Mwakilishi wa Misri ndani ya BRICS .... Ghazaly azungumza kwenye Kongamano la Vijana Wabunge nchini Urusi

Mwakilishi wa Misri ndani ya BRICS .... Ghazaly azungumza kwenye Kongamano la Vijana Wabunge nchini Urusi

Kwa kushirikiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi .. Ghazaly azungumza katika Kongamano la Vijana Wabunge wa Nchi za BRICS

   Ghazaly: Uzoefu wa Bunge la Vijana wa Misri unaweza kuhamishwa kwa nchi za BRICS, kwa kuzingatia sifa za kimuundo kwa taasisi za kazi za vijana 

   Ghazaly: Ushirikiano wa kibunge kati ya nchi za BRICS unatoa nafasi kubwa zaidi kwa shughuli za kijamii kati ya nchi hizo

    Mwanaharakati wa Kimataifa na Mwanaanthropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, alishiriki kama mzungumzaji rasmi anayewakilisha Jamhuri ya Misri kwa kutoa mada yenye kichwa "Uzoefu wa Misri kwenye Kuandaa na Kuwezesha Wabunge na Kujumuisha Vijana katika Mchakbato wa Kisheria" kwenye Kongamano la "Vijana Wabunge wa Nchi za BRICS" lililoandaliwa na Chama cha Kutunga Sheria cha Mkoa wa Novgorod kama shughuli za Kongamano la (Ushirikiano wa Miji na Manispaa za Nchi za BRICS).

    Kongamano hilo lilifunguliwa na Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, aliyeanza hotuba yake kwa kutoa pongezi kwa washiriki kuhusu kufanyika kwa Kongamano hilo mwaka huu kwenye mkoa wa Novgorod, unaojulikana kwa historia yake nzuri na ukarimu wake. Lavrov alithibitisha kwamba kama eneo hilo, kama Urusi nzima, linaonesha dhamira yake ya kujitokeza kwa dunia na tayari kwa maendeleo ya mahusiano ya kimataifa kwa msingi wa heshima, usawa, na maslahi ya pamoja. 

   Lavrov amebainisha kuwa Urusi, inayoshikilia urais wa BRICS mwaka huu, inafanya kazi kuimarisha ushirikiano kamili wa kimkakati ndani ya Chama, na kipaumbele maalumu kilichopewa ushirikiano wa kibinadamu na mawasiliano kati ya watu. Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya miji na manispaa una jukumu kubwa katika juhudi hizi. Alisisitiza kuwa Kongamano hilo limekuwa jukwaa bora la maendeleo ya mazungumzo kati ya mamlaka za mikoa na mitaa, limelosababisha kuanzishwa kwa mahusiano ya karibu kati ya wengi wao. Alisema kuwa kuongezwa kwa wanachama wapya kwenye BRICS mwanzoni mwa mwaka huu kuliongeza uwezekano wa utaratibu huu, kutoa fursa mpya za kubadilishana uzoefu kwenye nyanja mbalimbali za maisha ya mijini. Alitarajia kuwa Kongamano hilo litafanyika katika mazingira ya kazi na ya kirafiki, ambayo yatasaidia kuanzisha mawasiliano yenye manufaa na kujadili miradi ya pamoja ya kuahidi, pamoja na kuimarisha urafiki na uaminifu kati ya nchi za BRICS.

    Kongamano hilo lilihusisha kundi la wazungumzaji muhimu, wakiwemo Gleb Niktin, Mkuu wa Mkoa wa Novgorod, Evgeny Primakov, na Mkuu wa Shirika la Rossotrudnichestvo Bw. Yulen Evgeny Borisovich, Mratibu wa Chama cha Vyama vya Sheria vya Mamlaka za Nchi za mikoa ya Shirikisho la Urusi, na Fouad Jena, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana wa Afrika na Ubora, na Bi. Tatyana Urgomtseva, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Kirusi huko Beijing, na Raymond Matila, Mkuu wa Shirika la Vijana wa BRICS nchini Afrika Kusini (SABYA), Mikhail Solomentsev, pamoja na ushiriki wa wawakilishi kutoka nchi za BRICS.

    Kwa upande wake, Hassan Ghazaly alisisitiza jukumu linaloongezeka la vijana kwenye mchakato wa maamuzi ya kisiasa na sheria katika ngazi za kitaifa na mitaa nchini Misri. Alisema: "Bunge la sasa la Misri linashuhudia uwepo wa idadi kubwa zaidi ya wabunge vijana wanaoshiriki kikamilifu kwenye majadiliano ya sheria na sera, wakati Baraza la Wawakilishi lina kamati muhimu inayoshughulikia masuala ya vijana na michezo, inayoongozwa na Mbunge Mahmoud Hussein, mwanachama wa zamani wa Bunge la Vijana Simulation Model, na mwanachama wa bunge la sasa la Misri, ambayo inamaanisha ufanisi wa shughuli za maandalizi ya viongozi zilizoandaliwa na mashirika ya serikali, ambayo daima huthibitishwa na Waziri wa Vijana wa Misri."

