Abd ElNasser na Mambo ya Kale ya Misri 

Abd ElNasser na Mambo ya Kale ya Misri 

Imeandikwa na / Amr Saleh 

Je, Mheshimiwa Rais Gamal Abd ElNasser alipoteza vitu vya kale na hazina ya Misri na aliyagawa Duniani kote kulingana na matakwa yake kama ilivyosemwa na wapinzani Wake?!!

Tutasoma pamoja kitabu cha "sharaja zangu katika siasa na utamaduni " ; kujua ukweli kuhusu shughuli za Rais Gamal Abd ElNasser na Mambo hayo ya Kale ya Misri , ambacho ni pamoja na  Maelezo ya zamani ya Waziri wa zamani sana wa Utamaduni , Dokta Tharwat Okasha haswa sura ya sita ya sehemu ya pili ya sharaja hizo, ikiwa na kichwa "Jaribio langu kama mjumbe katika Baraza la kiutekelezaji la Shirika la UNESCO...Kampeni ya kimataifa ; kuokoa vitu vya kale vya Nuba ".

Vile vile, Dokta Tharwat Okasha ameshika madaraka ya Waziri  wa Utamaduni mnamno 1958 hadi 1962, Kisha wakati wa 1966 hadi 1970 , pia alishika madaraka ya ujumbe wa Misri hadi Kongamano kuu la UNESCO mnamo 1962 hadi 1970 .

Aidha, Dokta huyo  katika sharaja zake anasema kuwa mfumo wa Mapinduzi Julai 23 ni wa kwanza ulioanzisha Kituo maalum; kurekodi na kusoma historia ya Sanaa, Urithi na Ustaarabu wa Misri kwa ajili ya kulinda , kurekodi na kuandika vitu vyote vya Kale vya Misri.

Pia tangu1954, mfumo huo wa Mapinduzi 23 unashughulikia jinsi unavyookoa vitu vya kale vya Nuba huko Misri yakiwemo vitu vya pekee vya kale vyaonesha kilele cha Ustaarabu wa Misri ya kale kama Mahekalu ya Abu Simbel , Elfila na Kalabsha, haswa kuanzishwa kwa Tanki la Aswan mnamo 1902 kulisababisha vitu vya kale huko Nuba viko hatarini mwa kuzama baada ya maji ya Mto Nile yalianza yakivijaa mnamo wakati wa mafuriko kila mwaka,

Pia Dokta huyo anataja kitabu cha mtaalam wa Ufaransa na mwandishi Pierre loti kikiwa na kichwa (Kifo cha ElFila) anatabiri kuficha vitu vyote vya kale  vya Nuba.

Vile vile, Dokta Tharwat Okasha anataja shairi la mkuu wa washairi Ahmed Shwaqi "ewe, mpenzi wa Aswan kama nyumba yako" ambaye ameiandika mnamo 1910, ambapo ndani yake anaeleza hali za vitu vya kale vya Aswan kupitia neti zifuatazo : 

Angalia mambo ya kale haya yaliyozamwa bahrini.

Hayo yapo pamoja yakiwa na hofu 

Kama wasichana bado hawajaolewa wakiogpa bahari .

Hayo ndiyo ya nazama ndani yake 

Yanakaribia kupotea baharini

Baada ya yalikuwa juu kama Sayari .

Dokta huyo anasema kuwa mwanzo wa Kampeni halisi ya kuokoa vitu vya kale huko Nuba ilianza mnamo 1958, pamoja na kutekeleza mradi wa bwawa la Juu ambazo tafaiti zilithibitisha kuwa ziwa litakaloanzisha nyuma lake litazama vitu vyote vya kale huko Nuba , pia Dokta Okasha anataja kuwa fikra za serikali ya Misri katika Kampeni ya kuokoa vitu vya kale zilianza baada ya matembezi ya  Balozi wa Marekani huko Kairo pamoja na mkurgunzi wa makumbusho ya Marekani ya Metro Politan kwa ofisi ya Dokta Tharwat Okasha ili Balozi wa Marekani kuomba kununua Mahekalu yote na vitu vya kale vya Nuba yanayotarajiwa kuyazama baada ya kujenga Bwawa la Juu .

