Harakati ya kutofungamana na Upande wowote

Harakati ya kutofungamana na upande wowote umeanzishwa na nchi zilizohudhuria mkutano wa” Bandong 1995, Harakati hiyo imekuwa kama matokeo ya vita kati ya pande hizo mbili ( upande wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote).
Harakati isiyofungamana kwa upande wowote (NAM-Non-Aligned Movement) ilianzishwa mnamo 1955, baada ya Kongamano la Bandung, ilikuwa na nguzo ya nchi 29 zilizohudhuria Kongamano hilo: (Afghanistan, Algeria, Yemen, Myanmar, Cambodia, Sri Lanka, Congo. , Cuba, Cyprus, Misri, Ethiopia, Ghana, Guinea, India, Indonesia, Iraq, Lebanon, Mali, Morocco, Nepal, Saudi Arabia, Somalia, Sudan, Syria, Tunisia, Yugoslavia).
Waanzilishi wake wa kwanza walikuwa: Rais wa Misri Gamal Abd El Nasser, Waziri Mkuu wa India Jawaharlal Nehru, Rais wa Yugoslavia Tito, na mwishowe Rais wa Indonesia Ahmed Sukarno, na ilianzishwa kutokana na vita baridi vilivyozuka kati ya mataifa makubwa mawili wakati huo nayo ni: NATO. ikiongozwa na Marekani, ikiwakilisha kambi ya Magharibi (ya kibepari), na WARSO ikioongozwa na Umoja wa Kisovieti, ikiwakilisha kambi ya Mashariki (ya kikomunisti); kuzuia sera zilizosababisha vita hivyo, na wakati wa Vilele 19 vilivyofanyikwa kutoka 1961 hadi 2020 mara kwa mara, takriban kilele kimoja baada ya miaka 3 mfululizo, na cha hivi karibuni zaidi ni kilele wa Mei 4, 2020, kwa mpango wa Kiazabajani, Mwenyekiti wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote "Ilham Aliyev" kipindi cha (2019-2022), ambapo kilishughulikia kimsingi mapambano ya kimataifa ya kukabiliana na Janga la Covid-19 na kukuza Harakati ya Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote ili kuongeza mchango wake katika kushughulikia na kupunguza athari zinazosababishwa na Janga hilo katika utendakazi wa Mwenendo wa kazi za Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote.
Kweli, Harakati hiyo imekuwa na nafasi kubwa katika kuendelea Amani na Usalama wa kimataifa, Kushinda ukoloni, pia kuunda mataifa mapya yakijishughulisha masuala yao binafsi, na mnamo kipindi cha zaidi ya miaka 60, hadi 2020, idadi ya nchi wanachama wa Harakati hiyo imefikia zaidi ya 118, Na timu ya ufuatiliaji inayojumuisha takriban nchi 17 na taasisi 11.
Dhana ya kutofungamana kwa upande wowote: Ni Msamiati wa kisiasa uko na maana ya sera ya nchi zisizofungamana kwa upande wowote, pia zinakataa kufuata sera ya upendeleo kuelekea nchi moja kubwa kutoka zinazopingana, kwa maana nyingine, ni kundi la nchi za mwelekeo mmoja wa kisiasa, ukiwa na lengo la kuthibitisha uhuru wao dhidi ya mataifa makubwa mawili.
Nchi za Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote zilizingatia kanuni 10 za kimsingi, nazo ni:
1-Kuheshimu haki za kimsingi za binadamu na Malengo na kanuni za Hati ya Umoja wa Mataifa.
2-kuheshimu Udhibiti wan chi zote na Amni yao.
3-Kutojihusidha au kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.
4-Kuheshimu haki ya kila nchi kujitetea, kibinafsi au kwa pamoja, kwa mujibu wa Hati ya Umoja wa Mataifa.
5-Kanuni mbili za :
A- Kutoingia katika ushirikiano wa kijeshi na nchi kubwa.
B- kutotoa shinikizo kutoka nchi Fulani kwa nyingine.
6-Kujizuia kutishia au kufanya uchokozi wowote, dhidi ya Amani ya kikanda au uhuru wa kisiasa wa nchi yoyote.
7-Suluhisho la Amani kwa migogoro yote ya kimataifa, kwa mujibu wa Hati ya Umoja wa Mataifa.
8-Kukuza maslahi na ushirikiano wa pamoja.
9-Kuheshimu Uadilifu na wajibu wa kimataifa.
10-Kuidhinisha kanuni ya usawa kati ya jinsia zote, na usawa kati ya nchi zote kubwa na ndogo.
Wakati Mkutano wa Kairo mwaka wa 1961 uliidhinisha na ukatoa malengo muhimu zaidi ya harakati kama ifuatavyo:
*Kuunga mkono haki ya Hatima, uhuru wa kitaifa, Utawala na uongozi wa kikanda kwa nchi.
*Upinzani wa ubaguzi wa rangi.
*Kutofungamana kwa miungano ya kijeshi ya pande nyingi, na nchi za Harakati Zisizofungamana kwa upande wowote zikae mbali kutoka kwa mikusanyiko na mizozo kati ya nchi kubwa.
*Kupambana dhidi ya ukoloni kwa namna zake zote , pia kupambana na uvamizi, ukoloni mamboleo, ubaguzi wa rangi, utawala wa kigeni na upokonyaji silaha.
*Kutoingilia mambo ya ndani ya nchi.
*Kuishi pamoja kati ya nchi zote, kupinga nguvu au tishio kupitia kuzitumia katika mahusiano ya kimataifa, na *kukuza Umoja wa Mataifa.
*kukuza demokrasia kwa mahusiano ya kimataifa.
*Maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
*Kufanya upya kwa mfumo wa uchumi wa Dunia.
*Ushirikiano wa kimataifa kwa usawa.
magharibi ukiongozwa na Marekani ukiwa na NATO), na ( Kambi ya mashariki ikiongozwa na Umoja wa Kisovieti ukiwa na WARSO).
Rais wa Misri Gamal Abd El Nasser amekuwa mmoja wa waanzilishi wa harakati hiyo, pamoja na Waziri Mkuu wa Uhindi Jawahr Lal, Rais wa Yugoslavia Tito na Rais wa Indonesia Ahmed Sokarno.
Harakati hiyo inalenga kulinda Usalama na Amani Duniani kote kushinda Ukoloni kabisa, kuhakikisha Uadilifu kati ya Nchi zote, kuheshimu wanachama wote, kuimarisha maslahi ya pamoja na kuheshimu haki za binadamu
Nchi nyingi zimeshiriki katika harakati hiyo kutoka Mabara mbalimbali, lakini nchi maarufu zaidi zinazoshiriki kutoka bara la Afrika zimekuwa kama vile :
Madagascar, Senegal, Malawi, Algeria, Angola, Misri, Shelisheli, Sierra Leone, Eritrea, Somalia, Mauritania, Ethiopia, Afrika Kusini, Mauritius, Sudan, Morocco, Kenya, Tanzania, Burundi, Visiwa vya Comoro, Zimbabwe na nchi nyingine za Afrika