Kila Jaribio la Ulinzi wa Mashariki ya Kati lazima ukabidhiwe na watu wake

Kila Jaribio la Ulinzi wa Mashariki ya Kati lazima ukabidhiwe na watu wake

Imefasiriwa na / Ali Mahmoud

Uchokozi wa Israeli ukiendelea, itakuwa vigumu sana kudhibiti hatamu za wakimbizi wa Kiarabu huko Gaza, wakimbizi hawa masikini wamekuwa wakitumaini bure kwamba Umoja wa Mataifa utafanya chochote cha kutatua shida zao na kuwarudishia ardhi ya wazazi wao na babu zao; uvamizi wa hivi karibuni wa Israeli ulikuja na ulionesha kutojali kwa Israeli kwa Umoja wa Mataifa na kuudharau na uliharibu matumaini yote mengine ya wakimbizi, ilikuwa kawaida kwao kuasi dhidi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaotunza mambo yao; kwa sababu wanawaona kama alama ya nchi hizo ambazo zilikuwa sababu ya dhiki na maafa ambazo ziliwakabili.

Ninaweza kuwahakikishia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwamba serikali ya Misri imechukua na itaendelea kuchukua kila hatua iwezekanavyo ili kuwalinda.

Watu wa Mashariki ya Kati, ambao kwa muda mrefu wameteseka na udhibiti wa kigeni, wana shaka katika kila hati inayoungwa mkono – kwa hali yoyote – na nchi za kigeni ambazo zimewadhibiti kwa muda mrefu.

Kila Jaribio la Ulinzi wa Mashariki ya Kati lazima ukabidhiwe na watu wake wenyewe, na ulinzi wa eneo hilo unategemea misingi miwili: wa kwanza ni ulinzi wa ndani; kwa kuinua kiwango cha maisha, hatari ya vitu vya uharibifu na watetezi wa maoni ya kupotosha itaondolewa. Na wa pili ni ulinzi wa nje, nalo linapaswa kuachwa kwa watu wa eneo hilo kulisimamia kulingana na masilahi yao sio kwa masilahi ya mtu mwingine.

ــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــ

Kauli ua Rais Gamal Abdel Nasser kwa Gazeti La “Daily Mail” kutoka Kairo

Mnamo Machi 19, 1955.