Mahusiano ya Brazili-Misri baada ya Mapinduzi ya Julai 23, 1952

Mahusiano ya Brazili-Misri baada ya Mapinduzi ya Julai 23, 1952

Baada ya Misri ilikabiliwa na mashambulizi ya pande tatu mwaka wa 1956, kutokana na uamuzi wa Abdel Nasser wa kutaifisha mfereji wa Suez, Baraza la Usalama lilifanya mkutano wa dharura na Brazili ilikuwa ikiongoza nchi zilizokataa vita hii, na iliomba kwa uondoaji wa majeshi yote kutoka nchi ya Misri, na mjumbe wake aliomba kwa kuheshimu utawala wa Misri na ilipiga kura kwa ajili ya Misri.

 

Pia ilitoa mswada wa azimio katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Desemba ,1956, unatia ndani kutoa ada kwa 3% kwa meli zilizopita kupitia mfereji huu kukidhi gharama za kusafisha mfereji huo. Baada ya Israel ilijiondoa kutoka Sinai, Brazil ilishiriki kwa vikosi vya kimataifa vya dharura katika eneo la Sinai, Sharm El-Sheikh na Gaza, baada ya idhini ya Serikali ya Misri.

 

Mbali na hayo, Brazili ilikuwa miongoni mwa Nchi za harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, ambayo Gamal Abdel Nasser alikuwa mmoja wa waanzilishi wake, kwa lengo la kuondoa ukoloni na kuepusha kwa sera zilizosababishwa na Vita Baridi kati ya kambi za magharibi na mashariki.