Soko la Pamoja la Kusini na mahusiano ya Misri na MERCOSUR

Soko la Pamoja la Kusini na mahusiano ya Misri na MERCOSUR

Imefasiriwa na / Osama Mostafa

Mnamo miaka ya hivi karibuni, Misri iliweza kuweka makubaliano ya pamoja na  Nchi za Shirikisho la Soko la Pamoja la Kusini, ambayo ni moja ya vikundi muhimu vya kiuchumi huko Amerika ya Kusini, ambayo inajumuisha Brazil, Argentina, Uruguay na Paraguay.

Mkataba wa biashara huria unatoa fursa za upendeleo kwa mauzo ya nje ya Misri kuingia katika masoko ya Amerika Kusini na kupunguza gharama ya uagizaji wa Misri kutoka nchi za Amerika Kusini kama vile sukari, nyama na mafuta ya soya.

Makubaliano hayo yanalenga kupunguza ushuru wa forodha kwa zaidi ya 90% kati ya Misri na nchi za MERCOSUR na kufuta ushuru wa forodha kwa bidhaa za kilimo, na Makubaliano hayo yanajumuisha maeneo kadhaa yenye matumaini ya ushirikiano kati ya Misri na nchi za Jumuiya hiyo katika bidhaa na huduma mbalimbali. ikiwa ni pamoja na biashara ya nyama, maziwa, sukari, malisho, karatasi na kuni, na kufungua njia ya kuanzisha miradi Ubia katika sekta ya usindikaji wa chakula na juisi, pamoja na ushirikiano katika nyanja za utengenezaji wa magari, vifaa vya umeme na injini.
Hayo si yanayohusishwa na makubaliano, ila pia  hufanya kazi ili kupanua ujuzi wa pamoja kuhusu fursa za biashara na uwekezaji kwa pande zote mbili. Pande zinazoingia kandarasi huongeza shughuli za maendeleo ya biashara kama vile kufanya semina, misheni ya biashara, maonesho, semina na masoko.

Pande zinazoingia kandarasi zinafanya kazi ili kukuza maendeleo ya shughuli za pamoja zinazolenga kutekeleza miradi ya ushirikiano katika nyanja za kilimo na viwanda, miongoni mwa mambo mengine, kupitia kubadilishana taarifa, programu za mafunzo, na misheni za kiufundi.

mahusiano ya Misri na nchi za Kilatini yana sifa ya maelewano makubwa ya kisiasa na kina ambayo yanaenea hadi takriban miongo sita, kwa kipindi ambacho mizizi yake inarudi nyuma hadi enzi za kiongozi wa mwisho Gamal Abdel Nasser, na Makubaliano ya Biashara huria ya Kidini pamoja na Nchi za MERCOSUR tangu 2010 hadi sasa, nazo ni alama kuu za mahusiano hayo kwa upande wa ushirikiano wa kibiashara, kiutamaduni na kiuchumi.