Pia Dokta Okasha anasema kwamba aliomba kukutana na Mheshimiwa Rais Gamal Abd ElNasser baada ya pendekzo la Balozi wa Marekani ,na hilo lilimchekesha Rais, ambapo  alidharau kukataa kwa Wamarekani kuchangia kujenga Bwawa la Juu kisha wanafanya juu chini ; kutumia mchakato wa ujenzi wa kutawala Vitu vya kale nchini humo .

Wakati wa mkutano wake pamoja na Rais Gamal Abd ElNasser , Dokta huyo alionesha mpango wake; kuokoa vitu vya kale vya Nuba , pia aliomba msaada wake katika sherehe zote za kimataifa hadi Kampeni hiyo kuokoa hivyo itafanikiwa.

Aidha,  mradi wa kuokoa vitu vya kale huko Nuba umeshatekelezwa kwa msaada wa kisiasa na kifedha wa serikali ya Misri mnamo 1958 hadi 1968, pia kwa uratibu pamoja na Shirika la UNESCO na nchi kadhaa za Dunia .

Pia Dokta huyo aliandika kazi zote za Kampeni hiyo ndani ya kitabu chake (Mwanadamu wa Sasa anatawaza Mfalme Ramses) na toleo lake la kwanza la kiarabu lilitolea kutoka kwa Shirika la kitabu cha Misri mnamo 1971,Kisha Shirika la UNESCO limekitafsiri kwa Kifaransa kwa gharama zake na kukisambaza Duniani kote .

Vile vile, Wizara ya Utamaduni wa Misri alimwambia Mtoaji wa Senima wa Canda "John Finney " kutengeneza filamu kuhusu Vitu vya kale vya Nuba na mchakato wa kuviokao , utengezaji wa filamu hiyo ilichukua miaka minne , pia ilitolewa ikiwa na kichwa " Ajabu ya nane" , na hicho chaeleza mchakato wa kuokoa vitu vya kale vya Nuba kama "Ajabu ya nane ya Dunia " .

Aidha, Kampeni ya Misri ilisabibisha kuokoa vitu vya kale vya Nuba huko Sudan .

Vilevile, Kampeni hiyo haitoshi kuhusu Vitu vya kale viko hatarini mwa kuzama hapa tu, bali iliweza kwa juhudi za makumi ya jumbe za kimisri na kigeni zilizotafuta huko Nuba kugundua vitu vipya vya kale vya Misri wakati wa Kampeni hiyo ,vinavyoshikilia aghlabu ya vitu muhimu vya makumbusho huko Nuba vya vitu vya kale hivi sasa.

Pia, hiyo ndiyo iligharimu Dola milioni 80 za kimarekani, ambapo Misri ililipa theluthi moja yao, ilhali Marekani ,Ujerumani, Ufaransa, Uhispania na Uholanzi na shirika la UNESCO ziligharimu theluthi mbili iliyobaki ya gharama nzima 

Kampeni hiyo yazingatiwa mradi wa kwanza na mkubwa zaidi wa Utamaduni ; kulinda Urithi wa Dunia wakati wa historia ya sasa, pia mchakato wa kuvunjwa na kujenga tena hekalu la Abu Simble juu ya mlima wa Abu Simble unazingatiwa kazi ya kipekee ya Usanifu, Uhandisi na Jiolojia mnamo wakati huo, mchakato huo wenye gharama ya Kampeni nzima .

Pia nchi fadhili ziliweka masharti kupata baadhi ya vitu vya kale vya Misri mbele ya michango yake katika kuokoa vitu vya kale huko Nuba, Kwa hivyo kamati imeandaliwa na waatalam wa Shirika la Vitu vya kale vya Misri ; kuainisha na kuteua vitu hivyo vya kale .

