Mapinduzi ya Julai 23 na athari zake kwa harakati za kijamii

Imetafsiriwa na/ Abdelrahman Muhammad
Imehaririwa na/ Fatma El-Sayed
Mapinduzi ya Julai 1952, yaliyoongozwa na kiongozi Gamal Abdel Nasser, yalijaribu kufanya elimu yenye nguvu zaidi ya kijamii ambayo kwa upande wake ingeathiri maendeleo ya jamii kutoka chini ya piramidi ya kijamii.
Kwa hiyo, twapata katika miaka kumi ya kwanza: 1952-1962 ya umri wa harakati za jeshi, ambayo itabadilishwa kuwa mapinduzi ya kijamii, ambapo mapinduzi yalitumika katika elimu (kama nguzo ya msingi wa mradi wa kitaifa wa ufufuo) mara mbili ya kile kilichotumika katika miaka sabini iliyopita tangu kushindwa kwa vibaya na Misri ilipokuwa chini ya utawala wa ukoloni na wafuasi wake wa familia ya muuzaji wa tumbaku (1882 - 1952).
Inasemekana kuwa takwimu zaonesha kuwa paundi milioni 200 zilitumika tangu 1882 hadi 1952, yaani miaka 70.
Kwa upande mwingine, Mapinduzi ya Julai yalitumia pauni milioni 400 tangu 1952 hadi 1962 na miaka 10.
Takwimu hizo zazungumza kwa maneno ya kufikirika, bila kujali matukio makubwa na serikali ya Misri iliyokumbana nayo katika miaka hiyo;
1- Utaifaishaji wa Mfereji wa Suez na uchokozi wa tatu
2- Umoja na Syria kisha kujitenga
3. Kusaidia mapinduzi ya ukombozi kwenye Ulimwengu wa Tatu
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy