Kituo cha kitaifa kwa Tafiti za jamii na jinai  

Kituo cha kitaifa kwa Tafiti za jamii na jinai  

Kituo hicho kilianzishwa wakati wa enzi ya Rais Gamal Abdel Nasser kama taasisi ya uchunguzi wa jinai kwa sheria Na. 632 mnamo mwaka wa 1955 kwa kuizingatia taasisi huru yenye ubinafai wa kufikiria, wakati huo, taasisi ilihusika na utafiti wa masuala ya uhalifu na adhabu, ikiwa ni pamoja na sababu za uhalifu na kuzizuia, elimu, mazoezi na maandalizi katika nyanja za kinadharia na kiutendaji katika uwanja huu, na kuweka misingi muhimu ya kisayansi kuweka sera inayohusiana na uhalifu na adhabu.

 

Uhalifu ulipokuwa tukio la kijamii ambalo hakuna jamii isiyo na, na sio tu kwa kikundi fulani au mazingira maalum ya kijamii, ni jambo ambalo linaathiri watu wa jamii kwa ujumla, ilikuwa lazima kuichunguza kisayansi kupitia njia mbalimbali maalumu kama vile: sosholojia, saikolojia, kibaolojia, na nyingine.

 

Taasisi ilitengenezwa tena na iliitwa Kituo Cha kitaifa kwa Tafiti za jamii na jinai na uamuzi wa Rais wa Jamhuri kwa sheria Na. 221 kwa mwaka wa 1959 na ubinafai wake wa kufikiria ulithibitishwa na uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya wenye Na. 202 kwa mwaka wa 1969.

 

Nembo ya kituo (umbo la sanamu hubeba mizani) 

 

Huonesha sayansi na kile kinachohakikishwa kama uadilifu, lengo kuu la kituo hicho ni Elimu , lakini haki ni kufikia uwiano kati ya kile cha kisayansi na kibinadamu na kile cha kisheria na kijinai, hivyo kufikia haki inatoa madhumuni yake na inasaidia lengo lake.

 

Malengo ya kituo

 

Kituo hicho kinalenga kukuza Tafiti za kisayansi zinazoshughulika na masuala ya kijamii yanayohusiana na sehemu nyenginezo za Jamii ya Misri na matatizo yanayoikabili, na hivyo kwa lengo la kuweka misingi iliyohitajiwa kwa sera za busara za kijamii na kuchangia katika mchakato wa kutengeneza sera hizi kwa msingi sahihi wa kisayansi.

 

Na hivyo ni kupitia:

 

• Kufanya Tafiti na uchunguzi wa kisayansi wa porini na wa kimatumizi wa kiutendaji  na kuzosimamia.

• Kuandaa programu za mazoezi na elimu ya kuendeleza uwezo wa watafiti na makada wa ubora katika mashirika na taasisi katika nyanja mbalimbali zinazohusiana na shughuli za kituo hicho. 

• Kunpeleka tume za kisayansi na kiutendaji kujenga uwezo wa watafiti na kuongezeka kwa kiwango cha mfumo wa utafiti wa kisayansi.

• Kufanyika kwa mikutano, semina, vikao vya majadiliano, warsha za kazi na maonano ya kisayansi kutoa maoni ya kisayansi na kubadilishana uzoefu.

• Kuchapisha Tafiti na data za kisayansi na kubadilishana nao na taasisi nyingine za kisayansi. 

• Kuimarisha mahusiano ya kisayansi na vyuo vikuu, vituo vya utafiti na taasisi za kisayansi ndani na nje ya Misri kupitia kubadilishana kwa ziara za kisayansi na ushirikiano wa utafiti wa pamoja.

• Kutoa maoni kuhusu mswada wa sheria kuhusu masuala ya kijamii.

Kituo hicho kinajitahidi kukuza Tafiti za kisayansi  zinazoshughulika na masuala ya kijamii yanayohusiana na sehemu zote za jamii na matatizo yanayopata Jamii ya Misri, ili kuweka misingi ya sera za busara za kijamii na kuchangia katika mchakato wa kutengeneza sera hizi kwa msingi thabiti wa kisayansi.

 

Sehemu za kituo:

 

Kituo hiki kinagawanywa katika sehemu nne ambazo ni pamoja na vitengo vingi, navyo ni:

 

Kwanza: kitengo cha Tafiti za jamii na makundi ya kijamii kinajumuisha:

 

• Tafiti za jamii za mijini na miji mpya. 

• Tafiti za jamii za vijijini na jangwa. 

• Tafiti za wakaaji na makundi ya kijamii. 

Pili: kitengo cha Tafiti za taasisi na nguvu za maendeleo ya kijamii kinajumuisha:

 

• Tafiti za mawasiliano ya umma na utamaduni.

