Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi aanzisha tawi la kitaifa huko Congo-Brazzaville
Imetafsiriwa na: Nour El-Din Mahmoud
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Bw. Jean-Christ Bondungu Bukaka, Mhitimu wa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, alianzisha tawi la kitaifa huko Congo-Brazzaville, ambapo alianza kushiriki uzoefu wake katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi na Balozi wa Kongo nchini Misri, ambapo Mheshimiwa wake alihudhuria sherehe ya kufunga ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, na pia alikutana na Balozi wa Misri nchini Congo-Brazzaville na alialikwa kuhudhuria sherehe za Ubalozi wa Misri kwenye maadhimisho ya mapinduzi ya Julai 23, 2019, kwa kuhudhuria ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Kongo na Balozi wa Misri na kuwasilisha ripoti ya usomi.
Pia alikutana na Waziri wa Mawasiliano na Habari, na Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kongo, Bw. Thierry Lizin Mongala. Walizungumza juu ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi ambayo ni fursa inayofungua milango kwa vijana wa Congo, na pia walizungumzia umuhimu wa kufikisha picha nzuri ya nchi nje ya nchi.
Pia alikutana na Rais wa Burkina Faso, Roch Marc, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi cha Congo na Rais wa Seneti ya Congo.