Nafurahi kuona roho ya mapambano ya pamoja kati ya Nchi za Kiarabu

Imefasiriwa na / Abdullah Nasser Farahat
Nafurahi sana kwa fursa hii ambapo naona wajumbe Waarabu wakikutana kwenye Mkutano wa Wanasheria, tena ninafurahi pia kuona roho ya mapambano ya pamoja inayopatikana kati ya nchi za Kiarabu. Na Historia ndefu ya mapambano haikuishia kwa nchi moja bila ya nyingine, bali yalikuwa mapambano endelevu ambayo athari yake ilioneshwa kutoka nchi moja hadi nyingine. Nasi pia tunachota kutoka kwenu moyo wa mapambano, na tunahisi msaada wenu kwetu katika masuala yetu makuu, ambayo ni masuala yenu pia.
Natumai Mkutano huu, unaoleta pamoja Matumaini ya Utaifa wa Kiarabu, uwe nyenzo madhubuti ya kuimarisha Utaifa huo na kuinua hadhi yake, pia natumai utakuwa ni nguzo muhimu sana katika kuimarisha viunganishi kati ya watu wote wa nchi hizi.
Nina furaha pia kwamba Mkutano huo unashughulikia mnamo siku zijazo;ili kufikia lengo hili kuu ambalo Uarabu umekuwa ukitafuta daima katika sehemu zote za Dunia; nao ni unganishi mzito kati ya Utaifa huu mmoja ambao nguvu mbalimbali zilijitahidi kutenganisha, na hautatenganishwa kamwe.
Na ninahisi kuwa nipo miongoni mwa ndugu zangu na familia yangu, kwani ninyi si wageni kwetu, na nadhani kwamba mlihisi hivyo pia, na ninaamini kwamba mtahisi hisia hiyo hiyo mnamo kipindi ambacho mtakaa hapa; Mnahisi kuwa mko nyumbani mwenu na pamoja na ndugu zenu na familia yenu.
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika ujumbe wa Wanasheria waarabu.
Mnamo Februari 27, 1956