Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana azindua nchini Libya, tawi la kitaifa la baraza huru la Ushauri wa Vijana la Mkataba wa Biashara Huria Barani Afrika 

Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana azindua nchini Libya, tawi la kitaifa la baraza huru la Ushauri wa Vijana la Mkataba wa Biashara Huria Barani Afrika 

Mwanadiplomasia kijana wa Libya “Sanad Marzouk El-Fakri", Mwanadiplomasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Wizara ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Libya, mkuu wa mradi (kuzingatia Afrika na kuunganisha mifumo ya mawasiliano ya vijana), Mjumbe wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, na Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Jumatano jioni 4 Januari hii, amezindua rasmi tawi la kitaifa la Baraza la Ushauri la Vijana la Mkataba wa Biashara Huria ya Afrika katika Mji Mkuu wa Libya, Tripoli, ambapo hii ilikuja kwa mahudhurio ya wawakilishi wa Urais wa Baraza la Mawaziri la Libya, na Dkt. "Fathallah Al-Zani" Waziri wa Vijana, mawakala wa wizara za Serikali ya Umoja wa kitaifa, mwenyekiti wa baraza la kitaifa la Libya la makubaliano na mawasiliano, na kundi la viongozi wa vijana. 

Mwanzoni mwa hotuba yake, Al-Fakri aliwasilisha namna ya kazi ya baraza, ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa kazi na malengo yake, na mpango wa kazi wa ofisi ya Libya mnamo Mwaka ,2023 akisema kuwa shughuli za tawi la kitaifa la baraza itazinduliwa kwa msaada na Udhamini wa mpango wa "Bader" uliozinduliwa na "Abdul Hamid Al-Dbeibeh", Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa kitaifa na Mheshimiwa Waziri wa vijana, ambapo hii inakuja ndani ya mpango wa kitaifa wa kusaidia mipango na miradi ya vijana nchini Libya.

Kwa upande wake, "Hassan Ghazaly", Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana na Mratibu mkuu wa Tawi la Taifa la Misri la Baraza la Ushauri la Vijana la Mkataba wa Biashara Huria ya Afrika, alisema kuwa yuko karibu kuzindua tawi la baraza nchini Misri kupitia kipindi kijacho, akiashiria shughuli, warsha na semina ambazo alizizindua mnamo Mwaka 2022 kuongeza ufahamu wa suala la biashara huria ya Afrika, ikiwa ni pamoja na warsha kadhaa ndani ya shughuli za mpango wa Afromedia, na semina kadhaa ndani ya mfumo wa mpango wa kitaifa wa kuandaa makada wa wanafunzi katika Masuala ya Afrika, ambazo zilikuja chini ya uangalifu wa Taasisi ya Afrika ya Maendeleo na Kujenga Uwezo katika matayarisho ya kuzindua Baraza la Ushauri "ICYACA" nchini Misri. 

"Ghazaly" alihitimisha, akielezea kuwa Harakati ya Nasser kwa Vijana ilizinduliwa mnamo Julai 2019;  iwe jukwaa la kimataifa la vijana linalojumuisha viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi katika Ulimwengu, ili kuwaunganisha na Watoa Maamuzi na wataalam ndani ya nchi, kikanda na kimataifa, katika maandalizi ya kuanzisha mipango iliyozinduliwa na Umoja wa Mataifa, Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, Shirika la Mshikamano wa Watu wa Afrika-Asia na Ajenda ya Umoja wa Afrika 2063, haswa katika mambo yanayohusiana na vijana, wanawake, hali ya hewa, elimu, amani na usalama, utawala na ujasiriamali, katikati yake ni Mkataba wa Biashara Huria ya Bara la Afrika.