Dira ya Misri 2030

Dira ya Misri 2030

Ni Ajenda ya kitaifa inayojumuisha mikakati ya kisekta kwa mashirika mbalimbali ya serikali nchini Misri, iliyozinduliwa mnamo Februari 2016, kwa kusimamia taasisi za serikali na jamii kupitia uimarishaji wa  uwazi, mageuzi ya kiutawala na msaada wa mifumo ya ufuatiliaji na tathmini, kuhakikisha amani na usalama wa Misri na kufikia maendeleo ya kina, kwani inalenga hasa kuboresha hali ya maisha ya raia wa Misri na kuboresha kiwango chake cha maisha katika nyanja mbalimbali za maisha kwa kusisitiza uimarishaji wa misingi ya haki, ushirikiano wa kijamii na ushiriki wa raia wote katika maisha ya kisiasa na kijamii, pamoja na kukuza uwekezaji wa watu na kujenga uwezo wao wa ubunifu kwa kuhamasisha kuongezeka kwa maarifa, ubunifu na utafiti wa kisayansi katika nyanja zote.

Dira ya Misri ya 2030 pia inaonesha mpango mkakati wa muda mrefu wa serikali ya Misri kufikia kanuni na malengo ya maendeleo endelevu katika nyanja zote, kwa kuzingatia kanuni za "Maendeleo Endelevu" na "maendeleo ya kikanda yenye usawa" na kama maono kamili na thabiti, Misri imehusika katika ajenda hiyo wadau wote kutoka kwa washirika wa maendeleo, kwa lengo la kuendana na mabadiliko katika muktadha wa ndani, kikanda na kimataifa, na kuwa maoni yenye msukumo unaoelezea jinsi mchango wa Misri utasaidia ajenda ya Umoja wa Mataifa, na jinsi itakavyosaidia muktadha wa kimataifa. Masuala yote yanaingiliana kwa mtazamo wa vipimo vitatu vya msingi vya maendeleo endelevu: mazingira, kiuchumi na kijamii.  

Misri ina nia ya kukuza maarifa, uvumbuzi na utafiti wa kisayansi kama nguzo za msingi za maendeleo, hii ilikuja katika lengo la nne la Dira ya Misri ya 2030,  inayosisitiza umuhimu wa kuwekeza kwa watu, kujenga uwezo wao wa ubunifu, kuchochea uvumbuzi, kueneza utamaduni wake, kusaidia utafiti wa kisayansi na kuiunganisha na elimu na maendeleo, ndio Udhamini wa Uongozi wa Nasser inayotaka kimsingi kuifanikisha.

Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana na Udhamini pia zinakuja kama moja ya taratibu za kufikia lengo la nane la Dira ya Misri ya 2030, ambayo ni kufikia na kuimarisha nafasi ya uongozi wa Misri, kwani ajenda ya kitaifa ilikuwa na nia ya kuunganisha malengo yake ya maendeleo na malengo ya kimataifa kwa upande mmoja, na kwa ajenda ya kikanda, hasa Ajenda ya Afrika 2063 kwa upande mwingine, baada ya mafanikio ya Misri katika kurejesha utulivu wake na kuboresha uhusiano wake na idara zake za kigeni, lengo la kuimarisha nafasi na uongozi wa Misri katika ngazi za kikanda na kimataifa limekuwa muhimu kuendeleza maendeleo ya kina, yanayopatikana kupitia mifumo mingi. Muhimu zaidi ni kusaidia uimarishaji wa ushirikiano kikanda na kimataifa, hivyo kauli mbiu ya Udhamini "Ushirikiano wa Kusini-Kusini" ilikuja kama moja ya taratibu.