Vilevile, kamati hiyo iliamua kutoa hekalu la Dndo kwa Marekani, hekalu la Tafa la Uholanzi , nayo Mahekalu madogo yalikuwa yakitawanyika kama vipande visivyo kamili huko Nuba, pia vimehamishwa nchi tatu ambapo imeyarudishwa upya na imejengwa tena,pia imetolewa hekalu la Lycian Kwa Italia na Kisiwa cha Amenhotep ya nne kwa Ufaransa.

Hiyo ndiyo hadithi halisi kupitia hati ambayo imeandikwa na Shujaa mkuu wa kampeni ya kuokoa vitu vya kale mjini Nuba .

Pia jambo la kuchekesha ,kuwa kundi la Shamshirji, Uliberali na Udugu wanaposhataki Rais Gamal Abd ElNasser , wanasahau kwamba mchakato mkubwa zaidi wa kupora vitu vya kale huko Misri umeanza wakati wa Kampeni ya Ufaransa mnamo 1798 hadi zama la familia ya Juu.

Kwa mfano:

Nchini Ufaransa zipo obeliski 4 za kimisri,  tatu zimeibwa wakati wa Kampeni ya Ufaransa mnamo (1798_1801), Mohamed Ali Pash ametoa ya nne kwa Ufaransa mnamo 1833,ambapo ilikuwa Iko kwenya lango la hekalu la Luxor, lakini Sasa hivi iko Uwanja wa Concrde huko Paris .

Na ndani ya makumbusho ya Louvre ziko barakoa ya dhahabu ya Nefertiti , sanamu ya mwandishi wa Misri, sanamu ya Mfalme Ramsisi wa pili ll , sanamu ya Mfamle wa Akhenaten, sanamu ya Mfalme wa Amenhotep, pamoja na idadi kubwa sana ya mabaki ya Misri na zaidi ya vipande elfu 50 katika makumbusho hiyo hadi imepanuliwa makubusho hayo ; kujumuisha kumbi mpya 31 Ili kuchukua vipande vya kale vya Misri ambavyo vilitekwa na Wafaransa wakati wa Kampeni zao wa Uvamizi wa Misri, na vitu vya kale amabao Mohamed Ali Pash , wanawe, na wajukuu wake wametoa kwa Ufaransa mnamo zama la familia ya Juu .

Aidha,Jiwe la Rosetta liko katika makumbusho ya Uingereza kule , pia makumbesho ya Uingereza yaainisha vyumba 7; kuonesha mambo ya kale ya Misri yanayofikia vipande vya kale laki 100 vinavyotofautiana kati ya sanamu za kale , maiti , samani, johari na nyaraka za kihistoria .

Pia, mnamo 2001, imetolewa kwa makumbusho ya Uingereza kundi la Wendolf, linajumuisha vitu vya kale milioni 6 vinarudi zama zamani kabla ya historia huko Misri na Sudan, pia obeliski ya Misri ambayo imeshatolewa na Mohamed Ali pasha Kwa Waingereza Iko huko mnamo 1831, na imejengwa katika uwanja uko mbele na Mto wa Thames, mnamo 1826 Mohamed Ali Pasha ametoa Mfalme wa Ufaransa" Louis Philip" obeliski ya Misri imeshajengwa ndani ya uwanja wa Concorde kati ya mji mkuu wa Ufaransa Paris , mnamo 1879  Khedive Ismael ametoa obeliski nyingine ya Misri huko Marekani, naye imejengwa katika hifadhi ya Sintiral Park mjini New York sasa hivi .

