Kwa namna gani twafadhili Ajenda ya Afrika 2063 ?

Kwa namna gani twafadhili Ajenda ya Afrika 2063 ?
Kwa namna gani twafadhili Ajenda ya Afrika 2063 ?

Dokta. Hala Elsaeid, Waziri wa Upangaji, Ufuatiliaji na Mageuzi ya Utawala, alikutana na vijana waafrika walioshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi unaotelewa na Wizara ya Vijana na Michezo, na alitoa mhadhara wa kutoa taarifa za jinsi tunavyofadhili malengo ya Ajenda ya kiafrika 2063.

Mwanzoni mwa mhadhara huo, Hala ElSaeid alisisitiza nia ya kudumu ya Misri kuuimarisha ushirikiano pamoja na jirani zake za nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali haswa wakati wa Urais wa kisasa wa Misri kwa Umoja wa Afrika kwa mwaka wa 2019, pia aliashiria uratibu wa Misri wa mkutano wa kiafrika wa kwanza kupambana na ufisadi, mjini Sharm Elsheikh kwa siku mbili, mnamo kipindi cha Juni 12 na 13 kwa kuwepo na Ufadhili  wa Rais wa Jamhuri na ushiriki mkubwa wa takriban nchi  51 za kiafrika, nchi 4  za kiarabu na zaidi ya maafisa 200 wa ngazi ya juu wa Afrika, vilevile Misri itakaribisha kombe la Mataifa ya Afrika la Soka la toleo la 32 mwanzoni mwa wiki ijayo, mwaka ambao litashuhudia, kwa mara ya kwanza katika tarehe ya Kombe la Mataifa ya Afrika, ushiriki wa timu 24  za kitaifa zikilinganishwa na timu  16 za kitaifa mwaka uliopita ambao Misri ilitoa kila uwezo inao pamoja na ushirikiano na uratibu wa Wizara na Taasisi zote  ili kupata mafanikio ya michuano hii na iwe ya kipekee, na hivyo aliweka wazi uandaaji wa Wizara wa Upangaji , Ufuatiliaji na Mageuzi ya Utawala kwa upande wa kupokea Misri kwa kikao cha 40 cha Shirika la kiafrika la usimamizi mkuu mnamo robo ya mwisho ya mwaka huu.

Hala alieleza kutilia umuhimu uratibu  kwa Misri kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, kutokana na jukumu lake muhimu kukiunda kizazi kipya cha  viongozi vijana wa kiafrika watakaochangia kuunda mawasiliano kati ya wananchi wa bara,  kufikia maendeleo na Mustakabali bora zaidi kwa nchi zetu za kiafrika.

Alisisitiza kwamba Afrika ilikuwa wa kwanza kuweka mkakati wa Maendeleo Endelevu, ambapo nchi za bara ziliweka Ajenda ya Afrika 2063 mnamo 2013, iliyoidhinishwa na Umoja wa Afrika Januari 2015 kama mkakati wa muda mrefu na wa kimpito kufanya kazi siku zijiazo, unaoweka msingi wa mageuzi jumuishi ya kiuchumi na kijamii ya Bara la Afrika mnamo miaka hamsini ijayo.

Alisema kuwa Ajenda ya Afrika 2063 iliwekwa kufanikisha juhudi na mipango mingi kufikia Ukuaji na Maendeleo Endelevu na miongoni mwake: mpango wa kazi wa Lagos, mkataba wa Abuja, Ushirikiano mpya kwa maendeleo ya Afrika(NEPAD), mpango wa Maendeleo ya Miundombinu Barani Afrika(PDIA)  na mipango na programu zingine zinazolenga kufikia Maendeleo Barani Afrika.

Katika mfumo wa uratibu wa mipango ya kitaifa na kuimarisha ushirikiano wa kikanda Barani kufikia Maendeleo Endelevu, Hala Elsaeid aliashiria kuendelea kwa matukio katika uwanja huo ukiwa na : kufanyika kwa Kongamano la kiafrika la  Maendeleo Endelevu la mwaka 2017 Addis Ababa, pia hivi karibuni Aprili iliyopita ilikuwa na Kongamano la kiafrika la Maendeleo Endelevu la mwaka 2019 lilifanyikwa mjini Marrakech, Ufalme ndugu wa Morocco.