• Tafiti na upimaji wa maoni ya umma.

• Tafiti za elimu na wafanyakazi.

Tatu: Kitengo cha Tafiti za kemikali na biolojia kinajumuisha:

 

• Uchunguzi wa kugundua uhalifu. 

• Tafiti za madawa ya kulevya. 

• Tafiti za Mazingira. 

Nne: Kitengo cha Tafiti za uhalifu na sera ya jinai kinajumuisha:

 

• Uchunguzi wa uhalifu.

• Tafiti za mawasiliano ya Jinai.

  

 

Shughuli za kituo:

 

Kwanza: shughuli ya utafiti

 

Kulingana na kujali kikweli kwa kituo hicho katika masuala na matatizo ya jamii, na katika kukabiliana na maendeleo ya kimataifa ambayo kuwa na athari juu ya idadi ya masuala ya ndani, shughuli za kituo cha utafiti zinatofautiana kwenye nyanja mbalimbali zinazolenga kukuza njia ya maendeleo.

 

Agenda ya utafiti inajumuisha yafuatayo:

 

• Tafiti na upimaji wa maoni ya umma.

• Tafiti za mawasiliano ya umma na utamaduni.

• Tafiti za watoto.

• Tafiti za vijana.

• Tafiti za wazee.

• Tafiti za wafanyakazi.

• Tafiti za elimu.

• Tafiti za maendeleo ya mijini na vijijini.

• Tafiti za jumuiya za jangwa na miji mipya.

• Tafiti za jamii ya kiraia.

• Tafiti za uhalifu na matibabu ya jinai.

• Tafiti za uhamiaji.

• Uchunguzi wa kugundua uhalifu.

• Tafiti za madawa ya kulevya.

• Tafiti za mazingira.

• Mipango na miradi mikubwa ya utafiti.

• Ripoti ya kijamii ya Misri.

• Elimu, maendeleo na haki ya kijamii.

• Tafiti za wanawake.

• Mpango endelevu kwa madawa ya kulevya.

• Tafiti za maendeleo ya makazi duni katika Jamii ya Misri.

• Uchunguzi wa umasikini.

• Tafiti na uchunguzi wa vurugu katika Jamii ya Misri.

• Uadilifu wa jinai na haki za binadamu.

• Mpango wa Hali za kibinafsi.

• Uchafuzi wa mazingira.

 

Pili: kichunguzi cha kijamii

Kilianzishwa kwa lengo la kuangaza nuru kwenye matukio ya kijamii yaliyolengwa katika Jamii ya Misri na hivyo kwa kutoa maelezo sahihi ya kisayansi ya kiajabu, pia kuwa na pendekezo la mkakati kwa kupambana na kufanya utafiti wa uingizaji wa matatizo sugu ya kijamii ili kupata matokeo na mapendekezo ya kuwasilishwa kwa mtendaji wa uamuzi kuchukua hatua na taratibu muhimu zilizohitajiwa za kiutendaji.

 

Tatu: shughuli ya mazoezi

 

Pamoja na shughuli za utafiti, kituo hicho hupanga idadi ya kozi za mazoezi na hivyo kutayarisha  binadamu kinachowakilisha maendeleo na lengo lake.

 

Miongoni mwa kozi muhimu zaidi zilizoandaliwa na kituo hicho ni:

 

• Programu ya mazoezi kwa maingiliano na mbinu za kisasa za kuchunguza na kupambana na uhalifu.

• Programu ya mazoezi katika hojaji ya kielektroniki ya mbali.

• Mpango wa mazoezi katika umbali kijamii na idadi ya watu kwa mipango miji.

• Mpango wa mazoezi kuwezesha viongozi wanawake.

• Kozi ya mazoezi katika takwimu na matumizi yake katika Sayansi za kijamii.

• Mpango wa mazoezi kwa watafiti wapya.

• Programu ya mazoezi kwa waandishi wa habari kwenye mamlaka kuu ya habari.

• Kozi ya moja kwa moja kwa waendesha mashitaka.

• Vipindi maalumu vya mazoezi kwa ajili ya makada wa ubora katika uwanja wa madawa ya kulevya.

• Kozi maalumu kwa waendesha mashitaka.

• Kozi ya mazoezi kwa wanaohusika na uchunguzi wa maoni ya umma.

Kituo pia huendeleza kozi nyingi kulingana na mageuzi ya kiuchumi na kijamii nchini Misri, pamoja na kozi nyingi zilizoombwa na mamlaka.

