Hemat Mostafa.. Ni wa kwanza aliyesoma Taarifa ya habari kwenye runinga ya Misri

Hemat Mostafa Ismael alizaliwa mnamo Januari 12, 1927, mjini Mit Ghamr uhuko Mkoa wa Al-Dakahlia, Baba yake Mzee Mostafa Ismael, ndiye ni msomaji wa kwanza wa Misri, msomaji wa Ikulu ya Abdeen na msomaji wa mfalme Farouk.
Hemat alipata shahada ya kwanza ya Sanaa, sehemu ya Historia kutoka Chuo Kikuu cha Kairo mwaka wa 1950, kisha alijiunga na Redio mwaka wa 1951 kama mtangazaji wa programu za kiarabu, na alikuwa mwanafunzi wa mtangazaji wa programu za kisiasa kwa muda mrefu, Hossny Al-Hadidi, miongoni mwa programu hizo ni « Wiki ndani ya Saa Moja».
Hemat, alisafiri Syria mwaka wa 1958 , ili kutoa sherehe za Adwaa El-Madina huko Damascus, kisha alielekea Ujerumani katika Udhamini wa kimasomo kwa muda wa miezi miwili mnamo 1960 , na mnamo mwaka huo huo Misri ilichukua hatua ya kuanzisha runinga ya kimisri na alichaguliwa miongoni mwa watangazaji wa kwanza watakaofanya kazi ndani yake , na alikuwa mtangazaji wa kwanza kutazamwa na watu runingani , na pia alikuwa mtangazaji wa kipekee ndani ya televisheni na idhaa ya kimisri mnamo wakati huo, na alipewa tathmini kubwa na Rais Gamal Abdel Nasser ، na alisimamia kituo cha pili cha runinga wakati wa kuanza kufanya kazi katika televisheni mwaka 1962 , kisha alipandishwa cheo na kuwa mkurugenzi wa programu za kuwaelekeza watu mnamo Julai ya mwaka wa 1965, hayo ni pamoja na usomaji wake wa Taarifa ya Habari huko Idhaa .
Na mwanamke huyo aliteuliwa kama mtaalamu wa programu ndani ya Muungano wa Idhaa za Kiarabu,kwa hiyo anachukuliwa kama mwanamke mwarabu wa kwanza ndani ya Idhaa za Mashariki ya Kati anayeshika nafasi ya Mtangazaji mkuu.
Miongoni mwa mipango muhimu zaidi aliyezitoa kwenye runinga ni "Khali Balak", "Ala Shat Al Nile na programu ya mashindano "3×3" pamoja na baadhi ya mipango ya kisiasa kama vile programu ya "Mishumaa Minane"; alikuwa akionesha kazi maarufu zaidi za mapinfuzi ya Julai 23 mnamo miaka minane iliyopita kutoka maisha yake na mada za programu hii zilikusanywa na Hemat Mostafa kutoka historia yetu iliyooneshwa kwenye filamu, na Gazeti la Filamu la Misri,na kutoka mada nyingine zilizotolewa na Taasisi kuu ya Taarifa.
Miongoni mwa safari muhimu zaidi alizozifanya ni kutembelea Ufalme wa Saudi Arabia mwaka wa 1964 ili kutangaza Msimu wa Hajj.
Hayati Rais Sadat alitaka kufuata nyayo za Hayati kiongozi Abdel Nasser, hivyo alimweka uangalifu maalum na na alimtoa maongezi yake mengi na waandishi wa habari aliwasilisha Rais katika mipango ya moja kwa moja kwa umma wa Misri kutoka mji wake,Mitt Abu Al_koum, mkoa wa Menoufia, katika sherehe nyingi tofauti,maarufu zaidi ni siku yake ya kuzaliwa, Wakati mwingine Sadat alikuwa akionekana katika mazungumzo yake huvaa Sare na Buibui,na mikutano hiyo ilikuwa maarufu kwa kusema:"Hemat,binti yangu" ambayo Sadat alikuwa kurudiarudia kwa mwanamke wa vyombo vya habari wakati wa mkutano.
Mnamo 1978,Hemat Mostafa akawa Mwakilishi wa Televisheni ya Misri na Mkurugenzi mkuu wa mambo na habari ya kisiasa, kisha akawa Mkuu wa televisheni kuanzia Mei hadi Desemba 1980.
Na mnamo 1993,Hemat Mostafa alipata wadhifa wa Mkurugenzi wa utangazaji katika mtandao wa Redio na Televisheni ya Kiarabu nchini Italia,Na aliwafundisha watangazaji wengi wa kike.
Bi.Hemat Mostafa alifariki Dunia mnamo Desemba 14,1995.
Vyanzo
Gazeti la Al-Ahram la Misri.
Gazeti la Al-Akhbar Al-Youm la Misri.