Ama Kuhusu Ufadhili kama ni  changamoto muhimu zaidi inayokabili juhudi za kufikia Maendeleo Endelevu, ElSaid alisema kwamba mambo muhimu zaidi  yanayounganisha mipango na programu za kitaifa kufikia Maendeleo Endelevu ni kupatikana kwa Ufadhili na Rasiliamali zinazohitajika ikiwa katika mfumo wa kimataifa kupitia mpango wa Maendeleo Endelevu 2030 au mfumo wa kikanda na Barani kupitia Ajenda ya Afrika 2063, akiashiria kwamba Tafiti na taasisi za kimataifa zinathibitisha ongezeko la kuhitaji kwa Ufadhili kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu, akifafanua kwamba masomo ya kisasa ya benki ya maendeleo ya kiafrika yanaonyesha uhitaji wa ufadhili wa bara kutekeleza miradi muhimu ya Miundombinu kufikia maendeleo unakadiriwa kwa takriban dola bilioni 130 hadi 170 kila mwaka, na pia kuna ukosefu wa ufadhili kwa dola bilioni 68 hadi 108.

Alisisitiza kuwa kutopatikana kwa ufadhili wa kutosha kulisababisha upungufu wa matokeo yaliyofikiwa na mipango mingi ya kimaendeleo iliyofanywa na nchi za bara, kwa hivyo Ajenda ya Afrika 2063 ilipendekeza kuendeleza mfumo na taratibu za ufadhili za mipango ya kimaendeleo.

Na kuhusu juhudi za Misri kufikia Maendeleo Endelevu na ya kina, Waziri wa Upangaji alionesha kuwa Misri ilikuwa moja ya nchi za kwanza kuweka mpango wa kitaifa kufikia malengo ya kimataifa ya Maendeleo Endelevu kama mkakati wa Maendeleo Endelevu ya mtazamo wa Misri 2030 uliotolewa Februari 2016 ili kuunda mfumo mkuu uandaao programu za kufanya kazi miaka ijayo, ikitaka mtazamo huo uwe na uhusiano unaoendana na mabadiliko ya kitaifa na ya kimataifa ya kisiasa na kiuchumi, Wizara ya Upandaji, Ufuatiliaji na Mageuzi ya Utawala iliangalia umuhimu wa kustawisha mkakati huo, haswa kwa kuwepo kwa masuala na changamoto mpya katika jamii ya kimisri tangu 2016 ambazo ni muhimu kuziangaliwa na maelekezo ya usoni na ya kimkakati.

Alisisitiza kwamba Misri inawachukulia vijana kama msingi wa kisasa wa mchakato wa maendeleo na Mustakabali yake, hivyo inapanua utekelezaji wa programu za mafunzo, uundaji wa uwezo, kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuimarisha ujasiriamali na kuenea kwa wazo la kazi ya kujitegemea kati yao, pia kupanua katika uundaji wa uongozi wa kazi na kutekeleza miradi na programu nyingi zinazounga mkono uundaji huo, na miongoni mwao mradi wa Waanzilishi 2030, pia Misri inatilia umuhimu maalumu kuimarisha mchango wa mwanamke mmisri katika uwanja huo.

Pia alionesha juhudi, taratibu na Mageuzi muhimu zaidi zilizochukuliwa na Misri katika mfumo wa kutekeleza Mtazamo wa Misri 2030, mpango wa mageuzi ya kiuchumi na kijamii kama mageuzi ya mfumo wa kutunga sheria na wa kitaasisi kupitia kuweka idadi ya sheria, isitoshe uimarishaji wa mfumo wa kutunga sheria unaounga mkono Ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, kuandaa muundo muhimu ili kuvutia wawekezaji, kutaka maendeleo ya sekta ya miradi midogo na ya kati, kuunga mkono kuunganisha sekta ya umma na binafsi, kuhimiza Ujasiriamali, mafunzo ya kuandaa uwezo wa kibinadamu na hayo yote pamoja na kuendeleza na kudhibiti mfumo wa utawala wa nchi ambapo mpango wa kina wa mageuzi ya utawala unatekelezwa sambamba na maandalizi ya sasa kuhama Mji Mkuu Mpya wa Utawala, vilevile serikali ya kimisri inachukulia Mwelekezo wa ufanisi wa kubadilika kwa jamii ya kidijitali na kufikia ujumuisho wa kifedha kama moja ya nguzo za Maendeleo Endelevu na ya kina.

