Kumbukumbu ya Msibu mkuu ...jeraha  kubwa la Palestina na Utaifa wa Abd El Nasser

Kumbukumbu ya Msibu mkuu ...jeraha  kubwa la Palestina na Utaifa wa Abd El Nasser
Kumbukumbu ya Msibu mkuu ...jeraha  kubwa la Palestina na Utaifa wa Abd El Nasser
Kumbukumbu ya Msibu mkuu ...jeraha  kubwa la Palestina na Utaifa wa Abd El Nasser
Kumbukumbu ya Msibu mkuu ...jeraha  kubwa la Palestina na Utaifa wa Abd El Nasser
Kumbukumbu ya Msibu mkuu ...jeraha  kubwa la Palestina na Utaifa wa Abd El Nasser

Mnamo Novemba 2, 1917, Azimio la Belfour lilitangazwa ambapo Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Arthur Balfour aliipeleka ardhi ya Palestina kwa Wayahudi kuunda nchi ya kitaifa kwao, nayo ni ahadi ya  utoaji wa" asiye na chochote kwa asiyestahili ", na ahadi hiyo ya kusikitisha ilikuwa mwanzo wa uhamishaji wa Wayahudi kutoka sehemu zote za Dunia huko Palestina, kwa msaada wa Mamlaka ya kiingereza. Mnamo Novemba 1947, uamuzi wa Mamlaka ya Mataifa kwa kugawa Palestina ulitolewa, na uamuzi huo ulitoa sehemu ya Palestina ya Kiarabu kama ardhi inayowakilisha nchi ya kitaifa kwa Wayahudi kwa kutimiza Azimio la Belfour ya kiingereza. May 14, 1948 Waingereza waliamua kumaliza Mamlaka yao kwa Palestina, na siku hiyo hiyo, Rais wa Shirika la Zayuni, David Ben Gurion, alitangaza "Malazi ya nchi ya Israeli", na  Wapalestina walitangaza May 15 siku ya msiba wao mkuu.

Janga la Wapalestina lilianza kwa kuhamishwa kwa idadi kubwa ya Wapalestina na kuziharibu nyumba zao, kufukuzwa kwa Wapalestina zaidi ya 750,000 kutoka katika ardhi zao na kuwafanyike kuwa wakimbizi, na kusababisha mauaji ambapo mamia ya Wapalestina waliuawa, kuchomwa kwa vijiji vyao na uharibifu wa vijiji zaidi ya 500 na kuwepo Wayahudi na mahali pao, msiba huo pia ulishughulika na kuondoa utambulisho wa Palestina, kubadilisha majina ya jiografia ya maeneo ya Palestina kuwa kiyahudi , na kujaribu kufuta utambulisho wa kiarabu kwa nchi.

Harakati za kitaifa katika Palestina na maeneo mengine ya Dunia ya Kiarabu zilianza kupinga Uchokozi huo, na Mfalme Farouk alitoa amri yake ya kuanza vita,  pia Viongozi wa Kiarabu walihimiza majeshi yao kuingia vita, na nchi za Kiarabu hazikuwa tayari kupigana vita hivi.

 Jeshi la kimisri lilishiriki katika vita hivi kwa mtindo wa jadi wa mapigano dhidi ya vikosi vya kigaidi vya Wazayuni vilivyoundwa kwa njia ya vita vya waasi ambavyo Uingereza ilivisaidia kwa silaha na vifaa vya hivi karibuni wakati ambapo ilikataa kusaidia jeshi la kimisri kwa silaha na risasi.Wakati wa vita, watu wa jeshi waligundua uhaini, na ikawa wazi kuwa silaha zilizopokelewa na jeshi zilikuwa zenye makosa na siyo vizuri, na Maafisa Huru, wakiongozwa na kiongozi Gamal Abd El Nasser, walirudi kutoka vita vya Palestina 1949, wakipitia matukio ya Vita vya Al-Falugaa, na roho zao zilikuwa zinajaa moto ya mapinduzi kurekebisha hali zile.

Kwa hiyo, inaweza  kukumbuka kwamba Mapinduzi ya milele ya July 23 yalitoka kutoka kwa tumbo ya matokeo ya  suala la Palestina, pamoja na sababu kadhaa maalum zinazohusu Misri, lililoonyesha mtazamo wa kitaifa wa kiarabu kwa mapinduzi , malengo yake na sera mnamo miaka ya utawala wa Abd El Nasser, aliyeshikilia suala la Palestina juu ya mabega yake, na aliona kuwa ni Suala la ulimwengu wa Kiarabu sio suala la Wapalestina peke yao, na alilizingatia lengo kuu katikati ya malengo yake ya kitaifa, na usalama wa Palestina unahusishwa na usalama wa Misri. Hii ilimfanya kuwa katika mapigano ya moja kwa moja sio tu na Mamlaka ya kizayuni, bali pia na Magharibi yenye wazo la Ukoloni.

Abd El Nasser amehusisha nguvu na uwezo wa  kifedha na kijeshi wa Misri kwa kupambana na Muungano wa  kikoloni. Na  Abd El Nasser hakuzembea kutoa msaada kwa suala la Palestina, bali alichukua aina nyingine zaidi ya  kutoa fedha  kwa Jamaa za Palestina na kuwapatia silaha, wakati ambapo aliunga mkono upinzani wa kipalestina na alichangia uanzishaji wa Taasisi ya Ukombozi wa Palestina, kama Mamlaka inayoonyesha Utashi wa Watu wa Palestina, na inachukua jukumu la kuhangaika mpaka kurejesha haki zao, pia alisimamia utiaji saini wa "Mkataba wa Kairo" kati ya Taasisi ya Ukombozi ya Palestina na serikali ya Lebanon mnamo Novemba 1969 ili kuhifadhi mapinduzi ya Palestina na mwendelezo wa mapambano yake.

Abd El Nasser aliendelea kuunga mkono mapinduzi ya Palestina kwa juhudi zake zote hadi mwisho wa siku zake na kuaga Dunia kwake mnamo Septemba,28 1970. Na Mamlaka ya Zayuni , kwa miongo kadhaa ipitayo hadi leo hata, inajaribu kuondoa kitambulisho cha Palestina, kumaliza suala lake, na kuchukua haki za wamiliki wake.