Mnamo 1832, mtawala wa Misri Mohamed Ali Pasha aliuza sanamu mbili bora zinazotengenzwa Kwa itale kuhusu simba wa kichwa cha mwanadamu inaonesha Mfalme wa Misri " Amenhotep wa tatu lll" mwenye nafasi ya Tisa wa wafalme wa familia Kumi na nane, ambaye ametawala Misri mnamo ( 1391B.C hadi 1393 B.C) kwa Mfalme wa Urusi Nicholas wa kwanza zenye thamani ruble elfu 64.

Mwanzoni, Mohamed Ali pasha ameuza sanamu mbili kwa Mfalme wa Ufaransa " Charle wa Kumi ) lakini uzinduzi wa Mapinduzi Julai 1830 inayopinga Kwa Utawala wa Charle wa Kumi, ulifanya mktaba wa kuuza sanamu mbili zilihamia mfalme wa Urusi "Nicholas wa kwanza" 

Aidha, baada ya kufikia sanamu mbili huko Urusi zilihamishwa mji "Saint Petersburg" wakati ambapo zimeshawekwa mbele na bahari kuelekea Chuo Kikuu cha Mji huo.

Mnamo 1912,mtaalam wa Urusi Facilia Struve aliweza kutafssiri maandishi ya  hierglyphic yanayokwepo sanamu mbili, na maandishi yako yalikuwa yafuatayo:

"Adumu Horus , mfalme mkuu atendaye vizuri kwa hakika, na anaweka kanuni sheria na ajaliye ardhi, Horus wa dhahabu, Mfalme mkuu wa wafalme wote, mshindi wa maadui Tisa , Mfalme wa Misri ya Juu na chini , bwana na mmiliki wa ardhi Amenophis wa tatu lll mwana wa Mfalme Ra .

Mwana wa Ra mpendwa Amenhotep , mtawala wa Tipa , na picha ya Ra mbele ya watu wote .

Mmiliki mzuri wa milele .... Mmiliki wa maisha, utulivu, Furaha na Afya " .

Sanamu mbili kama umbo wa Abu Alhol zenye gharama robl elfu 64.

Pia, huko Italia Iko makumbusho MuseoEgizie inayojumuisha vipande vya kale 32500, vikiwemo sanamu za Miungu, majeneza, johari zinazohusisha wafalme, Wamisri wa kale na zana zao katika maisha ya kawaida .

Pia mnamo 1824, makumbusho hiyo imeaznzishwa na vitu vyake vyote ni mambo ya kale ya Misri amvavyo viliporwa na kuviibwa kutoka Misri kabla ya kuanzisha kwake, na mchakato huo uliendelea haswa baada ya kuianzisha wakati wa Utawala wa familia ya Mohamed Ali , haswa mnamo zama la Mfalme Fauad wa kwanza ambaye alikuwa akipenda Waitalia , pia wafuasi wake wengi ni waitalia wanaokaa huko Misri .

Pia ramani ya mambo ya kale ya Misri yanayoparwa na kuyaibwa ambayo imeshatolewa na watawala wa familia ya Mohamed Ali haifikii Ufaransa ,Uingereza na Itali tu , bali inaendelea Marekani , Ujerumani, Urusi, Denmark na nchi nyingine za Ulaya. 

Vilevile, Profesa Mukhter Al_Suwaifi katika utangulizi wake wa elezo Misri ya kale_ lililotungwa na mtaalam Mmisri wa akiolojia Dokta Saleem Hassan aliiandika akigundua sababu ya kustaafu Kwa Saleem Hassan mwenye umri 46?! 

