Biashara ya Misri na Kambi ya Mashariki Yapanuka kwa Upeo, na Hakuna Shaka kwamba Magharibi Yafanya Makosa kwa Kufungia Mali za Misri

Biashara ya Misri na Kambi ya Mashariki Yapanuka kwa Upeo, na Hakuna Shaka kwamba Magharibi Yafanya Makosa kwa Kufungia Mali za Misri

Imetafsiriwa na/ Dalia Hassan 
Imehaririwa na/ Mervat Sakr

Swali kutoka kwa mhoji: Je, Misri imevuka mipaka ambayo haiwezi kurudi nyuma katika Uhusiano wake na Urusi?

Rais Nasser: Hii sio haki; sera yetu ni huru, kwa hivyo ni nini maana ya kutoroka kutoka kwa udhibiti mmoja ili kuanguka katika udhibiti mwingine?! Hadi sasa, maamuzi yote juu ya siasa za Misri yamefanywa hapa katika ofisi hii, sio Moscow, sio Washington.

Biashara ya Misri na Kambi ya Mashariki imepanuka, na hakuna shaka kwamba Magharibi imefanya makosa katika kukomboa mali za Misri. Ninachukua tahadhari kubwa kukabiliana na mgomo wa biashara wa Magharibi juu ya Misri.

Inawezekana kuzuia kuzorota kwa Uhusiano wa Misri na nchi za Magharibi na kurejesha mambo katika hali ya kawaida, lakini hatua ya kwanza katika njia hii lazima iwe Upande wa Magharibi yenyewe. 

Naamini kwamba Magharibi imepuuza matarajio ya Mashariki ya Kiarabu na malengo yake ya kitaifa tangu kuanzishwa kwa Mkataba wa Baghdad, na ninaamini kwamba Waarabu wote hawakubali muungano wowote isipokuwa ni Waarabu tu, Uingereza imeotengwa hasa, kwa sababu ya chuki yao kali kwa utawala wa kikoloni, walioteseka sana hapo awali.

Rais Gamal Abdel Nasser alizungumza na Herald Tribune kuhusu Uhusiano wa Misri na Kambi ya Mashariki.

Mnamo tarehe Agosti 30, 1956


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy