Mpilo Desmond Tutu Mpigania Haki Anayetabasamu

Mpilo Desmond Tutu Mpigania Haki Anayetabasamu

Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled  


Mmojawapo wa wapigania kwa haki walio maarufu zaidi kwenye mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, mwenye harakati za kitaifa, mwenye suala linalozuka utata mkubwa sana , mfano wa Mandela, aliye rafiki yake kwa siku nyingi,  pia ni mtu anayeunga mkono sana wapalastina,  mtetezi mkuu wa suala la Palastina, akilizungumzia kuukumbusha ulimwengu nalo , kwenye majukwaa muhimu zaidi ya kimataifa, pamoja na kupata tuzo ya Nobel ya Amani mnamo mwaka wa 1984 , ili kuzisifu juhudi zake za mapambano, jambo  lililikuwa kama pigo kali kwa jamii ya kimataifa kwa Viongozi weupe wa Johannesburg , na vilevile ni nafasi nzuri ya kuwapa weusi haki zao zote za kiraia. 

Mkuu wa Maaskofu " Mpilo Tutu" hajakosa hamu yake ya kuhakikisha ushindi wa suala lake kwa Amani tupu na tabia nzuri, ambapo alikuwa mtu wa  uwajibikaji , kupigania haki na kuwasapoti waathirika wa vurugu na ubaguzi wa rangi, na licha ya haya yote alijulikana na kicheko chake chenye  kuleta furaha na kisichomfariki hadi alipofariki leo  akiwa na umri wa miaka 90  .

" Desmond Tutu" amezaliwa mnamo mwaka wa 1931 , kwenye kijiji kidogo karibu na jimbo la "Transefal" , halafu akajiunga na kanisa na alijifunza Falsafa, Saikolojia na Lahut , kisha akaendelea kupata masomo yake kwenye chuo kikuu cha London, halafu alifanya kazi kama mwalimu lakini aliiacha kazi hiyo tangu kutungwa kwa sheria ya Elimu ya "Bantu" mnamo mwaka 1953, sheria ambayo ilisababisha ubaguzi wa rangi shuleni wakati huo, halafu aliteuliwa kuwa padri wa kanisa ambapo alikutana na mapadri wengi waliokuwa wanaomb  haki za binadamu na  kuacha vurugu, jambo ambalo lilikuwa mwanzo wake wa kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Tutu" Alipata nafasi ya kuwa mwenyekiti mweusi wa kwanza wa Kanisa la Anglican huko Johannesburg mwaka 1975 , halafu alipandishwa cheo mara nyingi kadhaa na miongoni mwa nafasi alizopata , kuwa mwenyekiti wa kamati ya ukweli na maridhiano, ambapo alikuwa na kazi ya kuchunguza uhalifu uliofanywa wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi , na kutoa mapendekezo kuhusu wahalifu hao, lakini kamati hiyo haikufanya kazi yake kama inavyotarajiwa, huenda kwa sababu ya matatizo yaliyoikumba wakati huo.

Pia aliishughulikia nafasi ya mkuu wa Maaskofu wa kanisa la Anglikana, na mnamo mwaka 1988 , alipokataa sura zote za vurugu zinazofanyika na serikali iliyokuwa inawabagua weusi, akisema : " Tunakataa kuwa watumwa wa serikali " 
Ambapo alikuwa kama jinamizi kwa wakoloni wa Israel, na inasemekana kuwa alisema " vipi wayahudi hawa wanaweza kuwatesa vibaya wapalastina" !!!

Kiongozi yule hajaogopa kusema haki hata mbele ya kiongozi mwenye dhuluma ، bali aliisema nchini mwake , ambapo wakati wa ziara yake kuelekea uingereza mnamo aprili 1989 , alisifu uingereza kwa " uingereza wenye nyuso mbili" akionyesha ustajaabu wake kwa kuwa ni nchi inayotaka kuhakikisha uhuru na magereza yake yamejaa wafungwa waafrika.

Pamoja na kupata tuzo ya Nobel, "Tutu" Alipata pia tuzo maarufu ya " Templeton" inayoleng kuwaheshimu watu walioacha athari wazi katika kuthibitisha ukweli wa uwanja wa vipimo vya roho vya maisha , ambapo hakuna tukio   linaweza kushinda tukio hilo la kufariki kwa Tutu , anayezingatiwa kama sauti ya weusi huko Afrika kusini , na alama ya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi uliofanywa na weupe kiasi kwamba  ulifutwa na demokrasia tangu zaidi ya miaka 30 , ambapo hawajakata tamaa katika kuhakikisha ukombozi kwa bara letu , kwa roho yao tukufu, Rehema na amani.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy