Mkuu wa Muungano wa Vijana wa Sudan Kusini apongeza Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana kwa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya nne ya Kuanzishwa kwake

Mkuu wa Muungano wa Vijana wa Jamhuri ya Sudan Kusini,Gola Boyoi Gola, alipongeza Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana kwa kuadhimisha Kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwake,ambapo hiyo ilikuja kando ya kongamano la kwanza la mashauriano kwa vijana wa Afrika, lililoandaliwa na Muungano wa Vijana wa Afrika, huko mji mkuu wa Morocco, Rabat, iliyoambatana na Maadhimisho ya Kumbukumbu ya nne ya kuanzishwa kwa Harakati ya Nasser kwa Vijana, na pia sambamba na sherehe za watu huru, na kuadhimisha miaka sabini ya Mapinduzi matukufu ya Julai.

Katika muktadha unaohusiana, Gola Boyoi alitoa salamu zake za dhati kwa serikali na watu wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwa niaba ya watu wa Jamhuri ya Sudan Kusini, kwa uungaji mkono na ufadhili wao wa Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana na Mipango hiyo inafanya kazi ya kuwarekebisha vijana na kuwawezesha, akitoa shukurani zake kwa kiongozi huyo kijana, Hassan Ghazaly, Mwanzilishi na Mratibu mkuu wa harakati hiyo, kwa nafasi kubwa na yenye ushawishi mkubwa anayoifanya kwa vijana wa bara hilo kiujumla, na msaada wake kwa vijana wa Bonde la Mto Nile haswa.

 Boyoi  aliendelea, akiashiria ukubwa wa jukumu la Harakati ya Nasser kwa Vijana, katika kuandaa viongozi halisi kikweli  wenye uwezo wa kuleta nchi zao katika safu ya nchi zilizoendelea, akibainisha kuwa viongozi wengi wa vijana ni wanachama wa harakati hiyo, lililoweza kupata athari kubwa katika nyanja mbalimbali kama vile Utatuzi wa migogoro, Amani na Usalama na mengineyo, nao sasa mi watoa maamuzi na mawaziri katika nchi zao, inayothibitisha kikamilifu jukumu lililotajwa naye mwanzoni mwa hotuba yake, akisisitiza kuwa Afrika lina viongozi wengi bora wanaofanya kazi nzuri ya kujenga nchi zao, na kisha bara lao.

Na kwa upande wake, Mwanzilishi wa Harakati ya  Kimataifa ya Nasser kwa Vijana, Bw.Hassan Ghazaly,  alisifu kwa nguvu ya diplomasia ya vijana ya Jamhuri ya Sudan Kusini, akisema: “Nimeangalia kwa ukaribu ufanisi wa vijana wa Jamhuri ya Sudan Kusini, utamaduni wao mpana na uwezo wao wa kujadili na kusimamia mazungumzo katika programu nyingi za kibara na kimataifa ambazo ilizianzisha, na ikiwa ni pamoja na Kongamano la Kitaifa la kwanza la Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini, Aprili 2021, kama sehemu ya shughuli za Mradi wa Umoja wa Bonde la Mto Nile.. maoni ya baadaye.”

Na Ghazaly alihitimisha akieleza kwamba Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana inakuja kama mojawapo ya njia za kuamsha matarajio ya Ajenda ya Afrika ya 2063, na masharti na malengo ya "Mkataba wa Vijana wa Afrika" ambayo ni mfumo wa kisheria wa uwezeshaji wa vijana,sambamba na Mwelekeo wa Umoja wa Afrika kuwekeza kwa vijana, kama jukwaa la kimataifa la vijana kukuza ujuzi wao, kuinua ufanisi wao na kuwawezesha makada wa vijana ili kufikia Maendeleo Endelevu.