Rais wa Namibia "Sam Nujoma" akizungumzia Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser

Katika Julai na Septemba ya mwaka wa 1970, tuliwapotea watu wawili muhimu katika historia yetu, ambao mimi mwenyewe nilihuzunika.
Watu hao wawili walikuwa kiongozi (Hosea Kotaku), baba wa mapambano yetu kufikia uhuru na Rais (Gamal Abdel Nasser) Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Umoja, rafiki wa karibu ambaye alikuwa na nia ya kutetea maslahi yetu na ana uwezo wa kutusaidia katika ulimwengu ulio nje.
Rais Abdel Nasser aliweka imani yake katika Jumuiya ya watu wa Kusini-Magharibi mwa Afrika tangu hatua za mwanzo. Nami nilipeleka telegramu kwa serikali ya Jamhuri ya Kiarabu ya Umoja nikisema:
"Ulimwengu ilimpoteza mtu adhimu na wale wote wanaopigania uhuru na utu wa kibinadamu wamepoteza ndugu mmoja katika mapambano, Watu wa Namibia wanaelezea masikitiko yao kufuatia kifo cha ghafla cha Rais Abdel Nasser".
Mimi pia nilishiriki katika mazishi ya Rais Abdel Nasser huko Kairo, ambapo yalihudhuriwa na idadi kubwa ya maafisa wa kimataifa kutoka Duniani kote.
Nasser amekuwa msukumo mkubwa kwetu nchini Namibia tangu mwaka wa 1956 wakati alipopiga vita na Waingereza, Wafaransa na Waisraeli baada ya kudhibiti Mfereji wa Suez.
Wakati tuliposoma kuhusu mapigano magazetini katika Kusini-Magharibi mwa Afrika, tulisimama kwa nguvu upande wa Misri.
Vita vya Suez viliwahamasisha na kuwaunganisha Watu wa Misri, na viongozi wa Afrika Kaskazini kama vile Nasser na wengine Barani Asia walikuwa chanzo cha msukumo wa kisiasa kwetu katika sehemu za Afrika zilizotawaliwa na kukaliwa na wakoloni.
ــــــــ
Kutoka wasifu wa Kiongozi wa Namibia "Sam Nujoma" Rais wa Kwanza wa Namibia baada ya uhuru wake mnamo mwaka wa 1990.