Mahusiano ya Sudan na Misri baada ya mapinduzi ya 23 julai, 1956

Mahusiano ya Sudan na Misri baada ya mapinduzi ya 23 julai, 1956

Mahusiano ya Sudan na Misri yaliimarishwa kwa kiasi kikubwa wakati wa enzi ya Rais Abdel Nasser, ambapo Misri ilikuwa nchi ya kwanza kutambua Uhuru wa Sudan mwaka 1956.  Katika vita vya Juni 1967, kikosi cha askari wa miguu cha Sudan kilishiriki katika kusaidia majeshi ya Misri.  Uwepo wake pamoja na Misri uliendelea hadi 1971;  Kikosi hicho kiliongezeka maradufu na kuwa brigedi inayounga mkono Jeshi la Tatu la ardhi hadi Agosti 1972.

 

Mkataba wa biashara, forodha na usafiri ulitiwa saini kati ya nchi hizo mbili mnamo 1965.  Mnamo 1962, makubaliano ya usafiri wa anga yalitiwa saini kati ya nchi hizo mbili.

 

Tangu mwaka wa 1956, shule za misheni za elimu za Misri zimechangia kujenga mfumo wa elimu nchini Sudan, na mojawapo ya shule kubwa zaidi za Misri nchini Sudan ilikuwa Shule ya Sekondari ya Gamal Abdel Nasser huko Khartoum.

 Mnamo 1956, Rais Gamal Abdel Nasser alitoa amri ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Kairo, tawi la Khartoum.

 

Katika nyanja za fasihi na sanaa, idadi kadhaa ya waandishi wa Sudan wamejitokeza nchini Misri; miongoni mwao ni Al-Tayyib Salih, aliyowasilishwa na mhakiki Raja Al-Naqqash, na alichapisha riwaya yake ya kwanza mnamo 1969 nayo ni "Msimu wa uhamiaji kuelekea Kaskazini".  Mnamo 1968, Bi. Umm Kulthum alitembelea Khartoum, ambapo alitumbuiza matamasha mawili kwenye ukumbi wa Kitaifa wa Om Durman.

 

Katika Harakati ya Nasser kwa Vijana tunaona kwamba mahusiano baina ya nchi hizo mbili ni mahusiano yaliyojaliwa na Mwenyezi Mungu hadi Siku ya Kiyama.