Twasherehekea siku hii ya milele katika historia; alfajiri ya ukombozi wa Kiarabu

Imetafsiriwa na: Esraa Abdelazeem Ahmed
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Enyi Wananchi:
Katika siku hizi za milele katika historia ya Waarabu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa mioyo yetu yote kwa sababu zama za utawala wa kigeni zimeisha bila kubatilishwa; enzi ya ukoloni, enzi ya udhibiti na enzi ya wavamizi imeisha kutokana na uamuzi wa Waarabu katika Jamhuri ya Kiarabu.
Leo, tunaposherehekea kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiarabu, kila mmoja wetu anahisi kwamba jamhuri hii mpya imeanzishwa inayowakilisha mapenzi yetu; mapenzi ya kila mmoja wenu, iwe kaskazini mwa Syria au kusini mwa Misri, sio mapenzi ya mkoloni, wala mapenzi ya mvamizi, wala mapenzi ya mtu wa nje, wala mapenzi ya wale wanaotaka kutuweka ndani ya maeneo ya ushawishi. Mapenzi ya watu wa kweli wa Kiarabu. Leo, ndugu zangu, kila mtu katika ulimwengu wa Kiarabu na katika taifa la Kiarabu ana haki ya kujisikia fahari ya kweli, kwa sababu kabla ya hapo, mnamo mwaka 17, waligawanya ulimwengu wa Kiarabu. Waliigawanya kwa penseli kwenye ramani katika nchi na mataifa madogo ili yawe ndani ya maeneo ya ushawishi. Walitulazimisha hali hiyo na kukubaliana na Wayahudi katika mwaka wa 17 kuwapa Palestina. Leo sisi ndio tunaoamua, hakuna mgeni anayeamua. Hakuna mvamizi anayeamua.
Leo ndugu zangu... Leo ndugu zangu... Ni mapenzi yetu - watu wa Kiarabu - ambayo ina uhuru, ina nguvu, ndio inayoamua, ndiye anayeamua kuanzishwa kwa Jamhuri ya Kiarabu.
Leo, ndugu zangu, tunasherehekea siku hii ya milele katika historia, alfajiri ya ukombozi wa Waarabu, alfajiri ya kuondoa udhibiti wa kigeni, na tunasherehekea siku hii tukiangalia majaribio ya zamani na ya kigeni ya kutudhibiti, na kwa maneno waliyokuwa wakisema: kwamba kuna utupu ambao wanataka kujaza katika eneo hili, na kwamba eneo hili lazima lijumuishwe ndani ya maeneo ya ushawishi.
Leo, wakati tunasherehekea, kila mmoja wetu anahisi ndani kabisa kwamba mapenzi yake yameshinda, kwamba imani yake imeshinda, kwamba malengo yake yameshinda, kwamba utaifa wa Kiarabu ambao ulikuwa ndoto kwa kila mmoja wetu, utaifa wa Kiarabu ambao tulikuwa tukiuita katika hotuba, utaifa wa Kiarabu waliokuwa wakisema mashairi kwa miaka mingi. Kwa miongo kadhaa, tunaposherehekea, tunahisi kwamba utaifa huu wa Kiarabu unaanza kubadilika. Leo, wakati tunaangalia kuzaliwa kwa Jamhuri ya Kiarabu ambayo iliibuka kutoka kwa mapenzi yako na dhamiri yako, tunahisi kuwa huu ndio mwanzo
Ndugu zangu, huu ni mwanzo wa ukombozi, mwanzo wa kuondoa utawala wa kigeni na kuondokana na ukoloni. Huu ndio mwisho wa udhaifu na mwanzo wa madaraka. Huu ndio mwisho wa kutochukua hatua, mwisho wa mawakala wanaofanya kazi na wageni kuuza nchi yao, na mwanzo wa utawala wa uhuru; utawala wa watu... watu wa taifa. watu wa kweli.
Leo, ndugu zangu, ninaposema maneno haya, ninazungumzia taifa la Kiarabu kama taifa la Kiarabu linalosimama peke yake, ambalo kila mmoja anahisi mwenzake, kila mmoja anaunga mkono mwenzake, kila mmoja kwa mshikamano na mwingine, kila mmoja ndani yake - katika nchi yoyote na katika nchi yoyote ya Kiarabu waliyotunga baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia - anahisi kwamba nchi yake inajumuisha nchi zote za Kiarabu.
Leo ndugu zangu tunaposherehekea kuzaliwa kwa jamhuri hii tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie, na tunamuomba Mwenyezi Mungu atusaidie kwa uwezo wake, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aende kwa dhamira na imani, na tunamuomba Mwenyezi atutie nguvu ili tuweze kufikia ndoto tulizokuwa tunaziita, na ili tuweze kuanzisha katika eneo hili la uhuru wa kweli wa dunia, na kwamba hakuna nafasi ya maeneo ya ushawishi, na kwamba tujaze utupu ambao wanauzungumzia wenyewe, na kwamba tunaweza kuwa msaada kwa Waarabu wote katika kila nchi kutoka nchi yao, na katika kila nchi yao.
Leo, ndugu zangu, tunaposherehekea kuzaliwa kwa Jamhuri ya Kiarabu, ambayo iliibuka kutoka kwa mapenzi yetu, kutoka kwa dhamiri yetu, na ilikuwa matokeo ya uamuzi wetu, tunaelekea siku zijazo tukiamini kwamba tuko mwanzoni mwa njia; njia ya uhuru, njia ya kazi, njia ya umoja, na njia ya mshikamano. Mungu akupe mafanikio.
Amani na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu.
-------------------
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser kutoka Ikulu ya Rais katika umma wa Misri na Syria na miili ya kumpongeza kwa urais
Mnamo tarehe Februari 23, 1958.