Aliendelea kusema kuwa kujaribu kudhibiti matumizi ya pesa ya umma kunaendana na juhudi zilizopita kwa kupitia uendelezaji wa mfumo wa mpango nchini Misri kwa ujumla kuongeza ufanisi wa matumizi ya Rasilimali fedha zilizopatikana ambapo kwa sasa, Misri inapanua kutekeleza usawazishaji wa programu na utendaji kama moja ya malengo makuu ya siasa ya fedha na ya kiuchumi ya nchi, na katika mfumo huo Misri iliunda mfumo wa mipango na ufuatiliaji wa kitaifa kama zana ya kisasa yenye ufanisi ya elektroniki ambayo ni ya kwanza ya aina hiyo kufuatilia na kutathmini utendaji wa mifumo yote ya nchi.

Hala alionyesha kwamba  matokeo muhimu yaliyofanyika kama tokeo la taratibu na Mageuzi yaliyochukuliwa na nchi miaka ya hivi karibuni ni:  uchumi wa kimisri ulifikia kiwango cha juu cha ukuaji cha mwaka tangu miaka kumi kwa 5.6% katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha huu 18/2019, ambapo kinapita viwango vya ukuaji katika masoko yanayoibuka na nchi zinazoendelea, ni pamoja na upungufu wa kiwango cha ukosefu wa ajira kikifikia 9.9% kikilinganishwa na 13.2% mwaka wa 13/2014, mbali na mtazamo wa matumaini wa mashirika ya kukadiria mikopo na Taasisi ya kimataifa ya uchumi wa kimisri.

Aliongeza kwamba, ikiendelea maelekezo ya usoni nchini, vipengele vya msingi vya mpango wa uwekezaji wa mwaka 19/2020 viliamuliwa ambavyo ni malengo makuu ya mpango huo kama kufikia ukuaji mkubwa wa uchumi ufikie 6%, kudhibiti viwango vya ongezeko la watu vifikie 2.3%  mwaka 2020, kutekeleza uwekezaji kikamilifu kwa thamani ya paundi ya Misri trilioni 1.17 kwa kiwango cha 26.5% cha ukuaji, kuongeza kiasi cha uwekezaji wa umma hadi Paundi bilioni 533,6 kwa kiwango cha 29% cha ukuaji, Kuongeza viwango vya uwekezaji kwa pato la taifa kwa ujumla katika mwaka wa 19/2020 hadi 18.3% vikilinganishwa na 17.3% vinavyotarajiwa mwaka huu 18/2019, na 16.7% vya halisi mwaka jana 17/2018, kupungua kiwango cha ukosefu wa ajira hadi 9.1% na kuendelea kwa utekelezaji wa mpango wa mageuzi ya muundo ili kuendeleza sekta zenye matumaini zaidi na thamani.

Inaonekana wazi kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi ni Udhamini wa kiafrika wa kwanza unaolenga viongozi vijana waafrika watekelezaji wenye Taalamu mbalimbali katika jamii zao, na inachukuliwa kama moja ya taratibu za vipengele wazi vya kuwezesha vya mageuzi ya kiafrika yaliyoandaliwa na Ajenda ya Afrika 2063.

Malengo ya Udhamini unawakilishwa kupitia kuhamisha jaribio la kimisri la kuimarisha na kujenga taasisi za kimataifa, uundaji wa kizazi kipya cha viongozi vijana waafrika vya mageuzi wenye mitazamo sambamba na maelekezo ya Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika wenye uwezo wa kifikia malengo ya Umoja wa kiafrika kupitia ukamilifu, pamoja na kukuza taarifa za viongozi vijana waafrika wanaoathiri zaidi  Barani kwa mafunzo na kuwaongezea ujuzi muhimu na maoni ya kimkakati, Udhamini huo uliwalenga viongozi vijana 100 wenye utekelezaji kutoka nchi za Umoja wa Afrika, na muda wake ni wiki mbili kuanzia Juni 8 hadi 22, 2019.