 

Nne: uhariri na uchapishaji wa kisayansi

 

Kulingana na historia yake ndefu, kituo hicho huchapisha mamia ya ripoti za tafiti, kazi za mikutano, semina, vikao vya majadiliano na mengine. Mbali na hayo yote, kituo hicho huchapisha majarida ya kisayansi tatu, ikiwa ni pamoja na: majarida matatu ya kisayansi, majarida mawili theluthi moja mwaka (kila baada ya miezi minne), nayo ni: 

• Gazeti la kitaifa la jinai: toleo lake la kwanza lilichapishwa mnamo Machi, 1958.

 

• Gazeti la kitaifa la kijamii toleo lake la kwanza lilichapishwa mnamo Mei, 1964.

 

Pamoja na uwepo wa gazeti la mara mbili kila mwaka, nalo ni:

 

• Gazeti la kitaifa la utafiti wa kutumia madawa ya kulevya na: toleo lake la kwanza lilichapishwa mnamo Januari2004.

 

• Mfululizo wa makala wa kielektroniki wa kila mwezi “kwa kalamu ya mtafiti”, toleo lake la sifuri lilichapishwa mnamo Mwezi Mei, 2021, hujadili mada muhimu zaidi na matatizo ya kijamii yaliyopo uwanjani.

 

Mkutano huo hushiriki kila Mwaka katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu jijini Kairo.

 

Tano: semina na makongamano

 

Kituo hicho kinafanya mkutano wa kila mwaka kujadili masuala ya kijamii na ya jinai kwa Jamii ya Misri, ambapo viongozi kadhaa na maafisa wakuu katika nchi hushiriki kwa kuongoza vikao vya au kwa kuhudhuria na kujadili, na mikutano hii inawakilisha nafasi ya kupunguza pengo kati ya utafiti wa kisayansi na mchakato wa kufanya maamuzi.

 

Kituo pia huandaa semina nyingi za kisayansi na vipindi vya majadiliano, ikiwa kwa kuweka mbele au kujadili baadhi ya vichwa vinavyohusiana na suala fulani la kijamii katika maandalizi kwa ajili ya kuvisoma kwa kina au kujadili matokeo ya utafiti uliofanywa ili kuyatathmini na kuyaajiri katika kufanya sera za umma, pamoja na uwepo wa kituo katika mikutano na warsha ya kitaifa na ya kikanda.

 

Sita: washirika

 

Kituo hicho hubadilishana ziara za kisayansi na vituo vya utafiti na taasisi za kisayansi ndani na nje ya Misri. Pia kinashirikiana katika kufanya miradi ya utafiti na kubadilishana uzoefu na taasisi zifuatazo:

 

• Taasisi ya Urais

• Vyuo vikuu na vituo vya utafiti kulingana na mahitaji ya utafiti.

• Wizara husika kama vile: Mshikamano wa kijamii, Haki, Mambo ya Ndani, Ulinzi, Mambo ya Nje, Afya na Wakazi, Upangaji na Maendeleo ya Kiuchumi, Elimu, Elimu ya juu na Utafiti wa kisayansi, Utamaduni, Al-Awkaf, Maendeleo ya mitaa, Wafanyakazi, Uhamasishaji na Mambo ya Misri nje ya nchi, Umwagiliaji, Vijana na Michezo, Fedha, Ugavi, na Baraza kuu la kupanga vyombo vya habari.

• Ushehe wa Al-Azhar Al-Sharif.

• Kanisa.

• Nyumba ya fatwa.

• Baraza la Taifa la Ulinzi.

• Shirika la utawala wa udhibiti.

• Chuo Cha Polisi.

• Chuo cha utafiti wa kisayansi.

• Mamlaka kuu ya habari.

• Baraza la kitaifa la udhibiti na matibabu ya madawa ya kulevya na matumizi yake.

• Mamlaka ya kuendeleza miradi ya kati, ndogo na ndogo mno.

• Baraza la kitaifa la Haki za binadamu.

• Baraza la kitaifa la wakazi.

• Baraza la kitaifa la wanawake.

• Shirika la kati kwa uhamasishaji wa umma na takwimu.

• Kituo cha habari na kuchukua maamuzi -Baraza la mawaziri.

• Mikoa na mashirika yanayohusika na masuala ya kijamii.

• Mashirika ya kikanda na kimataifa kama vile: Jumuiya ya nchi za kiarabu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Shirika la kazi Duniani, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa ya kulevya na uhalifu na ESCWA.

Kituo hicho kinazingatiwa mwanachama mshiriki katika kamati nyingi za kitaifa na taasisi za kufanya maamuzi.

 

Kituo hicho pia kina maktaba yenye vitabu kwa karibu elfu ishirini vya kiarabu na vya kigeni pamoja na majarida na ensaiklopidia,  vinavyojumuisha matawi yote ya Sayansi ya Jamii, na baadhi ya matawi ya Sayansi ya Asili. 

 

Vyanzo 

Tovuti ya Kituo Cha kitaifa cha Tafiti wa jamii na jinai.