Mwanahistoria Profesa Mostafa El-Abbadi

Mwanahistoria Profesa Mostafa El-Abbadi
Mwanahistoria Profesa Mostafa El-Abbadi

Mostafa Abdel Hamid El-Abbadi alizaliwa mnamo Oktoba 10, 1928, huko Aleskandaria. Alikua katika nyumba kubwa miongoni mwa nyumba za elimu , ambapo Baba yake, mwanahistoria Abdel Hamid Abdel-Abbadi, ni profesa wa historia na Ustaarabu wa Kiislamu na mkuu wa Kitivo cha Sanaa, Chuo Kikuu cha Aleskandaria.

Alipata Shahada ya Kwanza ya Sanaa kutoka Sehemu ya Historia katika Chuo Kikuu cha Aleskandaria mnamo mwaka 1951 BK, kisha akasafiri kwa Uingereza ili kupata Shahada ya Uzamivu ya Ustaarabu wa Kigiriki na Kirumi kutoka Chuo Kikuu maarufu cha Uingereza cha Cambridge mnamo mwaka 1961 BK.

Al-Abbadi alirudi kwa Chuo Kikuu cha Aleskandaria na alianza kazi yake ya kitaaluma, ambapo alifundisha kwenye chuo kikuu, akifuata nyayo za baba yake. kisha Alijumuishwa katika vyeo vya ualimu hadi alipopata uprofesa mnamo 1972, na akawa Mkuu wa Sehemu ya Mafunzo ya kigeriki-Kirumi mnamo mwaka huo huo, kisha akawa Makamu Mkuu wa Chuo cha Sanaa kwa Masuala ya Wanafunzi kutoka 1976-1979.

Alishikilia vyeo vyengi katika taasisi kuu za kisayansi, ikiwa ni pamoja na:

 • Mwanachama wa Chuo cha Sayansi cha Misri.

•Rais wa Jumuiya ya Mambo ya Kale huko Aleskandaria.

Mwanachama wa mamlaka ya Kimataifa ya Papyrus katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.

• Mwanachama  wa Jumuiya ya Amerika ya Mafunzo ya Papyrus huko mjini New York .

• Mwanachama mwangalizi wa Baraza la Kimataifa la Mafunzo ya Falsafa na  kibinadamu.

•Mwanachama wa baraza la  idara ya Jumuiya ya kimisri kwa Mafunzo ya Kihistoria (1977-1979).

•Mwanachama wa Jumuiya ya kimisri ya Mambo ya Kale ya Coptic.

•Mwanachama wa kamati za maandalizi kwa mradi wa kufufua Maktaba ya zamani ya Aleskandaria, ambaye alikuwa mmiliki wa kweli wa wazo la ufufuo wake .

•Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Ufufuo wa Maktaba ya Kale ya Aleskandaria.

•Mjumbe wa Kamati Kuu ya Historia na Mambo ya Kale kwenye Baraza Kuu la Utamaduni nchini Misri.

•Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Kale ya kimisri na Greco-Roman kwenye Baraza Kuu la Mambo ya Kale la Misri.

Al-Abbadi alijali sana  maktaba ya Aleskandaria  kwa kuzingatia ni kama maktaba ya kwanza ya kimataifa iliyojengwa katika Misri ya kale, na ilikuwa na takriban vitabu nusu milioni vya nchi na lugha mbalimbali, hadi ikawa rejeleo la juu katika suala hili na alitoa mihadhara juu ya Maktaba ya Aleskandaria katika maeneo kadhaa ulimwenguni na  alisajili  matokeo yake pia utafiti wake kwenye kitabu  kilichopendezwa na wakosoaji.

Al-Abbadi  alikuwa akihimiza mara kwa mara katika mihadhara yake kwa  kuanzishwa upya kwa maktaba hiyo kubwa ya kimataifa, naye alikuwa mwanzilishi wa wazo la kufufua Maktaba ya zamani ya Aleskandaria na kuanzisha Maktaba mpya ya Aleskandaria. vilevile , Aliweza kushawishi serikali ya Misri na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuunga mkono mradi wake.

Baada ya karibu miaka kumi na tano ya  utengenezaji  na ujenzi , mkataba ya Aleskandaria ilifungua milango yake mnamo mwaka wa 2002 AD.

Alishiriki katika makongamano mengi ya kimisri na kimataifa, na alitunga vitabu kadhaa, vikiwemo:

• Kitabu cha kimarejeo.

• Kitabu cha Maktaba ya Kale ya Aleskandaria, ambacho kilichapishwa na Maktaba ya Anglo mnamo 1977 AD, na kilipewa zawadi kwa roho ya baba yake, Profesa Abdul Hamid Al-Abbadi. Kutokana na kusoma kitabu hiki, inabainika kiasi gani cha uhai na shughuli  ya Aleskandaria ya kale katika katika nyanja za mawazo, utamaduni na sayansi.

• Kitabu cha Misri kutoka kwa Alexander Mkuu hadi Ushindi wa kiarabu.

Alexandria of Library Ancient the of fate and life  , kilichochapishwa na UNESCO, kilifsiriwa kwa Kifaransa, Kijerumani na Kihispania, na pia kuchapishwa kwa Kiarabu. pamoja na Misri, wafalme wawili wa roboti, na tafsiri ya Cairo,mkoa wa sanaa na biashara - kilichoandikwa na Gaston Fitbit.

Tafiti zilichapishwa katika majarida na magazeti ya kisayansi, au katika shughuli za  makongamano ya kimataifa, kikanda na ya ndani:

•chimbuko cha   Fikra ya Historia na maendeleo yake ," Ulimwengu wa Mawazo, (Kuwait) 2001 AD.

• "Demokrasia ya Athene", Ulimwengu wa Mawazo, Kuwait, 1992.

The making of world map : " bull of the  bibliotheca Alexandria, the problem of   the senete of  Alexandria, bull of  arch.souiety of 

Alexandria (1994)

 

Dkt. Mostafa alitunukiwa Tuzo ya Kafafi katika Masomo ya Kigiriki mnamo mwaka 1997  ,Tuzo ya Kuthaminiwa toka  Serikali katika Sayansi ya Jamii  mnamo mwaka 1998, na Tuzo ya Nile ya Sayansi ya Jamii mnamo  mwaka 2013, ambayo ni tuzo  kubwa zaidi ya kila mwaka iliyotolewa na Baraza Kuu la Utamaduni nchini Misri.

Dkt. Mostafa Al-Abbadi alifariki Dunia Jumanne,  tarehe 14 ,Februari , mwakani 2017.