Mnamo1936, Dokta Saleem Hassan alikuwa Mmisri wa kwanza anafanya kazi kama mwakilishi wa taasisi ya mambo ya kale ya Misri , ilhali aliandika taarifa ya vitu vya kale viko hapa, aligundua kuna kundi la mambo ya kale ambapo Mfalme Fauad alilichukua na alilihifadhi huko jumba lake, kisha akapiga simu wa Ikulu ; kulirudi Tena, kwa kweli imelirudi tena Kwa Taasisi na imelioneshwa katika makumbusho ya Misri huko Kairo , baada ya Kifo cha Mfalme Fouad, na Mfalme Farouk ameshika madaraka , Mfalme hyuo alitumia taasisi ya mambo ya kale anaiomba kurudi vitu vya kale anaiomba kurudi vitu vya kale kwa kuvizingatiwa Urithi wake kutoka kwa baba yake, lakini Dokta Saleem Hassan alimjibu Mfalme Farouk kuwa mambo hayo ya Kale ni ya Misri na alikataa kurudi tena, vitu hivyo vya kale kwa Ikulu hiyo.

Pia uamuzi wa Saleem Hassan ulisababisha hasira ya Mfamle Farouk kwake, Kwa hivyo aliendelea anajaribu kumuondoa hadi alifanikia katika lengo lake kwa kutoa uamuzi wa kustaafu kwa Dokta Saleem Hassan mnamo1939. baada ya alimsumbua katika kazi yake.

Pia Dokta Sleem Hassan baada ya kustaafu kwake alishughulikia kufanya elezo lake lenye sehemu Kumi na sita kwa historia ya Misri kale, ambalo lazingatiwa elezo muhimu zaidi la historia ya Misri ya kale , pamoja na kitabu chake muhimu kuhusu fasihi ya Misri ya kale .

Pia, Profesa Mukhter Al_Swaify anaongeza katika utangaulizi wake kuwa hali za Dokta Sleem Hassan zimebadilika zikawa bora baada ya Mapinduzi Julai 23 mnamo 1952, Mheshimiwa Rais Gamal Abd ElNasser amehurumia pamoja mtaalam huyo mkuu , na aliijua nafasi yake kubwa kwa Misri na Wamisri wote, Kwa hivyo akatoa uamuzi kumtembelea makumbusho ya Dunia yanayoonesha vipande vya Kale vya Misri ...

 Pia aliamua kumteua mshsuri wa makumbusho ya Misri huko Kairo mnamo1959.... Aidha, wakati wa 1960 ... Taaluma ya New York inayojumuisha zaidi ya waatalam 1500 kutoka nchi 57 ilimheshimu na kumchagua kama mjumbe ndani  yake kwa kauli Moja .

Vilevile, kundi la Shammsherji , Uliberali na Udugu na wafuasi wake Kwa kuharibu picha ya Gamal Abd ElNasser wanategemea kikubwa kusema Uwongo kisha kuurudia tena; ubadilike kweli kabisa, au kuchukua habari na kuisema kwa njia sio sahihi Ili kuharibu ukweli wa tukio maalum la kihistoria.

Pia, njia chafu hizo katika kupotosha historia na mashujaa wake haziwezi kusimama mbele ya kweli, vyeti na hati .

Mheshimiwa Rais Gamal Abd ElNasser hakupotea mambo ya kale ya Misri bali aliyaokoa kutoka kuzama na kupotea , alisaidia Kampeni ya kuokoa ya mamilioni ya dola,ingawa kushindwa kwa vita 1967 ila serkali ya Misri iliendelea kusaidia kampeni hiyo hadi imeadhinishwa rasmi kwa kumaliza hiyo kwa mafanikio mnamo Septemba 22, 1968, sio hivyo tu bali imeandikwa na kurekdiwa vitu vyote vya kale vya Misri kwa mara ya kwanza katika historia ya Misri, kwa sababu ya juhudi za Kampeni hiyo imegunduliwa maelfu ya vitu vipya vya Misri vya kale .

Picha hiyo wa posta la Misri ilitolewa miongoni mwa matukio ya kampeni ya kimataifa ; kuokoa mambo ya kale ya Misri mnamo 1963.

Marejeleo

Kitabu" sharaja zangu katika siasa na utamaduni_ sehemu ya pili : sharaja za DKT. Tharwat Okasha .

Kitabu "Ensaiklopedia ya Misri ya kale": DKT.Selim Hassan.