Miaka 52 tangu Mauaji ya Bahr El- Baqar (Aprili 1970)

Miaka 52 tangu Mauaji ya Bahr El- Baqar (Aprili 1970)
Miaka 52 tangu Mauaji ya Bahr El- Baqar (Aprili 1970)

Jumatano asubuhi , Aprili 8, 1970, wakati wa vita vya Kudhoofisha vilivyoanzishwa na Misri dhidi ya Israel, ndege 5 za "Phantom" za Israel zilivamia - kwa zaidi ya dakika 10 mfululizo - kwenye "Shule ya Msingi ya Bahr El-Baqar" huko kituo cha Husseinieh katika mkoa wa  Sharkia Kwa kutumia mabomu matano (yaliyokuwa na uzito wa pauni 1,000) na makombora mawili, lililosababisha kifo cha takriban watoto 30, makumi ya watoto na wafanyikazi wa shule walijeruhiwa, na jengo la shule liliharibiwa kabisa.

Israel ilidai kwamba wapiganaji wake walikuwa na malengo ya kijeshi, na kwamba Shule ya Bahr El-Baqar ilikuwa ngome ya kijeshi iliyofichwa, na kuwepo kwa watoto katika shule hiyo ni kujificha tu.” Misri ililaani uhalifu huo na kupeleka barua rasmi kwa Umoja wa Mataifa iliomba  mkutano wa dharura wa nchi wanachama.Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri alifanya mkutano uliopanuliwa wa mabalozi wa nchi hizo nchini Misri, Uhalifu huo ulizusha kulaaniwa kwa maoni ya umma wa Dunia, na ulielezwa kuwa hauna maana yoyote ya Utu.Umoja wa Sovieti ulilaani uhalifu huo. , ukisema, "Israeli ilipotaka kuchagua haki ya kujibu, haikupigana na jeshi, bali ilienda kulipiza kisasi kwa watoto wa shule ya "Bahr El-Baqar", ulielezea kama "jibu dhaifu".

Sinema ya Misri imeelezea mauaji hayo kupitia kazi nyingi za sanaa, haswa filamu ya "Umri ni punde" mnamo 1978, filamu ya "Visa vya Mgeni" mnamo 1992. Mshairi Salah Jaheen pia alielezea uhalifu huo katika shairi lenye kichwa "Somo. Limekwisha” ambapo amesema:-

Unaonaje doa nyekundu?

Ewe dhamiri ya Dunia, kipenzi changu

Hiyo ni ya msichana mweusi mmisri....

Alikuwa mwanafunzi bora zaidi...