Abd El Nasser wakati wa kikao chake cha kwanza na kiongozi wa India Nehru

Abd El Nasser wakati wa kikao chake cha kwanza na kiongozi wa India Nehru

Rais Gamal Abd El Nasser alikutana na kiongozi wa India “Nehru” kwa mara ya kwanza Februari 15, 1955. Nasser alikuwa na umri wa miaka thelathini na saba, kwani alizaliwa Januari 15, 1918. Ama kuhusu Nehru, alikuwa na umri wa miaka sitini na nne. Ambapo alizaliwa manmo Novemba 14, 1889,” na alikuwa Waziri mkuu wa nchi yake tangu uhuru wake Agosti 15, 1947, na licha ya tofauti ya umri, “kila mmoja wao aliacha athari kubwa na yenye nguvu kwa mwenzake,” kulingana na Muhammad Hassanein Heikal. katika kitabu chake “Abd El Nasser na Ulimwengu” akiongeza kuwa : “Uhusiano uliokuwepo kati yao umekuwa na kina na nguvu kama  upendo tangu mara ya kwanza, na kama inavyotokea mara nyingi, uhusiano  huu ulianzishwa kati ya watu wawili tofauti kabisa.

 Abd El Nasser alikuwa mkubwa na mwenye nguvu, na alikuwa mtu wa vitendo vikweli, ama Nehru alikuwa mwembamba na alikuwa mtu wa mawazo ya Utamaduni.

Haikal anamchunguza Nehru, akisema: "Aliathiriwa na mawazo ya Kiislamu ... Hinduki alizaliwa katika mji wa Kiislamu wa Ahmedabad. Upande wa kiakili alikuwa karibu na Uislamu. Alizungumza kwa urefu kuhusu wanafalsafa wa Kiislamu, na alivutiwa na historia ya Kiislamu."Haikal anaona: “Labda hisia yake ya historia ni iliyompa sifa ya mtazamo wenye kina na upana, na alikuwa na akili ambayo iliweza kufahamu Umoja wa Ulimwengu na Umoja wa Historia,alipokuwa akipambana tatizo hurudi historia kutafutia suluhisho kwake kutoka historia na Teito"Kiongozi wa Yugoslavia" amekuwa kufanya mzaha Pamoja naye akisema, "kila kitu pamoja na Nehru huanza kabla ya Kuzaliwa."

Haikal anasisitiza kwamba: “Nasser ameona Nehru kama mtu anayeweza kufikiri, anayeweza kuchunguza tatizo kutokana na vipengele vyake vyote na kuvijadili, na kubainisha kwa njia ya kimantiki mizizi yake, chimbuko, athari zake, na suluhisho linalofaa kwake.hivyo imekuwa ni upande wa kimantiki ambao ulivuta Nasser Kwa upande mwingine Nehru, amehisi hisia ya baba kwa mtoto wake, na kama ilivyo kwa baba wote, kulikuwa na mambo katika mtoto wake ambayo yalimvutia na kumtia hofu wakati huo huo.. Alivutiwa na ujasiri wa Nasser. lakini aliogopa  kutoka kwake.. Alijivunia uwezo wa Abd El Nasser wa kufanya kazi.Na alikuwa akimuonea wivu, lakini pia alimwogopa, kama baba msomi, mwenye akili, ambaye mtoto wake huelekea kipaji ca  kupanda milima.

Hii imekuwa maudhui ya mkutano wao, , na Haikal ametaja kwamba ziara ya Nehru ilichukua siku tatu, na anasisitiza kwamba: “Mambo yalikwenda sawa kadiri walivyoweza, kiasi kwamba Abd El Nasser aliamua kutenga siku nzima kuzungumza naye mbali na taratibu rasmi, na kwa hiyo akapanga wapitishe siku nzima kwa meli ya Nile, kuondoka kutoka Hoteli ya Semiramis hadi Qanatir al-Khairia, na ilichukua masaa manne kwa kwenda, na pia kurudi, na wamechukwa muda wote kuzungumzana, isipokuwa kipindi cha kula chakula cha mchana, Nasser alitaka kuanzisha tena mazungumzo kwa haraka, lakini Nehru alikataa, akisema: “Lazima tupe sisi wakati wa kulala usingizi.”

Naye akakaa juu ya kiti chake, akaangaza macho yake yaelekee ukingo wa mto Nile, kisha akalala kwa dakika tano, kisha akaamka tayari, Nasser ameanza mazungumzo mnamo asubuhi kwa kusema "jana tumezungumza kwa njia rasmi lakini nataka wewe leo nizungumzie kuhusu kupanga" Heikal asema: "Hakujua kuhusu kupanga elimu ya kutosha, kwani hakuwa na uzoefu wa awali katika kupanga mustakabali wa taifa, na aliamini kwamba kiongozi huyo wa Kihindi alikuwa amepata uzoefu huo, na hivyo Nehru aliuliza haswa: 'Tunapangaje? "

Haikal anaongeza: “Walitumia asubuhi kuzungumzana kupanga, na meli ilikuwa ikipitia Mto Nile kupitia vijiji vya kale, kiasi kwamba neno kupanga halikujulikana katika ulimwengu huo.. Wakati wa mazungumzo haya, Nehru alimwambia Abd El Nasser: “Ningependelea kama ningeweza kuachana na siasa kabisa, na kujikita katika kupanga kwa sababu ni Uwanja ambao mtu ana nafasi ya kutimiza jambo fulani." Nehru alisema hayo tena na kuzama katika mojawapo ya msungo wa mawazo ambayo ilikuwa ni tabia yake. kisha akaendelea, “Hata hivyo, nina shaka ikiwa iko katika uwezo wa mtu ye yote kutimiza mambo yote anayotaka".

Haikal asema hivi: “Nehru alikuwa akitoa maoni siku zote, kisha akayafikiria, kisha akarudi na kuyasema, na kuyaacha, na labda hiyo ilikuwa ni kwa sababu alikuwa kufikiri sana.”

Haikal anaendelea kusema: “baada ya Adhuhuri mazungumzo yaligeuka kuwa masuala ya kimataifa.. Nehru alitaka nchi za ulimwengu kutambua China ya kikomunisti.Alisema: “China ni kama milima ya Himalaya.Hakuna anayeweza kusema kwamba Himalaya haupo Asia. , na ukipuuza kuwepo kwao, unapuuza kitu kweli kabla ya yote.”, na pili, unajinyima kugundua kilicho nyuma yake.. Pia alipendezwa sana na atomu, na alikuwa akisema: “ Inamaanisha nguvu katika Vita na Amani, iwe kwa ushindi au kwa kuongeza uzalishaji.”

Haikal akieleza : "Si masuala madogo-madogo yaliyomvutia... Alipendelea kuchora michoro mikubwa yenye masomo makubwa, mada kama vile Elimu, Vita na Amani."

Haikal anasisitiza: “Mazungumzo yao yaliendelea siku nzima, yule mwanamapinduzi kijana Mwarabu alipokuwa akimsikiliza kwa moyo wake wote mwanafikra huyo wa Kihindi mwenye uzoefu.mazungumzo yao yaliendelea kati ya yule wa kwanza kwa akili na mawazo yake pia na wa pili  anayeyumbayumba na kutoridhishwa kiakili.. Hata hivyo, Nehru alimwambia Abd El Nasser siku hiyo: “Kadiri tulivyozungumza zaidi, ndivyo tulivyosadikishwa zaidi kwamba tuna mawazo sawa.