   Ghazaly amesisitiza kazi ya Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa kwenye kuhamasisha ushiriki wa vijana kupitia miradi na mipango ya kitaifa ikiwemo Shule ya Kitaifa ya Maandalizi ya Makada (Bozoor), inayolenga kutoa mafunzo na kuhitimu wanafunzi wanaosoma lugha bila malipo (Kiingereza, Kirusi, Kifaransa, Kiswahili, Kihispania) kwa lengo la kuwaandaa kama mabalozi na viongozi wa kimataifa wanaoamini kwenye maadili ya mshikamano wa kimataifa ili kushiriki kikamilifu kwenye jumuiya ya kimataifa kupitia uwezo wao wa lugha kuwasiliana, kwa kutumia teknolojia imeyoweza kuwezesha mawasiliano ya kimataifa kati ya watu.

   Ghazaly aligusia juhudi za kuwawezesha vijana nchini Misri kupitia taasisi mbalimbali za serikali, muhimu zaidi ni Wizara ya Vijana na Michezo, taasisi muhimu zaidi inayolenga kambi za watu wengi, hasa kupitia vituo vya vijana, na ina jukumu muhimu kupitia shughuli mbalimbali zinazolenga kuendeleza vijana na kuwahamasisha kushiriki katika jamii, niliyokuwa na bahati ya kuwa sehemu ya vituo hivyo vilivyosaidia kuunda upande wangu wa kiakili. Mbali na mifano ya kuiga ya Bunge la Misri na mfano wa  kuiga wa Seneti ya Misri, ambayo ni jukwaa la kufundisha vijana kuhusu uongozi, siasa, utawala na ujuzi wa uwazi, pamoja na vilabu vya vijana na mashirikisho yaliyoandaliwa hivi karibuni kwa namna ya umoja wa ubora wa vyombo vya vijana.

    Ghazaly pia alitaja jukumu muhimu lililochezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na harakati za vijana wa kimataifa zinazotoka Misri, hasa  Harakati ya Nasser kwa Vijana na Taasisi ya Vijana wa Mediterranean, kwenye kutoa fursa halisi za kubadilishana utamaduni.

   Pia alisisitiza nafasi ya Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo kwa Uongozi wa Vijana, kinachofanya kazi ya kuwawezesha vijana wa asili zote, hasa wanawake, na kuwaunganisha katika mipango ya maendeleo, kwa kuzingatia uwakilishi wa kijiografia kwenye ngazi ya Jamhuri.

   Wazungumzaji wakati wa kikao hicho walizungumzia mada kadhaa muhimu, kuanzia ushirikiano wa vijana wa kimataifa, mfumo wa mwingiliano kati ya miundo ya bunge la vijana katika nchi za BRICS, maendeleo ya mabunge ya vijana na mazoea bora katika nchi mbalimbali za BRICS, na mkakati wa mafunzo ya usimamizi katika Jamhuri ya Watu wa China. Wazungumzaji pia walijadili uzoefu wa Bunge la Vijana ndani ya nchi za BRICS, na majadiliano yalishughulikia ushiriki wa vijana katika michakato ya kisheria ya nchi za BRICS: kusoma kesi ya Afrika Kusini, na ushiriki wa Chama cha Wabunge Vijana katika utekelezaji wa sheria nchini Urusi.

    Kikao hicho kilihitimishwa kwa kujadili jukumu la vyuo vikuu katika kuunda uwezo mbalimbali wa usimamizi wa viongozi vijana, na njia za kuimarisha dhana za mshikamano kama nguvu ya kuendesha sera ya vijana katika nchi za BRICS.

    Ni vyema kutajwa kuwa kongamano hili limekuja ndani ya maandalizi ya Kongamano la Mabunge ya BRICS, lililoanza Jumatano, Julai 10 katika mji wa St. Petersburg nchini Urusi na litaendelea hadi Julai 13, ambapo wasemaji wa mabunge katika nchi za kundi la kiuchumi la BRICS na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wanachama, wakiongozwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Misri, Mshauri Dkt. Hanafi Gebali, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana wabunge kati ya nchi wanachama wa kundi hilo.

   Wakati wa Kongamano hilo, Rais Putin alisema kuwa suala la kongamano la sasa ni jukumu la mabunge kwenye kukuza ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo na usalama wa kimataifa tu, ambalo ni suala muhimu sana linalohitaji kusisitiza asili ya mabadiliko ya msingi ya ulimwengu ambayo sayari yetu inashuhudia leo. Rais alibainisha kuwa majadiliano ya wazi na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya wawakilishi wa watu yanaonesha kikamilifu kanuni za BRICS, kwa kuzingatia maslahi ya wengine, kuzingatia demokrasia katika mahusiano ya kimataifa, heshima ya uhuru na haki ya maendeleo ya kujitegemea kwa wote. Aidha, ameongeza kuwa mazungumzo ya bunge leo hasa ndani ya muktadha wa BRICS, yamekuwa muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote, kwani wabunge wanaeleza madai na mahitaji ya mamilioni ya watu kama watetezi wa matakwa ya watu wao na haki zao za kisiasa na kitaifa, zinazochangia kuimarisha demokrasia ya kimataifa.