Mahdi Al_ Manjara

Mwanachumi na Mwanasosholojia wa Morocco katika masomo ya Siku zijazo na kazi yake kubwa ilikuwa utafiti na kusoma juu ya mustakbali wa ulimwengu na binadamu.
Al_ Manjara alizaliwa mnamo Machi 13, 1933 katika mji wa Rabat, Morocco, alipata elimu yake ya msingi katika shule ya wana wa watajiri wa kiislamu , Alijifunza lugha ya kiarabu nyumbani kwa msaada wa Idris El_ Kenani na Mostafa El_ Gharboui , na aliingia shule ya sekondari ya Leouti katika
El_ Dar Elbaydaa na alikuwa akipinga idara yake na upinzani wa kudumu na walimu wa Ufaransa; kwa sababu ya ukataaji wake wa wazo la ukoloni wa Ufaransa nchini mwake. Baba yake aliamua kumpeleka mnamo 1948 kwa Marekani; ili kutimiza masomo yake, na huko alipata mafanikio katika Biolojia na Kemia, vilevile katika elimu za kisiasa katika Chuo Kikuu cha Marekani cha Conel na alihamia kufikia London mnamo 1954; ili kuendelea katika elimu yake, na alipata shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha London na maudhui yake ulikuwa kuhusu Lugha ya kiarabu .
Mahdi alishika nyadhifa nyingi tofauti nchini Morocco na nje ya nchi, Mfalme Mohamed Al_ Khames alimpokea mnamo 1959 kama profesa wa kwanza wa Morocco katika Kitivo cha sheria huko Rabat na profesa mdogo zaidi huko na akamteua Mkurugenzi wa redio na televisheni ya Morocco, alirudi London mnamo 1970, na alifanya kazi kama Mhadhiri na Mtafiti katika masomo ya kimataifa, katika Kitivo cha Sayansi za kiuchumi katika Chuo Kikuu cha London. Alitawala kazi ya Mshauri maalum wa Mkurugenzi mkuu wa UNESCO, na alikuwa Mshauri wa kwanza wa ujumbe wa kudumu wa Morocco katika Umoja wa mataifa.
Al_ Mahdi Al_ Manjara aliacha kazi kutoka mashirika ya kimataifa; kwani mtazamo wake wa kisiasa unapinga mawazo yake, ambapo alikuta kuwa yanafanya kazi kwa huduma ya masilahi ya nchi kubwa tu, na baadaye alirudi nchi yake, na alifanya mwenendo wa kisayansi na mawazo yake kwa ajili ya kuchambua matatizo ya kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni ya nchi changa na kuweka njia ya mbadala ya maendeleo ya siku za usoni inayochangia kuhifadhi maadili ya kiutamaduni na kuacha kufuatilia nguvu katili ya ubepari na kutambua mafanikio ya ustaarabu wa kisasa.
Al_ Mahdi Al_ Manjara alitunga vitabu vingi muhimu vinavyohusiana utandawazi, maendeleo ya kiuchumi na vingine , vitabu hivi pia vilitafsiriwa kwa zaidi ya lugha kumi , na vitabu vyake viliuzwa zaidi nchini Ufaransa kati ya 1980 hadi 1990, Na miongoni mwa vitabu vyake maarufu sana ni vita vya kwanza vya ustaarabu , Utusi katika enzi ya Mega ya kibepari, utandawazi wa utandawazi, thamani ya maadili na mawasiliano ya mazungumzo. Maktaba ya Al_ Mahdi Al_ Manjara ilikuwa na vitabu 5,566, magazeti 808, CD 788, na picha nyingi na mabango.
Katika mwenendo wa kazi yake, Al_ Manjar alipata tuzo na Nishani nyingi, ambapo huko Morocco alipatia medali ya ufalme katika sherehe nyingi, na alipata tuzo kutoka mfalme wa Japan kwa utafiti wa umuhimu wa mfumo wa Japan kwa nchi changa
na alipata tuzo ya maisha ya kiuchumi mnamo 1981, medali kuu ya chuo cha ujenzi cha Ufaransa mnamo 1984, Medali ya sanaa na fasihi huko Ufaransa mnamo 1985, Medali ya Jua linayong'aa huko Japan 1986, medali ya Amani kutoka chuo cha Albert Einstien cha kimataifa , na tuzo la mafunzo ya mustakbali la shirikisho la kimataifa mnamo 1991.
Mahdi Al_ Manjara aliaga Dunia mnamo Juni 13, 2016, na mkewe baada ya kifo chake alitoa maktaba yake ya kibinafsi kama mchango kwa maktaba ya ufalme wa Morocco ya kitaifa huko Rabat.