

Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa aliongeza kuwa toleo la pili la Udhamini huo limepanuliwa ili kujumuisha viongozi wa vijana kutoka Asia na Amerika ya Kusini pamoja na bara letu la Afrika, akielezea kuwa viongozi wa vijana 100 katika mabara matatu ya Afrika, Asia na Amerika Kusini wanashiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa miongoni mwa makundi yanayolengwa na watoaji wa maamuzi katika sekta ya umma, wahitimu wa Mpango wa Kujitolea wa Umoja wa Afrika, viongozi watendaji katika sekta binafsi, wanaharakati wa mashirika ya kiraia, wenyekiti wa mabaraza ya kitaifa ya vijana, wanachama wa mabaraza ya mitaa, viongozi wa vyama vya vijana, wanachama wa taasisi ya ualimu katika chuo kikuu, watafiti katika vituo vya utafiti wa kimkakati na mawazo, wanachama wa vyama vya kitaaluma, wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, wajasiriamali wa kijamii .... n.k.

Ikumbukwe kuwa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi lilitekelezwa mnamo Juni 2019 kwa uangalizi wa Waziri Mkuu wa Misri Dkt. Mostafa Madbouly, uliolenga viongozi vijana wenye taaluma mbalimbali za utendaji ndani ya jamii zao ili kuhamisha uzoefu wa maendeleo wa Misri katika uimarishaji wa taasisi na ujenzi wa taswira ya kitaifa.

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mwendelezo wa juhudi za serikali ya Misri baada ya Urais wake wa Umoja wa Afrika mnamo 2019 katika kutekeleza jukumu lake linalolenga kuimarisha jukumu la Vijana waafrika kwa kutoa aina zote za misaada, ukarabati na kutoa mafunzo, pamoja na kuwawezesha katika cheo cha uongozi na kufaidika na uwezo na mawazo yao. Pia unachukuliwa kama mojawapo ya taratibu za utekelezaji wa (Mtazamo wa Misri 2030 - Misingi Kumi ya Shirika la Mshikamano wa Afro-Asia - Ajenda ya Afrika 2063 - Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 - Ushirikiano wa Kusini-Kusini - Mwenendo wa Umoja wa Afrika kuhusu Uwekezaji kwa Vijana - Hati ya Vijana wa Afrika).